Serikali: Kuna matukio 19,726 ya Ubakaji Tanzania tangu Mwaka 2019-2022

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Vitendo vya Ukatili.jpg


Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema takwimu za matukio ya vitendo vya ukatili Nchini vilivyoripotiwa kwenye vituo vya Polisi kuanzia mwaka 2019 hadi Machi, 2022 ni 27,838.

Masauni amesema hayo leo Aprili 6, 2022 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge la Viti Maalum, Fatma Toufiq alipohoji Je, kuna wahanga wangapi wa vitendo vya ukatili nchini kuanzia mwaka 2019 hadi 2022?

Masauni amesema mchanganuo wa takwimu hiyo ni matukio ya kubaka ni 19,726, kulawiti ni 3,260 kati yao wanaume 3,077 na wanawake 183, kuunguzwa kwa moto ni 198 kati yao wanaume 73 na wanawake 125, kutupa watoto wachanga ni 443 kati yao wanaume 177 na wanawake 266, kipigo ni 4,211 kati yao wanaume 16 na wanawake ni 4195.

Vitendo vya ukatili katika jamii.png


Masauni amesema jumla ya kesi zilizofikishwa Mahakamani ni 21,063 na watuhumiwa waliohukumiwa ni 14,278 na mashauri mengine yako kwenye hatua mbalimbali za upelelezi na mahakamani.

Aidha, Serikali inaendelea kuiasa jamii kutumia vema taasisi za familia, kaya, jumuiya za kidini na ngazi za vitongoji, vijiji na mitaa kudhibiti vitendo vya ukatili katika jamii.
 
Mbona haieleweki "kutupa watoto wachanga 443 kati yao wanaume 177 na wanawake 266"?? Hapa idadi ni jinsia ya watoto au ni idadi ya waliotupa watoto?
 
Mbona haieleweki "kutupa watoto wachanga 443 kati yao wanaume 177 na wanawake 266"?? Hapa idadi ni jinsia ya watoto au ni idadi ya waliotupa watoto?
Chukua 443 utoe 177,idadi inayobaki ni watoto wa kike.
 
Mbn zile za mauaji hazipo na hiii miezi ya karubuniiii zimeshamiriiiii sanaaaa
 
Watoto wa kike wengi hutolewa usichana wao kwa kubakwa,na hayo matukio yangeripotiwa,sijui ingekuaje?
 
Back
Top Bottom