Serikali: Kupanda kwa bei ya Nyama kunatokana na upungufu wa Ng'ombe

Wapromote ufugaji wa Ngrooohhhh? Miezi sita tu anaingia sokoni, wakati Ng'ombe anahitaji miaka miwili na uzao wao ni wa 1\1\ na mimba ya miezi 9. Wakati Ngrooohhh mimba moja watoto 12 na mimba ni miezi mitatu tu.
hahah noma sana
 
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameeleza sababu ya nyama kupanda kwa bei katika maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na upungufu wa upatikanaji wa ng’ombe na ongezeko la mahitaji ya viwanda vya kuchakata nyama.

Hata hivyo wafanyabiashara wa mifugo na wauza mabucha wamesema kuwa kupanda kwa kitoweo hicho kuanzia wanakochukua (machinjioni), gharama za usafirishaji na msimu huu wa kiangazi kumesababisha pia bei ya nyama kupanda kwani wafugaji wengi hawapendi kuuza ng’ombe wakati huu wakidai kwamba mifugo hiyo inakua haina uzito kutokana na kupungua kwa malisho na maji.

Bei ya nyama kwenye mikoa ya Arusha, Moshi na Dar es Salaam inadaiwa kuwa shilingi 7,000 mpaka shilingi 8,000 kwa kilo tofauti na awali ambapo kitoweo hicho kilikua kikiuzwa shilingi 6,000.
Kitoweo kinatokana majini..samaki ndiyo kitoweo! Nyama ni mboga
 
Baada ya Ethiopia ni Tanzania ndiyo ya pili kwa idadi ya mifugo Afrika.

Ukweli ni kwamba, wafugaji hasa wasukuma hawataki kuuza mifugo yao kwa sababu wanacho chakula cha kutosha (Mahindi na mpunga), na hakuna namna ya kuwalazimisha wauze kwa sababu wanafuga kama ufahari, na huuza wanapokuwa na njaa!

Serikali lazima ijikite kuwawezesha wafugaji wafuge kibiashara.
Jamii za kifugaji asilimia kubwa wamekataa kubadilika na kuachana na ufugaji wa kizamani.

Imefika wakati inatakiwa sera na sheria zitungwe kudhibiti ufugaji holela wa Ng'ombe.

Lazma kuwe na maximum capacity ya kumiliki Ng'ombe kwa kikundi au mtu ambae anatumia Communal graizing area. kama chanzo cha marisho ya mifugo yake.

kila Ng'ombe anaezid maximum capicity ilio wekwa ni lazima alipiwe kodi. Hii sio tu itapunguza ufugaji wa Ng'ombe wengi wasio na tija bali itasaidia kutunza mazingira yetu.

Special school kwa hizi jamii za kifugaji. Kuna msemo unasema "You can't teach an old dog new technic" Wekeza kwa watoto wanao zaliwa sasa hivi, Wapewe elimu ya kutosha. Ikiwezekana wawe wanasoma boarding school, huko unahakikisha ideoligy ya ufugaji wa kienyeji inaondoka na baada ya miaka 25 kutakua na kizazi kipya cha hizi jamii ambacho kinafikiri tofauti na kizazi cha sasa hivi.
 
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameeleza sababu ya nyama kupanda kwa bei katika maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na upungufu wa upatikanaji wa ng’ombe na ongezeko la mahitaji ya viwanda vya kuchakata nyama.

Hata hivyo wafanyabiashara wa mifugo na wauza mabucha wamesema kuwa kupanda kwa kitoweo hicho kuanzia wanakochukua (machinjioni), gharama za usafirishaji na msimu huu wa kiangazi kumesababisha pia bei ya nyama kupanda kwani wafugaji wengi hawapendi kuuza ng’ombe wakati huu wakidai kwamba mifugo hiyo inakua haina uzito kutokana na kupungua kwa malisho na maji.

Bei ya nyama kwenye mikoa ya Arusha, Moshi na Dar es Salaam inadaiwa kuwa shilingi 7,000 mpaka shilingi 8,000 kwa kilo tofauti na awali ambapo kitoweo hicho kilikua kikiuzwa shilingi 6,000.
Jana niliwasikia wenye mabucha wakisema sababu ni upungufu wa wateja! Hivyo wanawakamua hao wachache.
 
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameeleza sababu ya nyama kupanda kwa bei katika maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na upungufu wa upatikanaji wa ng’ombe na ongezeko la mahitaji ya viwanda vya kuchakata nyama.

Hata hivyo wafanyabiashara wa mifugo na wauza mabucha wamesema kuwa kupanda kwa kitoweo hicho kuanzia wanakochukua (machinjioni), gharama za usafirishaji na msimu huu wa kiangazi kumesababisha pia bei ya nyama kupanda kwani wafugaji wengi hawapendi kuuza ng’ombe wakati huu wakidai kwamba mifugo hiyo inakua haina uzito kutokana na kupungua kwa malisho na maji.

Bei ya nyama kwenye mikoa ya Arusha, Moshi na Dar es Salaam inadaiwa kuwa shilingi 7,000 mpaka shilingi 8,000 kwa kilo tofauti na awali ambapo kitoweo hicho kilikua kikiuzwa shilingi 6,000.
The last time I checked Abdala Ulega alikuwa naibu waziri wa mifugo na uvuvi na Si vinginevyo kama unavyotujuza hapa
 
Jibu la kipumbavu sana kutoka kwa huyo waziri. Suala la idadi ya mifugo katika nchi ni sera ambayo inapaswa kusimamiwa na serikali ili kuregulate bei ya nyama pamoja na mifugo hiyo katika nchi.

Huyu waziri ni sawa na anawaambia wananchi kuwa kazi imemshinda, halafu sad enough hana hata habari kuwa anadeliver message kama hiyo.

Wafanya biashara katika habari hii wanaonekana kutoa sababu ambazo ni za kiuchumi na ambazo ni genuine kuliko waziri mwenye dhamana.
Kama kuna watu wana bahati duniani ni huyu jamaa anayeitwa Waziri, .... Kwanza uongeaji wake tu unaonyesha ni mwongo, ni fundi wa kupanga maneno balaa... namkumbuka akiwa naibu Waziri wa Habari na Michezo kwenye ishu ya SERA YA MICHEZO TANZANIA ..
 
Tz ni nchi ya pili Africa kwa kuwa na ng'ombe wengi ukitoa Zambia
Sa iweje ng'ombe wapungue
Tozo had kwenye mazao ya mifugo ndo shida
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom