Serikali kumwaga ajira kwa maofisa ugani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kumwaga ajira kwa maofisa ugani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 9, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wednesday, 08 August 2012 18:50

  [​IMG]Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharb Bilal

  Israel Mugusi, Dodoma na Fredy Azzah
  SERIKALI imesema itaajiri wataalumu wa kilimo 1,000 katika Mwaka wa Fedha wa 2012/13 na kuwa vijana wanaomaliza vyuo vya kilimo watapewa mitaji na ardhi ili wafanye kazi za uzalishaji wa kisasa. Hayo yalibainishwa jana na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharb Bilal, mjini Dodoma alipokuwa akizungumza katika kilele cha Madhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane). "Serikali itaendela kufundisha na kuajiri wataalamu wa kilimo mpaka tuhakikishe kila kijiji kinakuwa na mtaalamu wa kilimo," alisema Dk Bilal.

  Wakati DK Bilal akisema hayo, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Dk Chrisopher Chiza alisema vijana wanaomaliza vyuo vya kilimo watapatiwa mitaji pamoja na ardhi ili wafanye kilimo cha kisasa. Alisema kuwa, kufanya hivyo kutasaidia nchi kujihakikishia uhakika wa kuwa na chakula cha kutosha. Kwa upande wake, Dk Bilal alisema pia kuwa ni vyema vyama vya ushirika nchini vikafanya kazi zake kwa uaminifu lengo likiwa ni kuwasaidia wakulima. Dk Bilal alisema kuwa, hali hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini pamoja na kuwasaidia wakulima. Dk Bilal pia aligusia suala la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu ambapo aliwataka wakulima kuhakikisha wanashiriki.

  Alisema kwamba kupitia sensa hiyo Serikali itapata takwimu za wakulima nchini jambo ambalo litaisaidia kupanga mipango yake ya maendeleo. "Ni vyema wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau wengine wa kilimo mkajitokeza kuhesabiwa ili kuisaidia Serikali katika kupanga mipango yake," alisema Bilal. Mwenyekiti wa Chama cha Kilimo Tanzania (Taso), Engelibert Moyo alisema washiriki waliojitokeza kushiriki maonyesho hayo kwa mwaka huu ni 450. "Katika hao washiriki kuna taasisi mbalimbali Serikali zisizo za Serikali pamoja na wakulima," alisema Moyo.

  Alisema kuwa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo imekuwa ikiwasaidia sana wananchi kwa kuwapatia huduma mbalimbali, mwaka huu haikushiriki. "Wananchi huwa wanapatiwa huduma mbalimbali na Wizara ya Afya kwa sababu huwa wanakuja na madaktari bingwa, kwa hiyo kutoshiriki kwao kumewakosesha wananchi huduma muhimu za afya," alisema Moyo.

  Â…Awashukia watendaji vyama vya ushirika Katika hatua nyingine Dk Bilal amesema baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika nchini ni kikwazo cha kukuwa kwa vyama hivyo, jambo ambalo linakwamisha maendeleo ya wakulima nchini.

  Alisema ingawa kuna ongezeko kubwa la vyama vya ushirika nchini lakini, changamoto kubwa imekuwa kwa baadhi ya watendaji wa vyama hivyo kukosa uaminifu, uwezo na kutowajibika katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Pamoja na changamoto hiyo alisema vyama hivyo vimeongezeka kutoka vyama 2,244,727 mwaka 2010/2011 hadi kufikia vyama 2,396,001 kwa mwaka
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Habari njema sana kwa vijana wetu!
   
 3. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hivi bilal unaelewa unachosema. Are sure what exactly u are saying?. Mambo hayaendi hivyo. Kilimo ni shughuli. Hivi hicho kitakachozalishwa mtanunua serkali kwa bei ya hasara au mna maana gani hapa? Come 10 years on mtakuja na uongo mwingine iam very sorry i stand to prove the fact.
   
Loading...