Serikali kulichukua Shamba la mifugo la Utegi; Otieno Igogo achukuliwe hatua kwa kulifilisi shamba

koryo 2

Member
Jul 29, 2016
24
12
Leo kwenye taarifa ya habari STAR TV Mkuu mpya wa Mkoa wa Mara Dr. Mlingwa alitembelea Shamba la Mifugo la Utegi na kuwaeleza wananchi wa Vijiji Sita vinavyozunguka shamba hilo kuwa IMETOSHA sasa Serikali inalichukua shamba hilo kwasababu wameshindwa kuliendeleza.

Mimi binafsi ninailaumu Serikali kwa kumkumbatia Ndugu OTIENO OLUNG'a IGOGO aliyewanyang'anya wananchi Shamba hilo kwa ubabe licha ya wananchi kupiga kelele bila mafanikio.

Ndugu OTIENO OLUNG'A IGOGO ameuza kila kitu hapo shambani kuanzia ng'ombe ambao walikuwa takriban 2,000 sasa wamebaki siyo zaidi 200, ameuza mashine zote zilizokuwa kwenye kiwanda cha Maziwa bila kuwashirikisha wananchi.Ndugu huyu ameuza kila kitu hapo shambani.

Uharibifu huu ameufanya wakati wa Serikali ya awamu ya nne na kutamba kuwa hatuwezi kumfanya lolote.

Ni wakati muafaka Serikali KUMKAMATA Ndugu OTIENO OLUNG'A IGOGO kueleza kwa uwazi kabisa mali alizofuja na hatimaye kupelekwa mbele ya sheria.
 
Nakumbuka enzi Za utegi farm, kulikuwa na ng'ombe wengi Sana, yaani ulikuwa ukifika utegi farm kama vile umefika Texas.
Leo hii pamebaki historia, litna aduwa
 
Back
Top Bottom