Serikali kupandisha ushuru wa mkaa kulinda mazingira

Ukaridayo

JF-Expert Member
Oct 8, 2012
507
469
By Professor Maghembe

Biashara ya mkaa hivi sasa inaendeshwa na watu mbalimbali, mkaa unasafirishwa hadi zanzibar ukifika zanzibar unasafirishwa kwenda nje...

Sasa tutaweka kodi kubwa kwenye mkaa na watashindwa kuupata kwa urahisi.

Ili tulinde misitu yetu na utunzaji wa mazingira yetu.

Taasisi za serikali zinazotumia kuni na mkaa sasa zibadilike badala yake watumie mfumo wa gesi.
 
We ngeke wambie jamaa zako wapunguze bei ya gesi

OVA
Wakati bavicha wanahubiri maisha magumu, lindi na mtwara wana fedha nyingi hadi wananunulia na kunywesha soda Mbuzi

Bavicha jamani achaneni na kazi ya kufua nguo za Lowasa hailipi tena

La sivyo maisha yatazidi kuwa magumu kwenu
 
Wapandishe kabisa misitu sasa hivi inazidi kuwa majangwa kasi ya ajabu kuna milima kule sengerema miaka 95 ilikuwa mapori lakini sasa hivi yamebaki mawe tu peupe inatakiwa mkaa uzuiliwe kuingia mjini wa mjini tukazane na ges mkaa ubaki kijijini kwa sababu matumizi ya mkaa asilimia kubwa ni mjini
 
ac427600ae1a0295bced5d8a67f56919.jpg
 
Huo ni muendelezo wa kukurupuka hawajifunzi tu! Ni kama kupandisha bei ya mafuta ya taa
 
Kuna hatua tusipochukua sasa hivi vizazi vijavyo vitaikuta Tanzania ni jangwa ..huku kukata miti hovyo kupigwe marufuku ila pia serikali iangalie uwezekano wa kufanya gesi ni bidhaa ya kawaida sio luxury ila kila mtu aweze kuitumia
 
Wafute kodi zote kwenye gase,ili gase iwe nafuu kuliko mkaa,haiitaji uwe na akili sana kujua hilo,lakini hawalioni sijui makusudi au madharau kwakuwa wao hawaguswi na maisha ya watu wa kipato kidogo
 
By Professor Maghembe

Biashara ya mkaa hivi sasa inaendeshwa na watu mbalimbali, mkaa unasafirishwa hadi zanzibar ukifika zanzibar unasafirishwa kwenda nje...

Sasa tutaweka kodi kubwa kwenye mkaa na watashindwa kuupata kwa urahisi.

Ili tulinde misitu yetu na utunzaji wa mazingira yetu.

Taasisi za serikali zinazotumia kuni na mkaa sasa zibadilike badala yake watumie mfumo wa gesi.
Hapa angalau wamenena lakini sio maamuzi kama la lile mama kwenye elimu.
 
Huyu nae waziri ivi anachokiongea anajielewa kweli ...................Punguza bei ya gesi iwe ndogo kuliko mkaa then uone kama mkaa utapata soko
 
Kulinda mazingira au kuwanyonya wananchi wake masikini?? Umeme bei juu, gesi bei juuu, alafu kwa upumbavu serikali inashangaa eti kwanini watu wanatumia mkaa. Pumbavu kabisa.
 
Inashangaza wanapandisha kodi ya mkaa kudiscourage hiyo biashara halafu kwenye gas na umeme nako wanabana, wanataka tupikie nini?
 
Huyu nae waziri ivi anachokiongea anajielewa kweli ...................Punguza bei ya gesi iwe ndogo kuliko mkaa then uone kama mkaa utapata soko
Gesi imeshuka kidogo mtungi niliyoununua kwa 50000 sasa nanunua kwa 40000
 
Back
Top Bottom