Sawa, tusubiri ng’ombe wanenepe, then wataanza kuuzwa kwa wingi na wafugaji, na nyama itashukaWAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameeleza sababu ya nyama kupanda kwa bei katika maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na upungufu wa upatikanaji wa ng’ombe na ongezeko la mahitaji ya viwanda vya kuchakata nyama.
Hata hivyo wafanyabiashara wa mifugo na wauza mabucha wamesema kuwa kupanda kwa kitoweo hicho kuanzia wanakochukua (machinjioni), gharama za usafirishaji na msimu huu wa kiangazi kumesababisha pia bei ya nyama kupanda kwani wafugaji wengi hawapendi kuuza ng’ombe wakati huu wakidai kwamba mifugo hiyo inakua haina uzito kutokana na kupungua kwa malisho na maji.
Bei ya nyama kwenye mikoa ya Arusha, Moshi na Dar es Salaam inadaiwa kuwa shilingi 7,000 mpaka shilingi 8,000 kwa kilo tofauti na awali ambapo kitoweo hicho kilikua kikiuzwa shilingi 6,000.
Baada ya Ethiopia ni Tanzania ndiyo ya pili kwa idadi ya mifugo Afrika.Sisi si ndiyo mnasemaga tuna Ng'ombe wengi sijui wa pili Africa
Point!Baada ya Ethiopia ni Tanzania ndiyo ya pili kwa idadi ya mifugo Afrika.
Ukweli ni kwamba, wafugaji hasa wasukuma hawataki kuuza mifugo yao kwa sababu wanacho chakula cha kutosha (Mahindi na mpunga), na hakuna namna ya kuwalazimisha wauze kwa sababu wanafuga kama ufahari, na huuza wanapokuwa na njaa!
Serikali lazima ijikite kuwawezesha wafugaji wafuge kibiashara.
Okay nimekupata Mkuu kumbe Jamaa zetu wanafuga Ng'ombe kama UremboBaada ya Ethiopia ni Tanzania ndiyo ya pili kwa idadi ya mifugo Afrika.
Ukweli ni kwamba, wafugaji hasa wasukuma hawataki kuuza mifugo yao kwa sababu wanacho chakula cha kutosha (Mahindi na mpunga), na hakuna namna ya kuwalazimisha wauze kwa sababu wanafuga kama ufahari, na huuza wanapokuwa na njaa!
Serikali lazima ijikite kuwawezesha wafugaji wafuge kibiashara.
Usukumani wanafuga ng'ombe kama urembo kabisa.Okay nimekupata Mkuu kumbe Jamaa zetu wanafuga Ng'ombe kama Urembo
Dah,Basi kuna kazi kubwa sana ya kuwaelimisha Jamaa zetu Wafugaji.Usukumani wanafuga ng'ombe kama urembo kabisa.
Unakuta msukuma ana ng'ombe kama mia mbili hivi halafu anaishi kwenye nyumba ya nyasi. Ukitaka mgombane nae, mwambie akuuzie ng'ombe wakati hajapanga kuuza.
Ndani kukiwa na mpunga wa kutosha, viazi, mtama, na mahindi, hauzi ng'ombe.
Kumbikumbi watawafaaMwaka huu sisi wasingida
Mafuta bei juu
Ng'ombe juu
Mbuzi juu
Kuku juuu
Mungu atupe nini zaidi?
Mashehe......Wapromote ufugaji wa Ngrooohhhh? Miezi sita tu anaingia sokoni, wakati Ng'ombe anahitaji miaka miwili na uzao wao ni wa 1\1\ na mimba ya miezi 9. Wakati Ngrooohhh mimba moja watoto 12 na mimba ni miezi mitatu tu.
K'koo nmenunua mwezi mei kilo 5,500 Mara mbiliMbona mimi Dar nanunua nyama kilo 7000 miaka 3 sasa. Hiyo 6000 ni Dar ya wapi?
Mkaldayo banaNikajua watasema kutokana na bei ya nyama kupanda kwenye soko la dunia.