Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,444
- 7,808
Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa wa Benki hiyo anayesimamia nchi za Afrika-Kusini mwa Jangwa la Sahara, Bw. Akinsowon Dawodu, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).
Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa, Dkt. Mwigulu Nchemba, aliishukuru Benki hiyo kwa kuwasilisha mapendekezo yake serikalini kuhusu namna ya kufanikisha ujenzi wa mradi mkubwa wa Reli ya Kisasa ambao utakuwa na manufaa makubwa kiuchumi si tu kwa Tanzania, bali nchi nyingine zinazopakana na Tanzania ambazo hazipakani na Bahari.
Alieleza kuwa Mkandarasi atakayejenga kipande cha Reli ya Kisasa kutoka Makutupora ya mkoani Singida hadi mkoani Tabora amepatikana na mkandarasi atayejenga reli hiyo kutoka Isaka hadi Mwanza yuko katika eneo la mradi na Mkandarasi atakayejenga reli kuanzia Isaka hadi Tabora atapatikana muda si mrefu kuanzaia sasa.
“Dira ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuona kuwa Reli ya Kisasa ya kuanzia Makutopora (Singida) hadi Mpaka Mwanza na kuanzia Tabora hadi Kigoma, ijengwe sambamba na kwa kasi, wakati huohuo Reli ya Kusini mwa Tanzania kutoka Bandari ya Mtwara hadi Mbamba bay kuelekea nchi za SADC zilizoko ukanda huo ziweze kufikiwa na reli hiyo” alieleza Dkt. Nchemba
CHANZO: Wizara ya Fedha