Serikali kumlipa fidia baba wa Waziri Masha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kumlipa fidia baba wa Waziri Masha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 22, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,442
  Likes Received: 81,491
  Trophy Points: 280
  Serikali kumlipa fidia baba wa Waziri Masha

  Nashon Kennedy, Mwanza
  Daily News; Monday,December 22, 2008 @21:15

  Aliyekuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Sengerema mkoani hapa kupitia chama cha United Democratic (UDP) mwaka 2000, Dk. Fortunatus Masha, ameshinda kesi yake dhidi ya serikali bada ya serikali kuamuriwa kumlipa fidia ya Sh milioni 50 kutokana na kipigo cha polisi alichokipata wakati wa uchaguzi huo.

  Masha ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa UDP Taifa, alifungua shauri hilo mwaka 2006, katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, akidai alipwe fidia ya Sh bilioni moja kutokana na kupigwa na askari Polisi wa wilayani Sengerema Oktoba 31, 2000 wakati wa Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

  Kwa mujibu wa Msajili wa Mahakama Kanda Kuu ya Mwanza, Frederica Mgaya, hukumu hiyo ilitolewa Desemba 16, mwaka huu na Jaji A. Sumari. Dk. Masha ni baba wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, ambaye inadaiwa wakati wa tukio hilo la mwaka 2000, alikuwa pamoja na baba yake.

  Dk. Masha ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Afrika Mashariki, alikuwa akimlalamikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutokana na kupigwa na polisi wakati huo wa uchaguzi, ambao mgombea wa CCM alikuwa ni Dk. William Shija ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Katika kesi hiyo, Dk. Masha alikuwa akitetewa na Wakili maarufu nchini, Mabere Marando wakati serikali ilikuwa ikiwakilishwa na mawakili wake wawili, Ewin Kakolaki na Dora Komba.

  Kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mwaka 2001 na baadaye kuhamishiwa katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Mwanza ambako ni jirani na eneo la tukio hilo, nia ikiwa ni kuupata ushahidi na kuharakisha shauri hilo ambalo lilisajiliwa kwa namba 10/2006. Hata hivyo, mahakama hiyo imeacha wazi nafasi ya serikali kukata rufaa endapo kwa namna moja ama nyingine haikuridhika na uamuzi huo.
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Muandishi angekua mkweli tu kuwa wote wawili baba na mtoto, walikula kipigo na wote walitupwa rumande mpaka kesho yake walipotolewa kwa dhamana kwa kujaribu kushindana na Shija, aliyekua waziri kwenye serikali ya Mwinyi na Mkapa pia.
   
 3. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Duh!! Katika suala hili la kupigwa kwa wananchi wote wangelipwa (Mil50) serikali yetu ingekuwa mufilisi kwa sababu ni watu wengi sana wanapigwa, sasa naona uchaguzi wa 2010 itabidi tuwe tunatembea na video kamera ili kurekodi kila kitu na kurudi kudai mahakamani, nadhani hapo matendo ya kupigana yatapungua sasa.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Watu wanaendelea kupigwa, kuuawa au kuporwa mali zao. Na serikali au baadhi ya watu walioko serikali pia wanafanya hivyo na haki haitendeki, kuna wengine wanafungwa kwa kubambikiziwa kesi na kufanyiwa unyama mwingi tu. Hii ndio Tanzania yetu, wajanja wanaweza kulipwa wanyonge wataendelea kunyongwa. Kwa hiyo huyu jamaa inawezekana amelipwa kutokana na kuwa sasa kidogo yuko kwenye system and mwanae yuko huko, lakini angekuwa nje hata madai yake yasingesikilizwa.
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Dk. Fortunatus Masha ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Afrika Mashariki.

  Naomba kuuliza aliingia bungeni kwa tiketi ya chama gani mwishoni mpaka akaenda bunge la E.A?
   
 6. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa yaliyotokea Tarime! LISU tafadhali saidia...
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama unaamanisha kuingia Bunge la Tanzania, Mzee Masha hayumo humo wkani wabunge wa A. Mash hawatokani na wabunge wa nchi husika, wanachagukliwa kutoka nje ya Bunge. Huyu alipigiwa kampeni na watu wa CCM (nadhani mwanawe alihusika kwenye kuinjinia mzee apate nafasi hiyo)
   
 8. M

  Mutu JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Ok shukrani ,maana mimi nilikuwa naelewa siku zote wabunge wa Jamuhuri ndio wanabigiana kura kutoa wanaoenda kwenye bunge la E.A na nakumbukumbu kama hiyo .

  Ok vyema ,kumbe alirudi chichiemu apate urahisi.
   
 9. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Wabunge wetu hao, wanaangalia maslahi yao tu, na si kutetea wananchi kama wanavyojinadi. Ni nani anaweza kutumia mamilioni ya pesa zake kupiga kampeni eti ili awatetee wananchi?
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hajarejea CCM. Wabunge wa A Mash kutoka TZ wanapigiwa kura na wabunge wa Tanzania. kwa utaratibu uliopo, kunakuwa na wanne kutoka CCM na mmoja anatoka upinzani, nafasi ya upinzani ndio kaipata baba wa masha lakini kwa kupigiwa kura ya wabunge wengi wa CCM
   
 11. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mobile phone zitawamaliza
   
Loading...