Serikali kupeleka Bungeni muswada wa mapendekezo ya kutunga sheria ya tasnia ya uanasheria

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,353
Serikali kupeleka Bungeni muswada wa mapendekezo ya kutunga sheria ya tasnia ya uanasheria

0.png


MAENEO MAHSUSI YA SHERIA INAYOPENDEKEZWA KUTUNGWA KUHUSU TASNIA YA UANASHERIA NCHINI
1. Kuunda chombo kitakachojulikana kama Bodi ya Usajili wa Wanasheria, au Baraza la usajili wa Wanasheria, kusimamia taaluma ya sheria nchini na kutekeleza majukumu ya sheria kwa kushirikiana na Jaji.

2. Kushughulikia maombi ya usajili na kutunza daftari la watu wote wanaofanya kazi katika tasnia ya sheria

3. Kudhibiti watumishi wa umma kujishughulisha na masuala ya mawakili binafsi ikiwa ni pamoja na uwakilishi wa watu binafsi mahakamani, viapo na kudhibiti nyaraka mbalimbali

4. Kutoa na kufuta leseni za uwakili kwa kushirikiana na Jaji Mkuu

5. Kupokea malalamiko na kufanya uchunguzi, kushughulikia masuala ya nidhamu ya wanasheria na kuchukua hatua kwa kushirikiana na Jaji Mkuu, na kwa wanasheria walio katika utumishi wa umma, Wizara na taasisi za Serikali kwa mujibu wa sheria za Utumishi wa umma

6. Kuendeleza, kukuza, kuchunguza, kusimamia, kupitisha, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa majukumu ya wanasheria nchini

7. Kuboresha elimu ya sheria kwa kushauriana na taasisi zinazoshughulikia maendeleo ya elimu ya sheria nchini.

8. Kuainisha viwango vya ada, michango na tozo kwa kazi ya Wakili na taratibu za ulipaji wa ada, michango na tozo hizo

9. Kufanya ukaguzi katika ofisi za Mawakili kujirisdhisha iwapo zinakidhi matakwa ya sheria

10. Kushirikiana na taasisi zinazosimamia masuala ya elimu katika kuhakiki vyeti vya taaluma ya uanasheria na mafunzo endelevu ya elimu ya sheria nchini

11. Kuwawezesha watu walio katika tasnia ya sheria kujisajili katika taasisi za eneo la ubobevu za kitaifa, kikanda na kimataifa

12. Kushughulikia masuala ya utangamano wa kikanda na kimataifa na kutoa miongozo kuhusu masuala hayo

13. Kuondoa katika daftari jina la Wakili kwa kushirikiana na Jaji mkuu kutokana na sababu mbalimbali zinazoweza kutokana na;
A. Kufariki dunia.

B. Kushindwa kufanya kazi za uwakili katika Jamhuri ya Muungan kwa sababu zozote ikiwa ni pamoja na kushindwa kufanya shughuli za uanasheria kwa muda wa zaidi ya miaka mitano (5)

C. Kushindwa kupata alama za elimu endelevu ya sheria zinazotakiwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili (2); na kuondolewa chini ya aya (b) na (c) hapo juu kunaweza kubatilishwa iwapo muhusika atafanya maombi na kubainisha sababu zilizopelekea kuwepo kwa tukio lililosababisha kushindwa kutekeleza masharti ya sheria.​

14. Kuweka masharti ya kuanzisha na kufungua ofisi za uwakili zinazomilikiwa kwa ushirika (law firms) ama makampuni

15. Kuhusisha sheria zinazosimamia tasnia ya uanasheria nchini zikiwemo Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (Utekelezaji wa Majukumu), Sheria ya Mawakili, Sheria ya Chama cha Wanasheria Tanganyika, Sheria ya Maafisa wa Viapo, Sheria ya Taasisi ya Uanasheria kwa Vitendo na Sheria ya Usimamizi wa Mahakamani.
 
Serikali kupeleka Bungeni muswada wa mapendekezo ya kutunga sheria ya tasnia ya uanasheria

Naunga mkono hoja wawe na bodi kama za madaktari mainjinia wahasibu nk ambayo itaweza kutoa leseni kusimamia utendaji wao kitaalaamu na kuwanyabganya leseni wakionekana wamechemka. Hiki ki club kisichokuwa na meno kids NGO kinachoitwa chama cha wanasheria kibakie cha hiari Kama club anayetaka ajiunge asiyetaka aache sababu siyo proffessional body
 
Mkuu, jambo hilo nimeliona na, kama mdau, najitahidi kulifuatilia.

Naogopa kama State Attorneys wetu ni wale waliotuingiza kwenye UHUJUMU uchumi wa raslimali zetu,basi tumekwisha kama TAIFA siku CCM wakiondoka hatutakuwa TAIFA tena nadhani tunakitu kingine tunatakiwa tuanze kujiita
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom