Serikali kukopesha Mikopo ya elimu ya juu bila kuzingatia aina ya kozi

dah tutashukuru mungu
ila mpka huo utaratibu ukamilike bas miaka na miaka itapta.
yan tutashukuru sana ikiwa hvyo
pongezi kwako mheshimiwa!
 
Upinzani uchwara watakuja kupinga
Issue sio upinzani, tatizo HESLB wameshatoa muongozo na katika muongozo huo kuna makundi tofauti ya utoaji mikopo na uombaji wa mikopo umeshafunguliwa. Hivyo ni vigumu kwa taarifa iliyo andikwa hapa kujua ukweli ni upi. Kama kuna mwenye taarifa kamili atuwekee hapa ili tujue ukweli uko wapi na pia muktadha wa tamko la waziri mkuu ni upi. Wenye wasi wasi katika hili ni wengi hivyo taarifa kamili itasaidia.
 
Uongo mtupu. Juzi bodi ya Mikopo ilitoa criterias 2016/2017 na kozi za priority ziliorodheshwa.

Waache kutudangaya.
 
Mheshimiwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa Amesema Serikali inaandaa utaratibu wa kuweza kukopesha wanafunzi wote wahitaji wa elimu ya juu bila kujali kozi wanazosoma, yaani bila kuzingatia kozi za vipaumbele "priority courses"

Chanzo : Clouds.
Ingawa umetaja chanzo cha taarifa, bado kuna maswali mengi kuhusiana na maudhui ya taarifa hiyo. Iwapo utamudu ongeza mengine yaliyotamkwa ili tusiendelee kujiuliza mwaswali tusiyoweza kujajibu hususani ukizingatia mwongozo wa Heslb uliotolewa mapema juma hili.
 
Sheria inabadilika hyo ya kusema Heslb wameshatoa mkuu kaishasema lazma wazingatie hlo.
 
Mmh mtasomeshwa lkn tatizo ajira kuna taarifa kuwa swala la ajira za ualimu zitasimama hadi miaka 3 ipita kama enzi zile za mwaka 92 taarifa rasmi itatoka j3 kwa wakubwa ,kweli namba twasoma kimyakimya hakuna huruma kwa watoto wa wasakatonge.
 
Issue sio upinzani, tatizo HESLB wameshatoa muongozo na katika muongozo huo kuna makundi tofauti ya utoaji mikopo na uombaji wa mikopo umeshafunguliwa. Hivyo ni vigumu kwa taarifa iliyo andikwa hapa kujua ukweli ni upi. Kama kuna mwenye taarifa kamili atuwekee hapa ili tujue ukweli uko wapi na pia muktadha wa tamko la waziri mkuu ni upi. Wenye wasi wasi katika hili ni wengi hivyo taarifa kamili itasaidia.
Politics as usual.....heslb washatoa muongozo NA ndio unaotakiwa kufuatwa NA si kingine
 
Back
Top Bottom