Serikali kumsaka nyoka mwenye miaka 209 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kumsaka nyoka mwenye miaka 209

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Jul 21, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]20 JULY 2012[/h]Na Theonestina Juma, Bukoba

  SERIKALI imedhamiria kumsaka nyoka mwenye umri wa miaka 209 aliyepo katika Msitu wa Akiba Minziro, uliopo Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera.

  Lengo la kumsaka nyoka huyo ni kutokana na ukongwe wake hivyo kuwa kivutio kikubwa duniani hasa katika sekta ya utalii.

  Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki nchini, Dkt. Felician Kilahama, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari.

  Alisema nyoka huyo mwenye futi 47, atapatikana baada ya mapito yake katika msitu huo kuonekana ila ni vigumu kuonekana hadharani kwa sababu hupendelea kuishi mapangoni.

  “Huyu nyoka lazima tumfanyie mahesabu ya kumkamata kirahisi, umri wa miaka 209 sio mchezo, ameweza kutambulika Baada ya kupima urefu wa mapito yake, pia kuna chatu na nyoka wenye mapembe,” alisema Dkt. Kilahama.

  Aliongeza kuwa, licha ya nyoka kuhatarisha maisha ya watafiti lazima kufanyike uharaka wa kuupandisha hadhi msitu huo uwe hifadhi ya Taifa ili kuboresha usimamizi wake.

  “Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa Kagera (RCC), kilipitisha msitu huu upandishwe hadhi, nyoka huyu ambaye ni aina ya Giant Forest Cobra, kichwa chake kina rangi nyekundu na sehemu ya kiwiliwili rangi ya kijani.

  “Alianza kufanyiwa utafiti mwaka 2000 baada ya kupatikana kwa taarifa kutoka kwa wenyeji wa maeneo hayo juu ya kuwepo kwa aina ya nyoka huyo katika msitu huu,” alisema.

  Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Halmashauri ya Missenyi, kupitia Maofisa wa Misitu, mwaka 2010 walianza kuweka mitego ya sindano katika mapito anayotumia ili kuchukua damu yake na kwenda kuipima vina saba ndipo ilibainika kuwa hadi kufikia mwaka huo, alikuwa na miaka zaidi ya 207.

  Dkt. Kilahama alisema nyoka huyo atakuwa kivutio muhimu mkoani hapa kama atapatikana licha ya kukabiliwa na tatizo la ukumbwa wa msitu ambao hekta 25,000 kwani nyoka huyo amekuwa akihama mara kwa mara kwa ajili ya mawindo.

  Ofisa Misitu wilayani hapa, Bw. Wilbard Bayona, alisema nyoka huyo ana uwezo wa kuishi siku 68 bila kula chochote zaidi ya maji baada ya kumeza mnyama yeyote ambaye atamkamata mawindoni.   
 2. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Samahani, hivi life span ya nyoka ni miaka mingapi? Nilidhani ni kobe tu mwenye life span ndefu.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  nchi hii ina vipaumbele vya kipuuzi sana..
   
 4. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  yaani badala ya kufanya utafiti na ugunduzi wa nafaz za kazi wanakwenda kumtafuta nyoka ambaye wanahisi yupo lakini hawamuoni! Duh kazi kweli kweli
   
 5. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,797
  Likes Received: 6,306
  Trophy Points: 280
  Ngoja invoice ya kumsaka huyo nyoka ikija kuletwa, utakimbia.
   
 6. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kumpata huyo lazima wengi mpoteze maisha, na si rahisi kumpata, kwasababu nyoka huyo ni shetani, ni mzimu fulani wa watu wa huko ambao hakika yake hata mtu akichanjwa chale kwa mzimu huo mashetani yake kuja kumtoka si rahisi kwasababu amechanja na kujiunganisha na shetani mwenyewe.....kama mna akili timamu, hivi kuna kiumbe hai chenye damu ambacho kinaweza kuishi miaka yote hiyo kama si spiritual being?
   
 7. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbuga za wanyama tele tulizonazo hazitosh kuwavutiawatalii?!!.dah nchi hii.
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  naomba nikuulize, hivi ulihitaji kunukuu post yote ya awali wakati shida yako ni kuuliza hili swali moja?, huoni kama unatujazia server yetu bila sababu?.
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Duh mwili umesisimka.
   
 10. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Bado kuna vivutio vingi havijaendelezwa ambavyo vingelipatia taifa mapato mengi na kuongeza pato kwa wananchi wanaoishi jirani.
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Sijui kama umesoma habari hii vizuri ama umekurupuka tu kupost.
   
 12. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,320
  Likes Received: 2,299
  Trophy Points: 280
  Mzizi mkavu tenda hiyo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,583
  Trophy Points: 280
  average life span 22 years record is 47 years. Nyoka wa umri miaka 207 NAHISI uzushi, mradi wa kupata chochote kitu. How do you determine age from genetic material? ( only aware of radio carbon method of determining age of fossils)
   
 14. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Aina hii ya fikra na mitazamo kwa hawa watu wa misitu sijui itaisha lini? Yaani wao mawazo ni kuweka misitu katika hadhi ya uhifadhi tu! Hawawazi kama raia wanaokaa karibu na msitu huo kama wao wanataka msitu huo uwe wa hifadhi!!

  Matokeo yake, aina hii ya utekelezaji wa sera (top - down approach) ni kuwa hata huo usimamizi wanaotaka kuboresha unakuwa ni hadithi za Alfu Ulela. Usimamizi bila kuwashirikisha (tena kuwashirikisha kiuhalisia - kuanzia kwenye wazo la kuufanya msitu uwe wa hifadhi au lah) ni kazi bure. Pia ni jambo ambalo halina mafanikio ya muda mrefu, kwani bila kuwa na mipango madhubuti ya kutafuta vyanzo mbadala vya mapato baada ya msitu husika kuwa wa hifadhi, ina maana raia watakuwa wanasukumwa zaidi katika dimbwi la umaskini; kwani vyanzo vya mapato na kusukumia maisha vitakuwa vimepigwa stop - kwa jina la uhifadhi!

  Halafu huyo Giant Forest Cobra katika jamii za nyoka sijawahi sikia..najua kuna forest cobra, lakini giant forest cobra?!?


  [​IMG]

  Huyu ndiye forest cobra! Sasa huyu ginat forest cobra sijui yukoje?!?!
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sikujua wanaishi miaka yote hiyo
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  this is fantastic news. uchunguzi kuhusu huyo nyoka ni muhimu sana si tu kwa ajili ya intrinsic value of doing so, bali pia kuitangaza hiyo hifadhi na pengine kujua hiyo eco-system nzima inahusikaje na huyo kiumbe. kwa wale wenye mawazo ya kigagula na/au kutokujua umuhimu wa research poleni sana.
   
 17. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #17
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  unasema wewe, unauliza wewe ? Khaaa!
   
 18. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Ana kichwa chekundu na kiwiliwili cha kijani!
   
 19. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kwani Intelejensia ya Kova haifanyikazi huko msituni? Mafisadi wanamiradi mingi sana ya kutafuna kodi za walalahoi
   
 20. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Huyu giant forest cobra mwenye kichwa chekundu atakuwa ndiyo amegunduliwa duniani. Kwanza katika jamii za cobra, ni King Cobra (Ophiophagus hannah) ndiye mkubwa zaidi kuliko wote, ambaye anaweza kuwa na urefu wa wastani wa mita 3 hadi 4; na uzito uwa ni kama 6kg. Ila kama akiwa yupo kwenye Zoo anaweza kuwa mrefu hadi mita 5.7.

  Anyway, ngoja tuone matokeo ya uchunguzi huo; huwezi jua, anaweza patikana species mpya ya cobra.
   
Loading...