Serikali kupandisha ushuru wa mkaa kulinda mazingira

mafuta ya taa walitupandishia bei kwa kisingizio yanatumika kuchakachua mafuta ya magar yao wakaona watuangamize wapikia mchina tukakimbilia mkaa...huku nako wametufata hivi wanataka tuishije au ndo waliposem tutaishi kama mashetan hii pia ni namna yao ya tuishi kama mashetani?,

Anakuja mtu mzima anatetea sijui anafikilia kwa kutumia mata**,kabla huja support kwanza uliza kuna njia gani mbadala wametupatia wapikia mikaa,Umeme hatuwez kupikia,Gas hatuna uwezo watupe alternative bhas au kaa washushe bei za nishat nyingine.

Kuna faida gan kusema unatunza mazingira huku raia wanakufa wakikosa namna ya kuishi labda mnawatunzia mazingira wazungu!,nipe mbadala uone kama nitapikia mkaa au mnadhan tunapenda jinsi mkaa unafanya macho yetu yanakuwa mekundu kama tunavuta bangi!
 
Wapandishe kabisa misitu sasa hivi inazidi kuwa majangwa kasi ya ajabu kuna milima kule sengerema miaka 95 ilikuwa mapori lakini sasa hivi yamebaki mawe tu peupe inatakiwa mkaa uzuiliwe kuingia mjini wa mjini tukazane na ges mkaa ubaki kijijini kwa sababu matumizi ya mkaa asilimia kubwa ni mjini
Uharibifu mkubwa ambao upo sawa na wakata mkaa pia kwa wafugaji wa kuhamahama kama ule wa Wasukuma, Wamasai, Wamang'ati etc.

Nafikiri wote wangepigwa stop iliyo sawa.

Iangalie Shinyanga, haijaharibiwa na wakata mkaa bali wafugaji wamefanya yao. Kaione Chunya uone Wasukuma wasivyopatana na miti jinsi wanavyotaka Chunya ionekane vyema toka anga za juu. Nenda Kilombero, Usangu japo kwa sasa ni afadhali kidogo baada ya kutimuliwa.

Nafikiri wangeanza na wafugaji hata kabla ya hao wakata mkaa maana athari yao ni ndogo kuliko wafugaji.
 
Gas ishuke hadi 10,000 na 35000 kwa kg15 wallahi watu hawatagusa mkaa....maana hizo zitakusogeza hadi miezi minne wakati mkaa daily sh 2000×30=60,000
 
Nimesikia Waziri wa Mali Asli na Utalii akipendekeza maamuzi ya.kuongeza Bei ya mkaa ili kudhibiti ukataji miti holela. akisaidiwa na Waziri wa Mazingira-MH.January Makamba. anayedai mtanzania anatumia elfu nne kwa siku kukamilisha milo yake kwa kununua mkaa.akisema ni zaidi ya gharama za gesi.Hivi huu utafiti wa mtanzania kutumia elfu nne kwa siku kununua mkaa ni kweli? kama kwaajiri ya chakilula mtanzania anatumia wastani wa chini ya dola moja.anapata wapi hizo elfu nne za mkaa?

Zile sera za kutupatia gesi kwa gharama nafuu baada ya ugunduzi zimekufa?
Zile.sera za kila mwanafunzi apande miti zimekufa?
Je watu wakiacha kutumia.mkaa wakatumia kuni tatizo litakuwa limetatuliwa?

Hayo mapendekezo yametokana na utafiti? wadau mbona hatujashirikishwa?
Jf Members focus discussions that affect our lives serious like this one.
 
Hivi wananchi Wa Tanzania watapatia nafuu wapi?

Gesi mlihonga sasa mkaa bei juu....

Kuna haja ya kuwapima akili wafanya maamuzi Wa hii serikali ya mwendokasi......
 
Basi Ni kuingia barabarani Tu ndo kilichobakia, maana kila upande visiki, kulia visiki kushoto visiki
 
Halafu cha kushangaza wanataka kupandisha na bei ya umeme, aisee kweli hii Serikali inataka tuishi kama mashetani
 
Nimesikia Waziri wa Mali Asli na Utalii akipendekeza maamuzi ya.kuongeza Bei ya mkaa ili kudhibiti ukataji miti holela. akisaidiwa na Waziri wa Mazingira-MH.January Makamba. anayedai mtanzania anatumia elfu nne kwa siku kukamilisha milo yake kwa kununua mkaa.akisema ni zaidi ya gharama za gesi.Hivi huu utafiti wa mtanzania kutumia elfu nne kwa siku kununua mkaa ni kweli? kama kwaajiri ya chakilula mtanzania anatumia wastani wa chini ya dola moja.anapata wapi hizo elfu nne za mkaa?

Zile sera za kutupatia gesi kwa gharama nafuu baada ya ugunduzi zimekufa?
Zile.sera za kila mwanafunzi apande miti zimekufa?
Je watu wakiacha kutumia.mkaa wakatumia kuni tatizo litakuwa limetatuliwa?

Hayo mapendekezo yametokana na utafiti? wadau mbona hatujashirikishwa?
Jf Members focus discussions that affect our lives serious like this one.
huo ni uingo mkubwa,kuna sehemu mkaa wa 1500 unatoboa nao siku hata 3.Huo utafiti ni uongo na wanatafuta sababu za kuwanyonya tu watanzania.
 
Ushauri wangu kwa prof. Na makamba. Ili kunusuru miti serikari I subsidize majiko ya gesi na gesi yenyewe waone Kama kuna mtu wa mujini atatumia mkaa. Iwekwe sheria magereza yote. Shule za sekondari na taadisi zoote za serikali zitumie gesi. Wafugaji woote wawezeshwe watumie gesi ya wanyama. Naamini hili linawezekana ila viongozi
 
Hakuna anayezungumzia juu ya upandaji miti . Kila anayetoa tamko amekazania kodi miti iliyopotea inarejeshwa vipi ? maarifa ya kuanzisha kampeni ya upandaji miti yenye faida hakuna .wimbo imekuwa kodi kubwa.

Ukimkamata muuza mkaa amekwepa hiyo kodi hiyo unayomuwekea ujue mwisho wa siku utampiga faini ila miti ilishateketea. Hebu viongozi wetu mjiongeze kidogo fikiria kizazi kijacho . Wekeni gas ya bei nafuu ili tuachane na miti na turejeshe ile iliyopotea ardhi ni yetu na bado tunayo ila haina miti .
 
By Professor Maghembe

Biashara ya mkaa hivi sasa inaendeshwa na watu mbalimbali, mkaa unasafirishwa hadi zanzibar ukifika zanzibar unasafirishwa kwenda nje...

Sasa tutaweka kodi kubwa kwenye mkaa na watashindwa kuupata kwa urahisi.

Ili tulinde misitu yetu na utunzaji wa mazingira yetu.

Taasisi za serikali zinazotumia kuni na mkaa sasa zibadilike badala yake watumie mfumo wa gesi.
Kimsingi mkaa na kuni ndio nishati kuu zinazo tumiwa na familia nyingi hapa nchini hususani familia zinazo patikana mijini na vjijini. Hakuna nishati mbadala yakutosha kwasasa kutumika kwa matumizi ya nyumbani kama vile umeme, gesi, makaa ya mawe n.k. Kuweka ushuru/kodi kwenye nishati ya mkaa haliweji kuwa jawabu la ukataji wa miti kwa ajiri ya kuzalishia nishati hii hapa nchini. Njia sahihi ni kupunguza utegemezi wa nishati hii kwa wananchi wali wengi hususani wale wenye kipato cha chini kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya kupata nishati mbadala kama vile gesi na makaa ya mawe nishati ambazo kwasasa zinapatikana hapa nchini. Sioni kama Prof anatafuta njia sahihi ya kupunguza matumizi ya mkaa na kuni hapa nchini, hata sababu yenyewe anayotaka kuitumia kupandisha ushuru kwenye mkaa ni wazi kwamba haina mashiko yoyote. Kimsingi kwa idadi ya watanzania wanao tumia nishati ya mkaa na kuni kwasasa hata kama mkaa hautasafirishwa kwenda nje ya Tanzania bado uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti kwa ajiri ya kuni na mkaa utaendelea kuwa pale pale kutokana na kutokuwepo kwa nishati mbadala ya uhakika na ya bei nafuu kama vile gesi, makaa ya mawe, umeme, nguvu ya jua n.k.
Suala la msingi ni elimu kwa wananchi juu ya matumizi endelevu ya misitu na utunzaji wa mazingira hapa nchini kwa maeneo yote ya mijini na vijijini. Dar e s Salaam pamoja na mikoa mingine mikubwa hapa nchini kama vile Mwanza, Arusha, Mbeya n.k mkaa bado umeendelea kuwa nishati muhimu kwa wakazi wa mikoa hiyo walio wengi na ambao kipato chao ni cha chini. Kupiga marufuku au kuongeza ushuru wa nishati hiyo haiwezi kuwa njia ya kudumu ya kutatua tatizo la ukataji miti hapa nchini.
Njia ya kudumu nikuwa na nishati mbadala ya uhakika na ya kutosha
 
Back
Top Bottom