Serikali kukata rufaa upya, kupinga mgombea huru.

kuna hatari ingine, la mgombea binafsi likipita akina lowasa wakifukuzwa ccm wanakimbilia kule wanaanza kutumia vijisenti kununua wanachi halafu wanatinga bungeni na muda wengine wanatinga kwenye urais, ni lazima pia kuwe na mechanism ya ku-tackle situation kama hii
 
Madhara ya sheria hii yanaonekana kama ni makubwa kwa wananchi wa kawaida kuliko CCM, watanzania bado tunapiga kura kwa kurubuniwa na vijisenti kidogo sana, mkumbuke kuwa kuna akina RA, ED, Manji, ambao pamoja na kashifa walizonazo bado wanapenda kugombe uongozi ila CCM inaweza kuwadhibiti bila kuwapitisha na hivyo wakashindwa kutumia vijisenti vyao kuonga wananchi kuwapigia kura.

Nina wasiwasi wakiamua kugombea kama wagombea binafsi inaweza kuleta madhara makubwa kwa nchi yetu, labda ipitishwe sheria to that effect kwanza kabla ya kuruhusu hiki kitu.

Ni kweli vyama vinawabana wabunge kuongea lakini kama wabunge wetu wangekuwa ni wawakilishi wa wananchi wangelikataa hili kwenye vyama vyao kwanza, lakini wabunge wetu wanawakilisha vyama vyao na si wananchi ndo maana hawako tayari kupingana na masirahi ya chama.
 
Tufanye maandalizi ya kutosha KIFIKRA na KIMTAZAMO kwa Watanzania tulio wengi. Vinginevyo tujiandae kuwa na Wabunge na Maraisi kama Manji, Mengi, RA, Gachuma, Diallo, Bakhresa,Chenge, Lowassa, n.k., kwa sababu ya "vijisenti" vyao vs umasikini wetu. Binafsi nakubali mgombea huru hadi ngazi ya UBUNGE.

WildCard niko pamoja nawe katika msimamo huo.

Kwa nchi kama Tanzania inayoundwa na jamii changa ambazo hazina uhai wa hata Karne 2, ni wazi kuwa hazina mifumo imara inayoweka misingi juu ya masuala yanayoihusu kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Na hata kwa Tanzania kama nchi bado tu wachanga mno hasa baada ya wajanja kutuharibia safari yetu ya ujenzi wa Taifa imara pale walipoachana na ujenzi wa nchi na kuanza kula nchi.

Leo hii tumeshuhudia namna nchi ilivyovurugika kiasi ambacho anahitajika mtu jasiri wa kufanya mapinduzi (siyo ya kijeshi) ili kuirudisha nchi pale iliposimamia ili kuanzisha safari sahihi.

Tuhuma zinazowakabili wanaoitwa vigogo ni kielelezo tosha cha hatari iliyopo mbele ya Taifa letu pindi tutakaporuhusu mgombea binafsi katika ngazi ya Rais.

Tanzania hatuna mfumo wa kuweza kumdhibiti rais Dikteta atakayeweza kupenya kwa kutumia njia yoyote katika kuupata urais.

Kwa Tanzania ya leo yenye Sheria 415 za kucopy na kupaste, kuwa na rais Binafsi aliyechaguliwa kwa nguvu anazozijua, ni kuuza nchi.

Kwa Tanzania ya leo isiyokuwa na vyombo vya ulinzi na usalama vyenye
nguvu, tusitarajie neema zaidi ya maangamizi kutoka kwa Rais Binafsi.

Kwa Tanzania ya leo ambayo ni hivi karibuni tu tuliposhuhudia akina Ben na mmemwenza Mramba wakiuza nchi mchana kweupe licha ya kuwa wateule wa Chama, tusitarajie vinginevyo, endapo nchi itashikwa na Rais Binafsi.

Kwa Tanzania ya leo ambayo wasomi wakubwa waliopo vijijini ambako kuna 80% ya population ya nchi, ni wale waliohitimu kidato cha (iv) katika shule za Kata zisizokuwa na walimu huku wanaobaki huko, ni wasiyo na ujanja wa kufoji vyeti. Na si ajabu kukuta vijiji vingine hata hao waliohitimu shule za Kata hawapo kabisa.

Kwa Tanzania ya leo ambayo ili kupata ushindi wa kishindo U just need 28Bil./=
na hizo ni pamoja na zilizoibwa na wa wajanja, kadeal kamoja tu kama ka Richmond kanatosha kuchukua nchi.

EEE Mungu tuepushe na Mgombea Binafsi wa Urais
 
Naomba mnipe hizo faida tutakazo zipata wananchi kutokana na sheria hii ya wagombea binafsi..

Faida namba kubwa kuliko zote ni HAKI Mkuu, haki ya kuchagua na kuchaguliwa!
Kwa sasa haki ya mtu asiye mwanachama wa chama cha kisiasa imezuiliwa -haruhusiwi kuchaguliwa.
Ni kwanini Serikali ya Tz inatumia rasimali za watz (fedha n.k.) kuzuia haki za watz?
 
Tufanye maandalizi ya kutosha KIFIKRA na KIMTAZAMO kwa Watanzania tulio wengi. Vinginevyo tujiandae kuwa na Wabunge na Maraisi kama Manji, Mengi, RA, Gachuma, Diallo, Bakhresa,Chenge, Lowassa, n.k., kwa sababu ya "vijisenti" vyao vs umasikini wetu. Binafsi nakubali mgombea huru hadi ngazi ya UBUNGE.

Wildcard
Hao ulio wataja tunao tayari na naamini wataende CCM kwa maana ya kufanya mambo yao yawe mazuri siku zote kama CCM ndiyo itakuwa madarakani .Wazuri ambao wanachukia Nchi kuliwa wataenda kwenye kusimama wenyewe ama Vyama vingine na hapa itakuwa a full fiesta.

Mimi naomba kujua kama tunaweza kupata hukumu ile hapa .Tuone inasema nini .
 
Yaani serikali inashindwa kuipa kipaumbele kesi ya mafisadi yenyewe imekazana kupinga mgombea binafsi..ni nn wancho ogopa hapa kama serikali????naona taa nyekundu imewaka sasa inabidi wasimame na ufisadi wao...Tutapigana mpaka tumwage chozi la damu.
 
kuna hatari ingine, la mgombea binafsi likipita akina lowasa wakifukuzwa ccm wanakimbilia kule wanaanza kutumia vijisenti kununua wanachi halafu wanatinga bungeni na muda wengine wanatinga kwenye urais, ni lazima pia kuwe na mechanism ya ku-tackle situation kama hii

Mkuu Mwikimbi, heshima mbele chief.
Nimeona kweli mbeleni kutakuwa na tatizo endapo pia mafisadi hawatadhibitiwa kufanya makeke yao. na endapo itakuwa kweli wataweza kuwanunua wengi wetu, basi ina maana vyombo vya usalama wa Taifa vitakuwa vimelala kikatiba
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kimetangaza kusudio la kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa na Jaji Robert Makaramba wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu kesi ya matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Karatu.
Akitangaza kusudio la kukata rufaa ya hukumu hiyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mohamed Mbonde alisema uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo umefikiwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa katika kikao chake kilichofanyika Mei 17 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Katibu huyo kusudio hilo la kukata rufaa litawasilishwa mahakamani wiki hii kabla rufaa yenyewe mwezi ujao.
“Katika kikao hicho Kamati ya Siasa ilijadili kwa kina hukumu hiyo na kukubaliana kuwa hukumu ya Jaji Makaramba haikuwatendea haki wana CCM,” alisema Mbonde jana ofisini kwake.
Alisema kati ya vipengele ambavyo wanaona havijawatendea haki kile cha idadi ya kura zilizokosewa kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Solanus Nyimbi.
“Lakini hapa tunaomba Watanzania watuelewe kuwa CCM inachotafuta ni haki yake na tutatumia taratibu za kisheria kuwa haki hiyo inapatikana,” alisema Mbonde.
Alisema Kamati hiyo ya siasa katika kikao chake imeamua mlalamikaji katika kesi hiyo ya rufaa atatangazwa baadaye pamoja na mawakili watakaowatumia.
Hukumu ya kesi hiyo liyofunguliwa na wanachama watatu wa CCM wakiongozwa na Joseph Haymu kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 yaliyompa ushindi mgombea wa Chadema Dk.Wilbrod Slaa dhidi ya Patrick Tsere wa CCM, ilitolewa Mei 15 mwaka huu.
Katika hukumu yake Jaji Makaramba alisema kuwa Mahakama imeridhika kuwa Dk. Slaa alikuwa mshindi halali wa uchaguzi huo na kura zilizokosewa kuhesabiwa ziliwaathiri wagombea wote wawili lakini hayakuathiri matokeo ya uchaguzi huo.
Source: HabariLeo
 
CCM wapumnzike sasa je ikifika 2010 watakata rufaa ngapi????waanze kufungasha mizigo yao na wale walio kuwa na nyumba ndogo DOM waanze kuziamishia Dar kwani sijui kama wengi wao watarudi mjengo....
 
Nangoja kusoma vigezo vyao ya kukata rufaa .Hivi mimi nilidhani watu wa jimbo lile ndiyo wanao kataa rufaa kumbe ilikuwa CCM mkoa ? haya wacha tuangalie
 
Duh wamelamba wa chuya hata wakate rufaa 20 Slaa ataibuka kidedea tu hivi kuna wakiri gani hapa TZ ambaye yupo juu zaidi ya TINDU LISSU??
 
Baba H,
CCM sijui wasiwasi wao uko wapi, kama wanafanya hivyo kwa makusudi ya kumminya Dr. slaa hakika watakuwa wamechelewa, sanasana wanataka kumuongezea umaarufu, watanzania wameshaamka wanaelewa kinachoendelea, wasisahau yale ya zitto kule Mjengoni, sasa zitto anajulikana tz nzima. nawashauri ccm waachane na kesi hiyo kama watatusikiliza.
 
Haya wanajamii forums, hili nalo mnalisemeaje? Balali naye angeweza kugombea 2010 si fedha anazo?

Mgombea huru hapana - Serikali

2008-05-21 09:55:05
Na Mwandishi Wetu


Ikulu imesema serikali inakusudia kuwasilisha rufaa mahakamani kupinga mgombea binafsi.

Kuhusu baadhi ya viongozi wa chama tawala na serikali kuunga mkono hoja ya mgombea huru, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu, amesema wana haki ya kutoa maoni yao, lakini msimamo wa serikali ni kupinga.

Wiki iliyopita Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali rufaa ya serikali iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupinga kuwepo na mgombea binafsi kwenye chaguzi mbalimbali.

Hatua hiyo inafuatia Mwenyekiti wa DP, Bw. Christopher Mtikila, kufungua shauri Mahakama Kuu kupinga kifungu cha katiba cha kulazimisha mgombea wa nafasi za kisiasa kuwa na chama.

Mahakama ilikubaliana naye na kutaka kifungu hicho namba 39 (1) na 69(1) kufutwa.

Lakini serikali ilikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, rufaa ambayo ilitupiliwa kwa maelezo kuwa haikujitosheleza. Hata hivyo serikali imesema haitakaa kimya na inakata rufaa zaidi.

Mwenyekiti wa CCM (Bara), Bw. Pius Msekwa, aliunga mkono maamuzi hayo akisema ni mwafaka na kusisitiza kuwa haoni sababu ya kuendelea kubishania suala la mgombea huru.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Bw. Rweyemamu alisema serikali itakata rufaa na ni haki yake kufanya hivyo.

Bw. Rweyemamu ambaye alikuwa akijibu maswali ya wanahabari alisema serikali ina haki ya kuwasilisha rufaa licha ya baadhi ya viongozi wa chama tawala kutaka kuwa na mgombea huru.

Alipoulizwa na waandishi sababu za kukataa mgombea huru wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM, chama kinachounda serikali ameridhia kuwepo mgombea huru alijibu: ``Msekwa ana haki ya kuzungumza kama yeye. Ana haki ya kutoa maoni yake, huwezi kumzuia, lakini ni haki ya serikali kukata rufaa na itaendelea.``

Alipoulizwa kuwa kupinga kuwepo kwa mgombea binafsi ni kupingana na katiba ambayo ni sheria mama inayotoa haki ya kila raia kuchagua na kugombea kuwa kiongozi, alisema licha ya katiba kutoa haki hiyo lipo sharti dogo linalotaka ili kuchaguliwa lazima mgombea apitie kwenye chama.

``Katiba inaruhusu lakini kwa nini uangalie katiba pekee wakati kuna sharti jingine la kuwa mwanachama?`` Alihoji.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa, alikaririwa na vyombo vya habari akisema, anaunga mkono kuwepo mgombea huru.


SOURCE: Nipashe

Tuma Maoni Yako
 
Mwelewesheni maana kauliza ama kuna Wakili top kama Lissu.Kupondea si jibu .Inawezakana Lissu yuko juu ila hana publicity sasa unaweza kubisha nakutaja hao kwa kuwa wana andikwa .Lakini kesi a Slaa haikuwa kesi ndogo kushinda .Lissu naye ni mwamba kesha ishinda CCM na Serikali mara kibao .Mfano kesi ya Tarime ya Chacha Wangwe .Mkuu wa Wilaya Mabiti aliona aibu ya mwaka wakati ule .Kuna kesi za mauaji ya Bulyanhulu nk bado serikali haina majibu na Mrema aliyesema kwa kuambiwa na Lissu anapenda .Je una sababu yeyote ambayo inaweza kufanya asiwe top ama among the tops ?
 
Ikulu yampinga Msekwa

na Kulwa Karedia
Tanzania Daima

OFISI ya Rais Ikulu imekataa kuyatambua maoni ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa, kuhusu kuruhusiwa kwa wagombea binafsi.

Msimamo huo wa Ikulu ulitangazwa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Mwasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Rweyemamu ambaye alikuwa akitetea uamuzi wa serikali kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama ya Rufaa iliyoruhusu kuanza kutumika kwa mfumo wa kuruhusu wagombea binafsi, alisema msimamo wa Msekwa kuunga mkono uamuzi wa mahakama ni wake binafsi.

“Haya ni mawazo ya mzee Msekwa… Katiba yetu inaruhusu kila mwananchi kutoa maoni yake, naamini hata uongozi wa CCM utatoa tamko kuzungumzia suala hili,” alisema Rweyemamu.

Alisema pamoja na kauli hiyo, tayari serikali imewasilisha Mahakama ya Rufaa taarifa ya kupinga uamuzi wa kuwapo kwa mgombea binafsi.

“Pamoja na mahakama kuruhusu, serikali imekata rufaa juu ya jambo hili. Hapa kila mtu ana haki ya kukata rufaa na kuona mwisho wake, sasa nawaomba msubiri hadi mwisho juu ya suala hili,” alisema Rweyemamu.

Katika hatua nyingine, Rweyemamu alieleza kuunga mkono msimamo wa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, wa kukitaka Chama cha Wananchi (CUF) kumtambua kiongozi huyo kama sehemu ya kuimarisha jitihada za kusaka suluhu ya kudumu ya matatizo ya kisiasa Zanzibar.

“Nadhani mawazo yaliyotolewa na Rais Karume juu ya suala hili ni ya msingi, ambayo yanapaswa kutambuliwa na CUF, sasa ni wakati wao kukaa chini na kutafakari suala hili kwa kina, ili mazungumzo (ya muafaka) yaweze kuendelea,” alisema Rweyemamu.

Alisema Rais Karume yuko madarakani kihahali kutokana na kuchaguliwa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, hivyo anapaswa kupewa heshima zote kama kiongozi wa Zanzibar.

“Kwa vile kila upande umetoa maelezo yake, jambo la msingi ni kurudi mezani na kuendelea na mazungumzo kama alivyosema Rais Jakaya Kikwete wiki iliyopita,” alisisitiza Rweyemamu.

Alisema jambo kubwa linalotakiwa hivi sasa ni kuendelea kuheshimu uamuzi huo wa Rais Kikwete na Rais Karume, ili kuona siku moja wanafikia muafaka.

Alisema hadi sasa, CCM imekuwa ikiisihi CUF kurudi kwenye mazungumzo hayo, na licha ya habari kwamba CUF imegoma jambo ambalo alisema si kweli.

Alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya Rais Kikwete kuingia kati kuokoa mazungumzo hayo, Rweyemamu hakukubali wala kukataa, na kusema kuwa, rais ana njia nyingi za kufanikisha suala hilo.

“Ndugu zangu rais ana njia nyingi ambazo anaweza kuzitumia katika kufanikisha mazungumzo haya… sasa siwezi kusema kwamba ataingia kwenye mazungumzo kwa vile kila chama kinamwakilishi wake,” alisema.

Kuhusu mapigano ya koo za Wanchari na Wakira yanayoendelea wilayani Tarime, mkoani Mara, Rweyemamu alisema serikali imechukua hatua zote za kuyadhibiti haraka.

“Haya mapigano yamekuwapo siku nyingi, lakini serikali imechukua hatua za haraka katika kupambana na suala hili, viongozi wa mkoa wapo wanaendelea kuzungumza na wananchi,” alisema Rweyemamu.



Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 26 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)

Ndugu S. Rweyemamu si mwandishi wa habari tena, bali ni mtoa habari za serikali (mouth piece). Hii inasikitisha.

Lakini kimsingi, CCM inajua ina vigogo wengi tu ambao wakipewa fursa ya kugombea kibinafsi watakihama chama maana chama tangu kale kimekuwa kinanuka ufisadi... Hofu hiyo ndiyo inawafanya waogope wagombea binafsi hata kama hiyo inafisha haki za msingi za kikatiba za Watanzania. Fikra zao ni kongwe kama chama chenyewe.

na Mwanambuu s., Dar es salaam, - 21.05.08 @ 10:28 | #12125

Salva Reyemamu kwa nini critics zako na integrity yako imeshuka hivyo tangu upewe hiyo kaziya utarishi hapo ikulu?
Kweli njaa kitu mbaya sana, inaweza ikakufanya ukawa unatenda mambo ambayo kila mtu anakushangaa.

na Joseph, mwanza, - 21.05.08 @ 08:03 | #12133

Hii ndio demokrasia ya kweli makamu wa chama kutofautiana na mwenyekiti wake. Lakini suala ni nini hapa - CCM wanataka watu wapitie kwenye chama ili 'takrima na uchafu mwingine' ufanyike. Hii ni constitutional right na ni lazima haki ipatikane . Haki yetu!! Haki yetu!! Haki yetu!!!

na chaloo heri, TZ, - 21.05.08 @ 08:11 | #12139

ALIYEWADANGANYA UGOMBEA BINAFSI UTAONDOA TAKRIMA NA RUSHWA KWENYE UCHAGUZI NI NANI?

MBONA MADEREVA MNATOA SANA RUSHWA KWA MATRAFIKI INGAWA LESENI ZENU HAMKUZIPATA KWA TIKETI ZA VYAMA VYA SIASA BALI KAMA WATU BINAFSI?

WATANZANIA RUSHWA MNAZO KWENYE DAMU ZENU WALA HAZITOKANI NA VYAMA VYA SIASA.

na mviziaji, Bongo, - 21.05.08 @ 08:22 | #12167

mie naona salva ni msemaji ammbye anachukua maoni na kuyatoa hewani, si yake binafsi, mie nilishafanya kazi za aina hiyo, ni mara chache unatoa yako binafsi mostly unaagizwa kufanya so is not salva.in genaral mie nimefurahia sana sana kwani nasi wengine tutaweza kushika nafasi fulani maana mambo ya kupitia ccm wengine hatukuwa tunayapenda kwanza kuna kujuana sasa nimefurahi, maana hii nchi imekuwa sasa kama ya kifalme hivi.watoto wa mskini imekuwa ngumu kuwepo katika nafasi nzuri hata asome vipi!

na mama jav, DAR, - 21.05.08 @ 08:26 | #12169

naomba mchunguze ajira za watoto wa vigogo ministry of foreign affairs....

na mama Jav, dar es salaam, - 21.05.08 @ 08:29 | #12170

Hivi hawa CCM wanavyokataa mgombea bunafsi kwa manufaa ya nani? wanaogopa nini! wawaacha watu wenye hela na safi wagombee siyo kuwalazimisha wapitie kwenye uozo wao wa CCM.




na kassim,tegeta, dar, - 21.05.08 @ 08:31 | #12173

Mama Jav,
Ajira za watoto wa vigogo, ministry of foreign affairs ni mwanzo tu. Huu uchafu umenea kila sehemu nenda BOT, TRA etc. Lakini iko siku tutapata haki yeu.

Nenda chuo kikuu huria, OUT, VC anaajiri hawala zake, watoto wa ndugu zake. Watu wamelalamika lakini wapi. Yeye na Hosea wa Takukuru wanakula sahani moja. Bongo hiyo!!!!!!!!!!!!

na chaloo heri, tz, - 21.05.08 @ 08:39 | #12178

CCM kuendelea kukataa kuwepo kwa wagombea binafsi kunadhihirisha kitu kimoja kwamba uongozi ndani ya CCM unapatikana kwa mizegwe. CCM Wanaogopa kwamba mgombea akiondolewa kwa mizegwe atasimama kama mgombea binafsi.

Tuungane wote kudai haki yetu ya msingi ya kuchangua na kuchanguliwa bila kulazimishwa kupitia vyama. Mbona hao wabunge na Rais hawapigiwi kura na wanachama wa vyama pekee??!!

na Ron, TZ, - 21.05.08 @ 08:48 | #12180

Tusimhukumu salva, labla apimwe afya ya akili



na mange, Sengerema, - 21.05.08 @ 08:55 | #12185

Jamani huyu salva ni njaa tu inayomsumbua.hizi njaa zinaweza kukufanya umsifie hata shetani!!!!!!!!

na kakaa, mwanza, - 21.05.08 @ 09:04 | #12190


CCM hamuwezi kukwepa mafuriko na hata mkikataa wagombea binafsi hamtaweza kushindana na nguvu za wakati, kaeni chonjo saa mbaya, wasomi kama kina warioba,msekwa washayasoma haya

Muulizeni Mugabe

na lualua chilamba, mbeya, - 21.05.08 @ 09:34 | #12207

Ujue kila mtu ana uhuru wake wa kutoa Mawazo mm sioni tatizo la Salva yeye kama msemaji wa ikulu katoa tamko kuhusu serikali na Msekwa yale ni mawazo yake kama Msekwa na si kama CCM hivyo Tanzania muda wa kuwa na wagombea Binafsi bado na ni mbaya tutawapata Madikteta ww achana na utamu wa kushika Dola


na Mkula, Namanga, - 21.05.08 @ 09:40 | #12210

Ujue kila mtu ana uhuru wake wa kutoa Mawazo mm sioni tatizo la Salva yeye kama msemaji wa ikulu katoa tamko kuhusu serikali na Msekwa yale ni mawazo yake kama Msekwa na si kama CCM hivyo Tanzania muda wa kuwa na wagombea Binafsi bado na ni mbaya tutawapata Madikteta ww achana na utamu wa kushika Dola


na Mkula, Namanga, - 21.05.08 @ 09:40 | #12211

jamani huyu salva ni mtoa habari tuu,na habari anazozitoa ni zile anazopewa na maboss zake!!kwa hiyo tusimlaumu huyu salva!!

na mwahu y, tanzania, - 21.05.08 @ 09:43 | #12212

tukiviacha vyama vya siasa kututeulia watu safi wanaotufaa kuongoza nchi tutajikuta nchi tumeikabidhi mikononi mwa mabepari.mfumo uliopo utoshe tusiigize mapendekezo mengine ambayo yatakuwa hatarishi.tukiruhusu wagombea binafsi hao mafisadi tutakuwa tumewapa njia ya kuipindua nchi kwa kutumia fedha zao.tatizo la watanTZ njaa tunaiweka mbele kuliko maslshi ya taifa.mfano mzuri uchaguzi wa kumpata mgombea ndani ya CCm pale Dodoma 2005

na uswege, tukuyu, - 21.05.08 @ 09:49 | #12216

salva hana kosa kwani yeye hayamtoki mdomoni huyu ni RAIS we2 ambaye 2mechagua kwa kura nyingi kumbe hata mzee msekwa bado wamo, hapa hatuna Rais chenzyy huyu hamna ki2 hapa anajua mafisadi wote watahama ccm yeye anaogopa.

na john - 21.05.08 @ 09:53 | #12220

Hili la mgombea binafsi haliwezi kufunikwa wala kufa.Ni haki ya wananchi.
Kuhusu vita ya KOO huku Tarime ,MSEMAJI wa Ikulu S.Rweyemamu amesema ni la siku nyingi na Serikali inalishughulikia.Sawa,lakini Serikali mbona halitafutii suluhisho la kudumu.Mwaka jana mwezi Agosti Mhe.Lowassa alihutubia pale Tarime uwanja wa Saba Saba na akaahidi hatua zitachukuliwa akiwepo RC Mara, Dc wa Tarime;na viongozi wengine wote.Mpaka leo hakuna la maana likifanyika kufualtilia ahadi ya Lowassa na nyingine za huko nyuma.Pia vita ya sasa Tarime imechukua sura mpy zaidi na ya hatari kwa Taifa kwa sabubu watu wa upande mmoja sasa wanazo silaha za kisasa hasa bunduki ambzo wanazitumia mchana kuua wanachi;kupora mali hasa mifugo.Inaonekana baadhi ya watu wavamizi hawa wanatoka vijiji vya jirani hata nchini Kenya .Nyumba kadhaa ZA WANCHI bUNCHARI ZIMECHOMWA MOTO;CHAKULA KIMECHOMWA MOTO;SHULE ZIMEFUNWA;WATU WAMEUAWA na kadhalika.
Polisi waliopo vjijini hapa ni wachache mno na hawana nyenzo kamili ;na kufuatilia ni kidogo.Watu hwana pa kuishi;wameporwa mali;hawana chakula;na mateso meengi tu.
wANACHI TUNAOMBA Waziri MKUU na Rais Kikwete waingilie kati janga hili la miaka 15 sasa.Wawajibishe viongozi wa Mara hasa mKUU MKOA NA wILAYA YA Tarime na wasidizi huisika kwa kushindwa kufualitia na kutatua janga hili kama alivyoahidi Lowassa mwaka 2007.Pia Idara ya Polisi iongezee vituo vidogo vya polisi pale kwenye mapigano hasa vijijini vya REMAGWE; ngeregere;mote morabu;na Korotambe.
MBunge wa Tarime ndugu Chacha Wangwe usaidie hili janga liishe.Wanachi wanasubiri hatua yako.







na nia, mza, - 21.05.08 @ 10:05 | #12228

Hivi ni kweli Ballali amefariki?

na salme - 21.05.08 @ 10:07 | #12231

Jaman salva kama walivyotamka waungwana ni kwamba ni njaa inamsumbua na yuko pale kuganga njaa tu,kama shoga tu anavyoinamishwa,wanatetea uozo hao watawala,

na Kijita, Singida, - 21.05.08 @ 10:35 | #12242

Watanzania msilalame sana. Kwani nyie hamjui ni nini suluhisho la haya yanayotokea? Chukueni hatua za haraka kulinusuru taifa.

na James - 21.05.08 @ 11:28 | #12266

Hivi ni kweli Balali amefariki dunia ?.
Nimebahatika kuona nakala ya gazeti la Tanzania Daima ya leo,sijui kama mmetoa matoleo mawili tofauti kwa siku moja.Naamini kutoka moyoni jamaa kauwawa na mafisadi ili kupoteza ushaidi,S Rweimamu alisema serekali ikimuhitaji itampata kumbe walikuwa wanapoteza muda tu walijua Balali lazima afe.Mafisadi sasa watapumua vizuri kwasababu shahidi namba moja katangulia mbele ya haki.Tanzania imeingia katika mtandao wa mafia(mafisadi) kila wanachotaka kiwe kinakuwa.

na G KABONDE, ARUSHA,TANZANIA, - 21.05.08 @ 11:58 | #12272

Inasikitisha kuona watanzania wengine wanapenda kumwiga tembo kujisaidia!
Kuwa na mgombea binafsi kwa nchi maskini kisiasa, ambayo haijazoea siasa za kibepari kamaTanzania kuna lisaidia taifa nini? Inalichukua taifa siku ngapi kuhesabu kura? inaichukua nchi fedha kiasi gani kugharamia ruzuku za vyama? Mgombea binafsi wa tanzania atahitaji kuwa bilionea mkubwa sana wa kugharamia shughuli zote za kampeini; usafiri, kuandaa majukwaa, ya mkutano, kupata ulinzi, kutafuta wamachinga wa kumpamba.
SIKU HIZI MADAWA YA KULEVYA YAMEENEA SANA!! SISHANGAI WANANCHI FULANI KUTAMKA HIVYO!!!

na Genzi - 21.05.08 @ 12:09 | #12275

BALLALI HATUKUTAKA AFE, TULITAKA APATE AFYA NJEMA ILI TUWAJUE AKINA KIKWETE WAPO UPANDE GANI. NA INAWEZEKANA KABISA MAFISADI WAMEMUWAISHA ILI KUPOTEZA USHAHIDI, LAKINI MUNGU YU PAMOJA NASI HIVYO TUTAWAJUA TU NA MBELE ZA HAKI MTAFIKISHWA. KWANI WAPO WAPI AKINA CHARLES TAYLOR NA WENGINE?

na Solomoni - 21.05.08 @ 12:30 | #12278

bado hatujawa tayari kuwa na mgombea binafsi sana sana mafisadi ndiyo watafurahia hili.

na petro, tanga, - 21.05.08 @ 13:53 | #12316

Nilishawahi kusema na ninarudia,tatizo hapa ni Katiba mbovu na haifai ndiyo maana haiheshimiwi.Kama katiba inaruhusu mgombea binafsi,nani wa kuipinga? ni dhahiri inapingwa kwa sababu haina maana yoyote wala haiheshimiki.

Mimi sijaelewa sisi watanzania tunamtumikia nani au hawa viongozi wanamtumukia nani ambaye ana uwezo hata wa kutoiheshimu katiba ya nchi,ni nani huyo?

Ni lini tutakuwa taifa lenye kujiamini na kuheshimu vyombo vyake muhimu kama katiba ya nchi?
ukishaona katiba haiheshimiwi unategemea kitu gani hapo?kama mahakama ni chombo kilicho halali cha kutafsiri sheria,na kimeshatoa hukumu ya kuhalalisha kuwa ni sahihi kikatiba mgombea binafsi,aafu mtu mwingine anapinga,na yeye ndiye anayesikilizwa,kulikoni hapo si ni uozo tu.
Inatia shaka jinsi mtu wa kawaida anaweza kuamini taratibu hizi.ndo maana vibaka wanashughulikiwa hukohuko mitaani na watu wenye hasira maana wameshadharau vyombo vya sheria kwa sababu viongozi wenyewe wa nchi wameonyesha mfano wa kudharau katiba mama ya nchi.sasa hapa alaumiwe nani?ndo maana naiona tanzania kama kisiwa cha watu wa kusadikika ambao mambo yao ni ya kusadikika tu. kila mtu na lwake yote mbele kwa mbele

Hpa ninatabiri kuwa matokeo yakutoheshimiwa kwa katiba ya nchi ni kuwa kitazuka kizazi cha kuwa na msimamo wa kujikomboa,kama tulivyojikomboa kwa mkoloni.Maana lazima iwepo tofauti kati ya uongozi wa kikatiba unaoheshimu katiba ya nchi,na huu wa sasa ambao kila kukicha unakinzana na katiba yenyewe.Sasa kizazi hicho kitatumia mbinu gani Mungu anajua.

na Andrew Gadi Mrinji, Geita/Tanzania, - 21.05.08 @ 14:11 | #12326
 
Pundit,
Mkandara,

Faida ya kwanza, kuna wanachama wengi wa CCM kwenye uongozi ambao wamechoshwa na CCM lakini hawana chama kingine kizuri cha kujiunga nacho, wanaweza kuuzika kwa wananchi kama watu binafsi.Watu hawa ambao ufisadi wa CCM umewachosha kwa sasa wanalazimika kugombea ubunge, urais na nafasi nyingine kwa tiketi ya kifisadi ya CCM ambayo inakuja na masharti kibao yanayowaondolea independence na integrity yao.
Kwa hiyo faida moja itakuwa siasa zitakuwa na uhuru zaidi.
Faida ya pili hata kina sie ambao hatujaona chama chochote cha kujiunga nacho tutaweza kupata nafasi na haki yetu ya kugombea uongozi.Mimi binafsi siamini katika organizations na ninaamini zaidi katika "the power of individualism", katika mfumo wa sasa itabidi nikubali katiba nisizozielewa naku pay some lip service kwa policies ambazo siziamini.Mimi nataka niwe na nafasi ya kwenda kuongea na wananchi wa Tanzania kama mimi, ukiingia bungeni kama unataka kublast unablast tu hakuna upumbavu wa vikao vya discipline vya chama wala nini.
Kama sheria ya mgombea binafsi ingekuwepo 2005 huyu rais wetu bogus asingeweza kupata urais kirahisi hivi, na pengine mtu kama Salim angeweza kumchallenge kama mgombea binafsi.
Kukatalia wagombea binafsi siyo tu kunawanyima Watanzania wasio na vyama nafasi ya kuchaguliwa, bali pia vinawanyima Watanzania wigo mkubwa wa watu wa kuwachagua.
On closer examination not having a private candidate is at best constitutional but a violation of human rights, the very rights the constitution is entrusted with protecting, as stated above.
At worst the constitution is contradicting its earlier spirit (Ibara ya 2) katika ibara za 5, 39 na 67.

Mkuu hii ndio hofu yangu kubwa sana kwamba Siasa zitakuwa WATU badala ya CHAMA. yaani hao kina salim wanaondoka CCM kwa sababu ya watu fulani hali kimrengo na sera watakuwa wanatangaza kile kile wanachosema CCM... Hii itawalazimu wananchi kumchagua mtu nje ya chama hali mtu huyo anachojaribu kusema ni kile kile kinachotangazwa na vyama vinginevyo...
Hivyo siasa zetu zitageuka na kupikwa kwa sura za watu badala ya vyama jambo ambalo limezikumba nchi zote za Kiafrika. Viongozi kuhama chama fulani kwa sababu hawana KULA ama uhasama kati yao.. Wakipewa madaraka wanafanya vile vile kama wale waliotangulia kwa sababu vyama vyao havina mrengo na wala hawakuwa na sera isipokuwa hasira za kutoelewana na mtu fulani ndani ya chama.
Je, hii itaendelea hadi lini ikiwa leo simpendi Freeman basi nihame Chadema niingie CCM ama nianzisha chama changu.. wangapi watakuja na vyama hivi binafsi kwa kufikiria kwako tu.Kila mtu atataka kugombea Urais na kisheria hawa watu wote ni lazima wapewe fungu la fedha toka serikali kuendesha kampeni zao Kitaifa. Je, uwezo huo tunao kama watakuja wagombea 30 hadi 50 wa urais?.. it's possible kabisa kuwa na hesabu hiyo kwani mwaka jana tu tulikuwa na vyama visivyopungua 18..ina maana wagombea Urais 18 bado hatujahesabu huko visiwani.
Kweli yawezekana CCM wanaogopa kuwapoteza watu kama salim lakini kama kweli hawa watu ni wana siasa wanashindwa nini kujiunga na chama kimojawapo ama kuanzisha chama chao wenyewe ambacho kitajitangaza kwa wananchi ili kupata support..
Sioni kinachowashinda kwa sababu hata ukijitangaza mgombea binafsi tayari utakuwa umeshatoka CCM hivyo kama hofu ni Ku Kolimbiwa hujaepuka kitu. Mbona kina Mtei, Mrema,Seif hawa wote walikuwa CCM wameweza vipi kiasi kwamba iwe ngumu kwa Salim.
Hii habari ya Human right mkuu sidhani kama ina apply hapa, kwa sababu mgombea Binafsi ni yule asiyekubaliana na mrengo wa chama chochote na mwenye kusimamia sera ambayo haikubaliki ama haina umuhimu kwa vyama vinginevyo..So what do they bring?..na nini uhalali wake ktk mazingira uliyopo maanake Huwezi kulilia haki ya kibinadamu kama vile UKIMBIZI ktk nchi ambayo haipokei WAKIMBIZI..
Kuna cnchi zinaruhusu Suicide kama ni haki ya mgonjwa lakini sii kote duniani hata kama itapitishwa na UN.. Kuna haki za uzawa leo hii hazitambuliki Tanzania kwa sababu tu ya kuhama nchi na wapo watu wanaunga mkono serikali kukataa dual citizenship!..
Hivyo hili swala linahitaji debate ya nguvu na kulitazama zaidi nje ya sura yake...
 
Back
Top Bottom