tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,476
- 17,674
Serikali imetangaza kwamba zaidi ya 96% ya wanafunzi wa shule za msingi waliohitimu darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari mwaka 2014.
Akitangaza matokeo hayo, katibu mkuu wa TAMISEMI amesema kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kumetokana na ubora wa elimu na kwamba hiki ni kiashiria kwamba wanafunzi wanaelewa masomo kwa kuwa wanasomea katika mazingira bora.
Ili kuhakikisha kwamba nafasi zote za sekondari zilizopo zinajazwa, serikali ilishusha alama za ufaulu (passmark) hadi 40 kati ya alama 250 (kuna papers 5 na kila paper inachangia alama 50). Hii maana yake ni kwamba mwanafunzi yeyote aliyemudu kupata wastani wa alama 8 (sawa na 16% ya ufaulu) kwa kila somo alichaguliwa kujiunga sekondari.
Source : TBC1