Serikali kununua rada sita za kisasa

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
REIA1.jpg


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Ally Karume mara baada ya kumtembelea ofisini kwake Kisiwani Unguja.

RIA2.jpg


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa wakati viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo Kisiwani Unguja. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Ally Karume.

RIA5.jpg


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Ally (kulia) Karume wakati alipotembelea taasisi zilizochini ya Wizara hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hiyo Mustafa Abood Jumbe.

RIA6.jpg


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mustapha Abood Jumbe afafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) katika kikao kazi mjini Unguja.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za kutangaza zabuni kwa ajili ya ununuzi wa rada sita za kisasa kwa ajili ya kuboresha usimamizi na ufuatiliaji wa safari za anga hapa nchini.

Prof. Mbarawa amesema hayo mjini Unguja mara baada ya kukagua shughuli zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) na Uwanja wa Ndege wa Zanzibar ambapo amesisitiza umuhimu wa kufata sheria katika kumpata mzabuni.

“Tumejipanga kuhakikisha kwamba miundombinu ya safari za anga nchini inaimarika ili kuvutia utalii na usalama wa abiria wa usafiri wa anga”, amesema Prof. Mbarawa.

Ameitaka TCAA kuhakikisha kwamba marubani wanaopewa vibali vya kurusha ndege nchini wanakidhi vigezo vya kimataifa ili kuufanya usafiri wa anga kuwa salama na wa uhakika.

Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Ally Karume amempongeza Prof. Mbarawa kwa ushirikiano anaoufanya kati ya Wizara hizo na kusisitiza kuwa hali hiyo itaongeza ufanisi katika usimamizi wa shughuli za Serikali na kuleta tija kwa wananchi.

“Huduma wanazozipata bara ni vyema na sisi Zanzibar tukanufaika nazo ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano ili kuleta usawa kwa wananchi wa pande zote za Muungano”, amesisitiza Balozi Karume.

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amezungumzia umuhimu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kubadilisha mfumo wa masafa wa 700MHZ kutoka kwenye analogia kwenda Digitali ili kuuwiana na upande wa Tanzania Bara na hivyo kuondoa muingiliano wa mawasiliano.

Profesa Mbarawa yupo Mjini Unguja katika ziara ya kukagua taasisi zilizo chini ya wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na kubadilishana uzoefu na viongozi wa wizara hiyo (Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji) kwa upande wa Zanzibar
 
Dar !! Mungu ampe nguvu na uvumilivu Rais wetu
Azidi kutuongoza kwa moyo mmoja Watanzania.
Naamini Tutapata vitu vingi kupitia uongozi wa Rais wetu mtetezi wa Wanyonge
Tuzidi kumpa moyo
 
Tunarudishana kwenye hii miradi ya kazi. Humu bwana watu huwa wanatandika balaaa.
Yaani humu kubigwa vi 'bi' 'bi' tano saba kumi ishirini ni vimichezo vya kombolela kwa watoto. Hizi project ni uchochoro wa kutandikia.
Sina imani na hzi project bora waajiri walimu tu wanazengo wapate elimu
 
Wanafunzi Wanakaa chini, wamama wanajifungulia chini, chanjo za Watoto shida, madawa hospitalini ni kitendawili, walimu mishahara ya ovyo, vifaa vya maabara hamna, eti rada! Na kuna majinga kijijini yanashangilia! Hii nchi ni bado sana kwa kuwa idadi ya wajinga ni kubwa Mno! Kuikomboa hii nchi mkono wa mungu unahitajika
 
uzuri wa serekali inakopa italipa kidogo kwa kutukondesha huku tukipumulia gesi mahututi
 
Ndio viwanda vyenyewe hivyo vimeshaanza kujengwa. Kweli Tanzania ya viwanda itafika hata kabla ya miaka mitatu kuisha tokea sasa.
 
wale walala hoi mliokuwa na mategemeo kama jamaa yenu yupo pale kwa ajili yenu msahahu
 
Jambo jema sana hili mungu awaongoze kufanikisha adhima hii.

Kweli kabisa Simiyu Yetu;
Kama ile moja tu chenji iliyorudi ilikinaisha watu sasa 6 nadhani watakaa mda mrefu kabla ya kubuni mradi mwingine. Ila tunajiuliza, ile ya Chenge imekwisha zimika hadi tununue myingi hivyo? Au nyengine tunaweka stoo likizima hili tuvute ilio karibu na dirisha tu?? Nawaza tu msinipige mawe. Moja tu ilazima fegi, 6 si tutazimia njiani? Haya jamani, hata majani tule lakini usalama kwanza
 
Back
Top Bottom