Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,731
- 40,838
habari Leo
SERIKALI kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imeanza taratibu za kuwasilisha tena rufani inayopinga mgombea binafsi baada ya Mahakama ya Rufaa kutupa rufani yao kutokana na kubaini kasoro kadhaa.
Alhamisi iliyopita, Mahakama ya Rufaa ilitupa rufani ya serikali inayopinga mgombea binafsi baada ya kubaini kasoro kadhaa katika rufani iliyowasilishwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Akizungumza na gazeti hili jana, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe alisema taratibu hizo zilianza mwisho wa wiki iliyopita, ikiwa ni siku moja baada ya uamuzi huo wa Mahakama ya Rufaa.
Mbali na kuwasilisha rufani yao, Waziri alisema lengo la kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu wa kuruhusu mgombea binafsi wa urais na ubunge ni kutaka uamuzi kama huo utolewe na mahakama ya juu zaidi nchini ambayo ni Mahakama ya Rufaa.
Alipoulizwa kama Mahakama ya Rufaa ikitoa uamuzi sawa na wa Mahakama Kuu wa kuruhusu mgombea huyo binafsi, Chikawe alisema serikali haitapinga na itatekeleza mabadiliko ya sheria na kuyawasilisha bungeni kwa kipindi ambacho mahakama itaamuru.
Awali katika hukumu ya Mahakama Kuu iliamriwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kufanya marekebisho ya Sheria Namba 34 ya 1994 ambayo inapingana na kifungu cha 21 (1) cha Katiba ambacho kinampa haki ya kugombea na kupiga kura.
Mahakama Kuu ilimpa Mwanasheria Mkuu kati ya Mei 5, 2006 hadi uchaguzi ujao awe imewasilisha bungeni sheria inayotoa fursa ya kuwapo mgombea binafsi katika uchaguzi bila kutegemea chama chochote.
Kutokana na uamuzi huo wa Mahakama Kuu uliotolewa na majaji Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo, serikali ilikata rufaa ambapo inadai Mahakama Kuu ilikosea kisheria katika kutafsiri Ibara ya 21 (1) ( c ), 39 (1) (c ) (b) na 69 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachompa haki mtu ya kugombea na kupiga kura.
Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa John Mroso, Edward Rutakangwa na Engela Kileo walitoa hukumu ya kutupilia mbali rufaa ya serikali, hali iliyompa ushindi tena Mwenyekiti wa Democratic Party, (DP), Christopher Mtikila, ambaye amekuwa anahangaika na kuruhusiwa mgombea binafsi tangu mwaka 1993.
Mtikila baada ya kubaini kuwa kuna kasoro katika rufani ya serikali, aliwalisilisha pingamizi mahakamani hapo akidai kuwa ina kasoro kutokana na tarehe iliyoko kwenye amri ya hukumu kuwa tofauti na tarehe iliyoko kwenye hukumu ya Mahakama Kuu.
Katika pingamizi hilo, Mtikila kupitia kwa mawakili wake Richard Rweyongeza na Mpale Mpoki, waliliambia jopo la majaji hao kuwa rufaa hiyo haikuwa na rutuba ya kisheria kutokana na dosari hizo za tarehe tofauti kwenye amri na kwenye hukumu ya mahakama hivyo wakaiomba mahakama kukataa kusikiliza rufani hiyo.
Majaji walikubaliana na hoja za mawakili wa Mtikila wakisema kuwa amri hiyo (kikaza hukumu) ilikuwa hairekebishiki kwa kuwa ilitengenezwa Februari mosi mwaka jana wakati hukumu ya Mahakama Kuu juu ya suala hilo ilitolewa Mei 5, 2006.
Wanasheria Waandamizi, Joseph Ndunguru na Mathew Mwaimu waliokuwa wanaiwakilisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, waliiomba mahakama kukataa pingamizi hilo la Mtikila kwa vile suala hilo liliwasilishwa Mahakama Kuu chini ya sheria za haki za binadamu ambayo haihitaji kuwasilisha amri ya hukumu.
Kwa mujibu wa wanasheria hao walidai kilichokuwa kinabishaniwa siyo agizo la hukumu, bali maamuzi ya mahakama nyingine kwa hiyo hapakuwapo na sheria inayotaka tarehe iliyoko katika amri ya hukumu iwe sawasawa na ile iliyoko katika hukumu kama sheria inavyoelekeza kwenye agizo la hukumu.
Majaji kwa upande wao walisema maamuzi kama hayo yanaendana na sheria za mwenendo wa kesi za madai zinazohitaji amri ya hukumu yoyote ionyeshe tarehe inayofanana na ile iliyoko kwenye hukumu.
Mtikila alifungua kesi hiyo Februari 17, 2005 akiiomba mahakama kutamka kuwa ni kinyume cha Katiba ya nchi kupinga kuwapo kwa mgombea binafsi katika nafasi za kisiasa.
Katika uamuzi wa Mahakama Kuu, jopo la majaji watatu liliruhusu kuwapo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi, kwa sababu katiba ya nchi inatoa haki hiyo.
Majaji hao walibainisha kuwa katiba inatamka wazi kuwa kila mwananchi anayo haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi na haiweki masharti kuwa hilo lifanyike kwa mtu kujiunga na chama fulani.
Mwaka 1993, Mtikila alishinda kesi kama hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, lakini licha ya uamuzi huo wa mahakama, Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi na ndipo Mtikila alifungua kesi hiyo ya kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kushinda tena.
My Take:
Nyerere aliwaambia pale Uwanja wa Sokoine kuwa uamuzi wa serikali kufuta haki ya mtu kuchaguliwa kwa vile hataki kujiunga na chama ni uamuzi wa kipumbavu. He was right and still is. Kama mtu ambaye hana chama anaweza kupiga kura kumchagua kiongozi amtakaye, iweje mtu asiye mwanachama anyang'anywe haki ya kupigwa kura na watu wanaomtaka? Haki ya kuchagua na ile ya kuchaguliwa inatokana na haki ya raia. Kama raia anayo haki ya kumchagua amtakaye basi anayo haki pia ya yeye mwenyewe kuchaguliwa na yeyote yule.
Kwanini hata hivyo CCM inahofia sana mgombea binafsi? au wanakumbuka yale ya Chifu Sarwat wa Mbulu.