Serikali kupeleka Bungeni muswada wa mapendekezo ya kutunga sheria ya tasnia ya uanasheria

Kwa vipengele tajwa japo juu, naona TLS ya kina Tundu Lissu inaelekea
hali jojo. ni suala la muda tu nawaambieni.

Soma vizuri vipengele vya hapo mapendekezo kisha tafakari mara 2 mbili.
Haitamuathiri Lissu peke yake bali wanasheria wote. Hii ni ya kupinga na kuogopa sana.
 
Kwamba ndo ile kauli ya "tutaifuta Tanzania law society"??????
Kazi zote za TLS zimehamishiwa kwenye hiyo bodi mpya nadhani hiyo sheria mpya inakwenda kurepeal TLS Act na huo ndiyo mwisho wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kilichodumu kwa nusu karne sasa!
 
Hivi Lisu akiacha uwakili bado sharia hii itakuwa inafanyakazi? waache kutunga sharia kwaajili ya mtu mmoja..... Grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Hii nchi haitakuja endelea kama wale watu wa kijani wataendelea kuwa wengi vile, siku zote watatuamulia kule wanapotaka sisi twende
 
serikali ina nia ya kupoka mamalaka ya TLS na kuendeleza upambuvu wa kimabavu.

Kabudi anashiriki kwenye huu ujinga it will hunt him till his death.
 
Hapo anatafutwa mtu mmoja au wawili tu ili akomeshwe. Mambo ya serikali yetu ikiongozwa na wanasheria wake!
 
Napata ukakasi kwenye kipengele cha 3....kuna nia njema kweli kudhibiti watumishi wa umma kujishughulisha na uwakilishi wa watu mahakamani & affidavits. Serikali inahofu nini? Je kuna mgongano wowote wa kimaslahi kati ya mtumishi na serikali katika hzo mambo?
 
Kazi zote za TLS zimehamishiwa kwenye hiyo bodi mpya nadhani hiyo sheria mpya inakwenda kurepeal TLS Act na huo ndiyo mwisho wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kilichodumu kwa nusu karne sasa!
Hakuwa TLS act acha uongo
 
Yote hiyo ni kwa ajili ya kuiharibu TLS,kwani mafisiemu ni wengi bungeni,hivyo ni lazima ipite.
 
Naamini rais ajaye atazibadilisha sheria nyingi sana zinazotungwa awamu hii ya tano! Maana zinatungwa kwa mihemuko na nia ya kukomoa mtu fulani au kundi fulani, kitu ambacho tukipata rais wa hekima atazifutilia mbali
 
Naamini rais ajaye atazibadilisha sheria nyingi sana zinazotungwa awamu hii ya tano! Maana zinatungwa kwa mihemuko na nia ya kukomoa mtu fulani au kundi fulani, kitu ambacho tukipata rais wa hekima atazifutilia mbali
Mpaka sasa kuna sheria ngapi zimeletwa chini ya Magufuli?
 
Kufuatia mchakato wa kuifuta TLS na kuanzisha Bodi ya kitaaluma ya sheria ulioanzishwa na Serikali ninashauri wanasheria kuungana kuipigania haki yao maana wakikubali chama hili cha Wanasheria wa Tanganyika kilichodumu kwa zaidi ya nusu karne sasa toka mwaka 1955 watakuwa wamekubali kujikabidhi mikononi mwa serikali na zaidi mikononi mwa CCM.

Nchi zote za Afrika mashariki na za Jumuiya ya madola wana Bar associations na siyo bodi kama serikali inavyotaka kufanya. Sheria ni noble profession ni tofauti na taaluma zingine kama uhasibu nk ni lazima tulinde autonomous tuliyonayo chini ya TLS. Chama hiki kina historia ndefu sana kwa nchi hii hakiwezi kufa kifo cha mende.

Nashauri TLS iitishe mkutano wa dharula wa wanasheria haraka sana kujadili hili swala na kutoka na maazimio yatakayotoa mwelekeo na msimamo madhubuti wa kupinga hili swala.
 
Back
Top Bottom