Serikali kukataza wenye nyumba kukusanya kodi ya miezi 6, yasema inaumiza wengi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Serikali imesema ipo katika mchakato wa kuanzisha mamlaka itakayosimamia masuala yote ya nyumba

Kwenye sheria mpya ambayo itapelekwa bungeni itafuta wapangaji wa nyumba kulipa kodi kwa miezi 6 hadi mwaka mmoja kwa kuwa inaumiza watu wengi, badala yake watakuwa wanalipa kwa mwezi mmoja mmoja

Kodi itakuwa inalipwa kwa mwezi mmoja na utatakiwa kuweka amana ya miezi mitatu kwa ajili ya shughuli nyingine
 
Kuna Dingi mmoja Arusha alikuwa anachukua kodi yake kila siku. Yani kama kodi ya singo ni sh 30,000 basi yeye anataka buku daily, ukimpa buku 2 anakurudishia chenji yako, ukimuuliza kulikoni anakwambia hana uwezo wa kutunza pesa akipokea pesa nyingi hawezi kuzipangilia matumizi kwa kiasi.
 
real G

Wapangaji wengi watapata uvivu wa kujenga zao.

Halafu nadhani kutakuwa na kodi elekezi ambayo itakuwa na kodi ya Serikali ambayo itaenda kuiendesha Mamlaka hiyo.

Itapunguza kero za wenye nyumba kwa wapangaji ila itajenga uvivu wa kutukuka kwa wapangaji ili wasijenge zao kwani kodi ya kila mwezi mbona ni afueni
 
Back
Top Bottom