Serikali kukiri moja wa wagombea Uraisi ni mgonjwa, katiba yasemaje ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kukiri moja wa wagombea Uraisi ni mgonjwa, katiba yasemaje ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Aug 26, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Magari ya serikali yakampenia CCM

  Gazeti la Mwananchi -Thursday, 26 August 2010

  LICHA ya sheria na kanuni za Uchaguzi kuzuia matumizi ya magari ya serikali, msafara wa mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete umetumia magari kadhaa ya serikali katika mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera.
  Mbali na magari hayo, wakuu wa wilaya waliokuwa wameshiriki msafara wa mwenyekiti huyo wa CCM, walitumia magari yao ya kazi yakiwa yamewekwa namba binafsi huku wakivalia sare za chama hicho.

  Ukiondoa magari maalumu ya walinzi wa mgombea huyo ambaye pia ni rais, magari mengine ya wakuu wa wilaya na wakuu wa idara mbalimbali za serikali, yalitumika na kuwekwa namba binafsi.

  Kwa mujibu wa habari tulizozipata kutoka vyanzo vyetu zinaeleza kuwa hivi sasa Ikulu ya Dar es Salaam ina upungufu kwa kuwa wafanyakazi wa Ikulu hasa madereva pamoja na wapishi na wagawa vinywaji (waandazi), wanatumika katika kampeni za Rais Kikwete.

  Wapishi na waandazi hao wamepelekwa mikoani kulingana na ziara za kampeni.

  "Cha ajabu ni kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu hasa madereva, wapishi na waandazi wanatumika katika kampeni za CCM kupitia Rais Kikwete.

  "Wamegawanywa katika mikoa tofauti kulingana na ratiba za ziara za kampeni za rais,'' kilisema chanzo chetu.

  Juzi jijini Mwanza Mkuu wa wilaya Ilemela, Serenge Mrengo ambaye alifika majira ya saa 4:35 asubuhi uwanja wa ndege na gari lenye namba za STK 3551 huku wote wawili na dereva wake wakiwa wamevalia sare za CCM, lakini baada ya kusalimiana na viongozi wenzake, aliondoka.

  Akiwa wilayani Geita, Mkuu wa wilaya hiyo Philemon Shelutete alitumia gari lake la serikali ambalo lilikuwa limebandikwa namba T 804 BCZ huku akiwa amevalia sare za CCM. Pia gari la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Benson Katala lilitolewa namba za serikali na kubandikwa namba T 180 BKW.

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro alitetea hatua hiyo akisema sio kosa kwa kuwa Kikwete bado ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanania.

  Kandoro, alikiri kutumika kwa magari hayo ya serikali na kusema kuwa viongozi hao waliyatumia kumpokea na baadhi yao waliambatana naye katika ziara hiyo kwa kuwa mbali na kuwa mgombea wa CCM pia anayo hadhi ya urais.

  "Huyu ni Rais, amekuja kama kiongozi licha ya kwamba anagombea, bado hajavuliwa urais, sasa ma-DC walikuja kama viongozi wa serikali kumpokea rais. Kama kuna mkuu wa wilaya alivaa shati la CCM alivaa kwa sababu ya mapenzi yake kwa chama," alifafanua Kandoro ambaye alitumia gari binafsi la kiongozi mmoja wa CCM Kanda ya Ziwa.

  "Makosa ni kiongozi wa serikali kufanya kazi za chama na sioni kama kuna kiongozi wa serikali ambaye alifanya kazi za chama,"alisema

  Msafara wa Kikwete kuambatana na magari ya serikali haukuishia Mwanza na Geita pekee bali pia hata mkoani Kagera ambako magari mengi yalikuwa na namba za STK.

  Katika hatua nyingine, uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando umetoa ufafanuzi kwamba uamuzi wake wa kutoa gari la kubebea wagonjwa katika msafara wa mgombea urais wa CCM kuhakikisha usalama wa mgombea huyo.

  Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk Charles Majinge alisema kwa kawaida jukumu la kutoa magari huwa lipo mikononi mwa uongozi wa mkoa ambao uliomba gari kwao na wao waliamua kutoa gari hilo la wagonjwa namba T 848 AWN.

  "Sisi hatutoi ambulance kwa wagombea, ila tulitoa kwa Kikwete kutokana na kuwa ni kiongozi wa nchi. Kutoa magari huwa ni kazi ya uongozi wa mkoa, lakini sisi kama watalaamu wa matibabu tulichukua tahadhari na kuweka gari hilo," alieleza Dk Majinge.

  Alisema kwa vile akiwa jijini Mwanza aliwahi kuanguka, basi waliamua kuchukua tahadhari kuepuka kukosa huduma haraka iwapo jambo hilo lingejirudia akiwa mbali na hospitali ya rufaa.


  Akizungumzia gari hilo, Kandoro alisema uwapo wake ni utaratibu wa kawaida katika misafara ya viongozi wa serikali.

  "Huu ni utaratibu wa kawaida katika misafara ya viongozi, tumetoa kama utaratibu wa kawaida….unajua huyu ni kiongozi wa nchi, sasa unataka wakija na wagombea wengine wa upinzani nao tuwapatie magari ya wagonjwa, wao ni akina nani?" alieleza na kuhoji Kandoro ambaye pia aligombea kura za maoni kuwania kuteuliwa na CCM kuwa mgombea ubunge Jimbo la Kalenga na kushindwa.

  Akizungumza kwa sharti la kutotaja jina gazetini mmoja wa viongozi ambao walikuwa wakishughulika na kuratibu msafara huo alieleza kuwa gari hilo la wagonjwa ni lile ambalo lilitolewa na serikali ya Ujerumani chini ya ushirikiano wa Jiji la Mwanza na Wurzburg.

  "Gari hili liliandaliwa kutokana na maofisa wa usalama kuliomba na hili agizo limetolewa katika mikoa yote ambako atafika, kwani katika kampeni anakuwa amekwenda hadi katika wilaya ambazo haina hospitali na ikitokea dharura akimbizwe haraka hospitali huku akiendelea kupatiwa matibabu" alieleza kiongozi huyo wa chama.

  Hata hivyo, alisema gari hilo wao kama chama hawakuambiwa wala kuelekezwa kulilipia kwa vile ofisi ya mkoa ilisema watachukua wao katika hospitali ya Bugando, baada ya kuwasiliana na ofisi ya mganga mkuu wa mkoa.


  Yaonekana Ikulu, Ofisi na magari ya serikali pamoja na Hospitali zinatumiwa ipasavyo kwenye kampeni za CCM kuhakikisha Kikwete anashinda. Duh, kaazi kweli kweli !!

   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uchafu wa kutotenganisha dola na chama
   
 3. J

  Jafar JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Miaka yote ya uchaguzi hali ndiyo hiyo hiyo. Cha msingi hapa ili kukomesha hili ni KUTOWAPA KURA.
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mie nshasema
  nchi inaendeshwa kiimla hii.
  Tuwaombee wakengeuke wawe na HURUMA kwa wakulima na wafanyakazi na wajasiriamali wa nchi hii
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Unbelievable, kuwa kiongozi wa serikali wa miaka hii anaweza kuropoka namna hii.

  Kandoro wagombea wengine ni presidents to be, wananchi wakiamua. Inabidi uwaombe radhi wagombea wengine na kuwithdraw statement yako. Ni ya kipuuzi na kibaguzi.

  Pili aliyefanya wilaya zisiwe na hospitali ni nani kama sio CC wenyewe, miaka 50 baada ya Uhuru hatutakiwi kusema kuwa wilaya nyingine hazina hospitali. Hii yote inaonesha kushindwa kwa chama tawala majukumu yake muhimu kwa wananchi.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  CCM ni mwenye mbwa na serikali ndio jibwa lenyewe.
  Full kupelekeshwa
   
Loading...