Serikali kupandisha kodi uingizwaji wa bidhaa za ngozi za mtumba nchini

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Waziri wa viwanda na biashara nchini,Innocent Bashungwa amesema serikal inampango wa kupandisha kodi kwenye uingizwaji wa bidhaa za ngozi za mtumba nchini ili kuongeza thamani ya uzalishaji na utumiaji wa bidhaa za ngozi hapa nchini

Waziri Bashungwa amesema hayo leo March 04.2020, wakati akitembelea kiwanda cha ngozi cha Himo Tanneries L.T.D ambapo amesema ili kuongeza thamani hiyo watanzania wanapaswa kuwa wazalendo kwa kupenda na kutumia bidhaa zao asilia zinazozalishwa nchini kwa ikiwemo za ngozi kwa lengo la kuinua uchumi wao na raifa kwa ujumla.


"Serikali inaendelea kuhakikisha uchumi wa viwanda unaongezeka mara dufu kwa kuungwa mkono na wadau pamoja na watanzania wwnyewe,bidhaa hizi za ngozi ni nzuri sana na zinadumu kwanini tusiunge juhudi za wazalishaji wa bidhaa hii ya ngozi hapa nchini,wanazalisha viatu,mikanda,mikoba mbalimbali"amesema Waziri Bashingwa.

Pia amesema atahakikisha shule zinaingia ubia na viwanda vya ngozi vilivyopo nchini ili kujenga utamaduni wa jamii ya watanzania wanaokua kutumia bidhaa za ngozi na kuinuka kiuchumi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kiwanda hicho cha ngozi cha Himo Tannaries,Sabas Herman Oisso ameiomba serikali kusaidia kuhamasisha watanzania juu ya umuhimu wa kutumia bidhaa za ngozi zinazozalishwa hapa nchini badala ya kununua zinazozalishwa nje siziso na ubora wa kutosha tena zenye gharama kubwa.
 
Ni jambo jema ila inabidi wazalishaji wawe makini. Pia inabidi serikali iangalie namna ya kuwapunguzia gharama za uwekezaji. Mfano kiatu cha Ngozi kizuri kinauzwa 60,000/=.
Kama wakiwekewa mazingira rafiki bei inaweza kuwa pungufu.
 
Back
Top Bottom