Serikali kuondoa ajira za kudumu za umma, Juhudi na bidii ya mfanyakazi kazini kuamua hatma yake

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litafanyia mabadiliko makubwa sheria za utumishi wa umma kwa kuondoa ajira za kudumu serikalini, ili kuwezesha mabadiliko yaliyokusudiwa na Rais Dk. John Magufuli.

Katika mabadiliko hayo mfumo wa sasa wa ajira za serikali kuwa za kudumu utabadilishwa na badala yake, kudumu kwa ajira ya mfanyakazi kutategemea juhudi na bidii yake kazini, ili kuondoa uzembe uliodumu miaka nenda miaka rudi, katika sekta ya Umma.

===========================


Mabadiliko makubwa

*Bajeti za majeshi kumulikwa zaidi

*Sheria ya utumishi kufumuliwa

*Ukawa waibuka na mbinu mpya

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litafanyia mabadiliko makubwa sheria za utumishi wa umma kwa kuondoa ajira za kudumu serikalini, ili kuwezesha mabadiliko yaliyokusudiwa na Rais Dk. John Magufuli.

Katika mabadiliko hayo mfumo sasa wa ajira za serikali kuwa za kudumu utabadilishwa na badala yake, kudumu kwa ajira ya mfanyakazi kutategemea juhudi na bidii yake kazini, ili kuondoa uzembe uliodumu miaka nenda miaka rudi, katika sekta ya umma.

Akizungumza katika mahoajino binafsi na Raia Mwema, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, alisema baadhi ya sheria za kazi zinawafanya baadhi ya watumishi wa umma kuwa wazembe.

"Kwa mfano katika serikali ya sasa mfanyakazi mzembe kabisa kabisa, hata waziri kumfukuza kazi hawezi. Hata Katibu Mkuu hawezi mpaka afuate mlolongo mrefu na hatua nyingi sana, yaani kazi ni guarantee (uhakika) katika nchi yetu ni permanent and pensionable (ya kudumu na ina pensheni). Sheria za namna hiyo lazima ziondoke," alisema Spika Ndugai katika mahojiano ambayo yamechapishwa ukurasa wa 12 wa gazeti hili, na kuongeza; "Katika nchi ambazo zinaendelea kwa haraka moja ya jambo ambalo huna uhakika nalo ni ajira, ukifanya vizuri unayo ajira yako ukiboronga unaondoka saa hiyo hiyo na wakati huo huo, sasa sheria za namna hiyo ni lazima zibadilishwe ili watu wachape kazi. Wawe wakijua kabisa kwamba nipo kwa sababu nachapa kazi akileta uzembe kazini kwaheri."

Aliongeza kuwa mabadiliko mengine ambayo Rais Magufuli atayaleta ni pamoja na ile sheria ya ununuzi na sheria nyingine ambazo ni za hovyo hovyo, zinazoifanya serikali isifanye vizuri. Kwa mujibu wa Ndugai, Bunge litahakikisha sheria hizo zibadilishwa haraka.

"Huo ndiyo ushirikiano wetu tutakaompa lakini pia tutachangia vizuri katika mipango na bajeti zinazokuja tutazitengeneza vizuri zaidi kwa kupunguza fedha zote za ulaji ulaji, hii ya kila mwaka mapazia, kuweka makochi, kuweka makapeti na kompyuta kila mwaka na ofisi ni zile zile watu wale wale, bajeti ilikuwa imejaa ununuzi wa magari vilainishi lazima tukate kote huko," alisema.

Akizungumzia hatua hiyo, Rais wa Shirikisho la Vyama wa Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Gratian Mukoba, alisema hawezi kuunga mkono au kukataa hoja hiyo mpaka atakapoona hoja yenyewe na maelezo yake.

"Kwa kawaida muswada wa sheria huanzia kwanza kwa wadau, wakituletea tutaona, siyo kila kitu ni kibaya, sheria zinapotungwa zinakuwa na sababu kwa nini zimetungwa. Unaweza ukawa na maelezo mazuri tukajadili utekelezaji wake, tutaamua," alisema.

Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa baadhi ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa mazoea na kama sheria hiyo inaweza kutibu tatizo hilo, alikiri kuwepo kwa hali hiyo miongoni mwa watumishi wa umma lakini akatahadharisha kwamba tiba yake siyo kuondoa ajira za kudumu.

"Ziko sababu nyingi zinazosababisha baadhi ya wafanyakazi kuwa wazembe, siyo ajira ya kudumu peke yake. Kama kwenye nchi yenu mmeamua kubaguana kwa malipo, mmoja analipwa mara 30 ya mwingine, huyo anayelipwa kidogo hawezi kuwa na morali ya kazi, atanyong'onyea.

"Yule anayepata mara 30 ataathiriwa utendaji wake na hawa wenye kidogo kwa sababu ni wengi, kwa sababu watajifanya (wanaolipwa kidogo) na serikali itajifanya inalipa lakini kumbe kinacholipwa hakitoshelezi chochote," alisema Mukoba.
Aliogeza kwamba miaka ya 1970 na 1980 watu walikuwa na uhakika wa ajira za kudumu lakini walikuwa wanachapa kazi kwa bidii kwa kuwa kulikuwa na uwiano wa haki kwenye malipo ya mishahara, tofauti na sasa, akishauri pia suala la kushuka kwa morali ya kazi miongoni mwa watumishi wa umma lifanyiwe utafiti makini na si kulikurupukia.

Vyombo vya Ulinzi kubanwa
Katika hatua nyingine, Spika Ndugai ameliambia Raia Mwema kwamba ili kuweza kufanikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kupunguza na kubana matumizi ya serikali, bajeti za vyombo vya ulinzi zitakapitiwa kwa uwazi na Kamati ya Bunge, tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
?Safari hii tutavibana hata vyombo vya Ulinzi na Usalama, tunataka kuona matumizi yaliyo bora serikalini kote, kwa hiyo Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) tutaizingatia na tutahakikisha tunaijadili na kuchambua kwa undani kabisa yatokanayo na ripoti hiyo,? alisema.

Raia Mwema lilitaka kufahamu kama sababu zilizofanya bajeti za vyombo hivyo vya Ulinzi kutojadiliwa kwa uwazi katika bajeti zilizopita, hazina tena nguvu na kama zipo, Bunge litafanyaje kuhakikisha uwazi na uwajibikaji unakuwapo bila kuathiri mikakati ya usalama nchini, hapo Ndugai alijibu akisema; ?Vyombo vya Ulinzi na Usalama ni lazima viwe na usiri fulani katika mambo yanayowahusu, hilo litaendelea.

"Lakini tunataka uwazi na ukweli ndani ya usiri, hicho ndicho tunachokitafuta, hata kama mambo yote yataishia kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge, lakini hizo kamati zitachambua kwa undani na watauliza maswali na watataka waliofanya matumizi mabaya ya fedha wawajibishwe na serikali tofauti na ilivyokuwa nyuma. Huko nyuma wawajibikaji walikuwa ni wanasiasa pekee, lakini sasa tutapanua wigo kwa sababu lazima wote tuwajibike, ni nchi yetu sote, hatuwezi kuwa wengine mguu sawa wengine mguu pande," alisema Spika Ndugai.

Kamati ya POAC kurejeshwa
Katika kuhakikisha uwajibikaji kwenye mashirika ya umma, Spika Ndugai anasema Bunge litairejesha Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, ambayo ilifutwa katika Bunge la 10 chini ya Spika, Anne Makinda.

"Tulikuwa na kamati ya serikali za mitaa, kamati inayosimamia hesabu za serikali kuu na kamati inayosimamia mashirika ya umma, tukaunganisha hizi mbili za mashirika ya umma na serikali kuu, matokeo yake kazi zimekuwa nyingi mno, sasa ile kamati hata ifanye vipi haiwezi kumaliza kazi yake ndani ya mwaka mmoja. Kwa hiyo, tunafikiria kuirudisha kamati ile ya Mashirika ya Umma (POAC) ili mashirika ya umma nayo yamulikwe kama ambavyo serikali kuu inamulikwa," alisema Ndugai.

Akizungumzia uamuzi wa kurejeshwa kwa kamati hiyo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, alisema huo utakuwa ni uamuzi sahihi kwa sababu utaongeza ufanisi wa kazi za Bunge katika kuisimamia serikali.

"Mtaji wa Mashirika ya Umma ni shilingi trilioni 20 ni jambo jema la kuungwa mkono Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pekee inashindwa kusimamia Wizara na Mashirika, POAC italeta ufanisi," alisema Zitto.

Wapinzani 'kujibinafsishia' kamati
Wakati kamati hizo kikanuni zinapaswa kuongozwa na wabunge wa Upinzani, vongozi wa kambi hiyo wanataka badala ya wajumbe wote wa kamati hizo kuchagua wenyeviti wao, wanataka waachiwe wapinzani peke yao kuchagua wenyeviti.

"Kambi ya Upinzani wanalalamika wanasema kwamba wanapogombea wapinzani wawili au watatu wale wajumbe wa chama tawala ndani ya ile kamati, wanachagua mbunge wa Upinzani ambaye ni mpole zaidi, kwa hiyo wanataka zile kamati tukishaziteua zile tatu tuwaachie wao kambi ya Upinzani ndiyo wateuwe wenyeviti wa hizo kamati," anasema Spika Ndugai na kuongeza kuwa hilo kwa sasa halijakubalika, badala yake utaratibu wa zamani utaendelea kutumika.

Magufuli: Nitawazunguka kabla
Kuhusu wasiwasi kwamba wapo baadhi ya watu wanaweza kumzunguka Rais Magufuli ili kumhujumu katika juhudi zake, watu wa karibu na Rais huyo wamelieleza gazeti hili kuhusu msimamo wake katika jambo hilo.

"Wakati naanza kazi ya urais na kutangaza kupambana na wabadhirifu, wazembe na majizi wa mali za umma kama nilivyosema jana (Ijumaa) kuwa nimejitolea kutumbua majipu, nilijua uzito na ugumu wa kazi hiyo, lakini niwahakikishie Watanzania kuwa atakayejaribu kunizunguka mimi ndiye nitamzunguka kwanza, maana mimi ndiye bosi wake," alinukuliwa Magufuli na mmoja wa watu wake wa karibu kwa gazeti hili.
Kwa mujibu wa mtu huyo wa karibu na Magufuli (jina linahifadhiwa) Rais Magufuli anawaomba Watanzania waendelee kumwombea Mungu ili afanikishe nia yake ya dhati ya kutatua kero za wananchi.

Chanzo: Raiamwema
 
This is stupidity,, unapofanya hivyo basi maslahi ya wafanya kazi yatekelezwe kwa wakati .
Tusifanye watu kuwa watumwa
success come to who become success conscious & this is a principle.
////
/////
//////
 
Ili kuvunja mkataba wa sasa wa ajira ya kudumu inabidi kuwabembeleza watumishi wa umma waridhie kusaini mkataba wa muda. Ili kulazimisha mkataba wa sasa uvunjwe inabidi serikali iingie gharama za kuvunja mkataba wa sasa.
 
Nadhani kabla hawajapitisha hizo sharia zao wanapaswa kuboresha mazingira ya Kazi naupatikanaji wa vitendea Kazi. Hvi unamuitaje mfanyakazi mzembe aside navitendea Kazi? Labda waweke kwa baadhi ya idara kama TRA. By the way, wangepitia vitu kama posho kwa watendaji wa serikali na tofauti kubwa ya salary kati ya kada moja na nyingine kwa kiwango sawa cha elimu, utambuzi wa watumishi wanaojiendeleza na maslai mfano fani zingine wanatambua uwepo wa master na PhD na so on na stahiki zao katika level husika ila sio kwa walimu ni ujanja ujanja mwingiii!! Sasa kwa hali kama hii nadhani itaradhimu walimu wore wawekwe pembeni tulete wachina.
 
Hii, si walishashindwa wanarudia tena!!. Walifanya hivyo wakashindwa kuwalipa pesa zao baada ya mkataba kumalizika. Leo wanarudia yale yale au wamesahau walikwama wapi?
 
Hii, si walishashindwa wanarudia tena!!. Walifanya hivyo wakashindwa kuwalipa pesa zao baada ya mkataba kumalizika. Leo wanarudia yale yale au wamesahau walikwama wapi?

safari hii wamejipanga wewe subiri hapohapo usijelalamika hapa tena.
 
Ni kheri tu,cha msingi wasikwamishwe kwa namna yoyote ile pale wanapotaka kutekeleza majukumu yao,maslahi yao yazingatiwe,wapewe vitendea kazi,hakuna mtu atakayezembea kazi kama akitimiziwa kila kitu
 
Ili kuvunja mkataba wa sasa wa ajira ya kudumu inabidi kuwabembeleza watumishi wa umma waridhie kusaini mkataba wa muda. Ili kulazimisha mkataba wa sasa uvunjwe inabidi serikali iingie gharama za kuvunja mkataba wa sasa.

kwani sheria ya kazi inasemaje? Mwajiri akivunja mkataba anakulipa mshahara wa mwezi mmoja
 
Ili kuvunja mkataba wa sasa wa ajira ya kudumu inabidi kuwabembeleza watumishi wa umma waridhie kusaini mkataba wa muda. Ili kulazimisha mkataba wa sasa uvunjwe inabidi serikali iingie gharama za kuvunja mkataba wa sasa.

Ndiyo hapo sasa,maana watumishi wa umma waliingia mkataba wa kudumu hivyo lazima walipwe miaka iliyobaki ndiyo waingie upya mkataba. Magufuli aache kukurupuka ataligharimu taifa hili.
Taifa hili lilishaoza tangu muda hivyo Linahitaji busara ili kulitibu na si kukurupuka.
 
Back
Top Bottom