Serikali kuongeza bajeti NIMR

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
SERIKALI imesema inakusudia kuiongezea bajeti Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ili iweze kutekeleza malengo ya milenia kwa ajili ya utafiti.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, alisema hatua hiyo itasaidia kuboresha utendaji wa NIMR, kuinua viwango vya maisha ya jamii na kukuza uchumi.
“Serikali inathamini sana mchango wa NIMR katika suala zima la kuendeleza afya za jamii yetu, napenda kuihakikishia bodi hii kuwa tutatenga asilimia mbili ya bajeti ya wizara yangu kwa shughuli za utafiti,” alisema Waziri Mwakyusa.
Alisema katika ulimwengu wa sasa kuna magonjwa mengi ambayo yamekuwa yakiibuka, kama vile saratani, shinikizo la damu, kiharusi, kisukari na magonjwa ya moyo ambayo katika nchi zilizoendelea yanasababisha vifo kwa asilimia zaidi ya 60.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NIMR, Dk. Mwele Malicela alisema pamoja na mafanikio hayo, taasisi hiyo bado inakabiliwa na uhaba wa fedha kwa ajili ya utafiti, maabara, vitendea kazi, magari na majengo ya ofisi za taasisi hasa katika vituo vya utafiti vya Amani, Tabora, Muhimbili na Tanga.
“Mbali na tatizo hili, NIMR bado inakabiliwa na uhaba wa watafiti katika nyanja za sayansi ya jamii, demografia, afya ya mazingira, takwimu na uchanganuzi wa taarifa za utafiti na sera,” alisema Malicela. Bodi mpya iliyoteuliwa inaundwa na wajumbe 12 ambao ni Dk. Hassan Mshinda, Dk. Luka Siyame, Dk. Edith Ngirwamungu, Jonathan Tangwa, Dk. Malick Abdallah Juma, Profesa Eligius Lyamuya, Dk. Catherine Kuwite, Elli Pallangyo, Profesa William Mahalu na Dk. Salim Mohamed Abdulla.



h.sep3.gif


juu
blank.gif
 
Back
Top Bottom