Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Serikali imesema imeanza mchakato wa kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Uingereza dhidi ya Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL).
ATCL imeamriwa kulipa Dola 30.1 milioni (Sh69.23bilioni) kwa kampuni moja ya Liberia kama fidia baada ya kuvunjika kwa mkataba wa kukodisha ndege.
Kesi hiyo inahusu makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2013 na aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mattaka ya kukodisha ndege aina ya Airbus kutoka kampuni ya Willis Trading.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Uingereza, Christopher Butcher aliiamuru ATCL kulipa fedha hizo pamoja na riba inayoweza kufikia dola 10 milioni (Sh23 bilioni) kwa kampuni hiyo ya Liberia, ambayo inajishughulisha na masuala ya kuuza na kukodisha ndege, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa.
Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi aliliambia Mwananchi kuwa mkataba wenyewe ulikuwa wa kifisadi wa kuitia nchi hasara.
Dk Kilangi alisema kuwa serikali imewasiliana na ofisi yake, ambayo imeanza mchakato wa kukata rufaa. “Tumeanza mchakato wa kukata rufaa na tunazingatia sheria na taratibu za Uingereza,” aliongeza.
Dk Kilangi alieleza kuwa hukumu hiyo imewashangaza kutokana na ukweli kuwa ndege yenyewe ilitumika kwa miezi saba tu. “Hawa watu wameibia nchi na tutapambana mahakamani kuhakikisha tunashinda kesi hii,” alisisitiza Kilangi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Leonard Chamuriho na Ofisa Mkuu Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi wote hawakutaka kuzungumzia suala hilo walipotafutwa kwa njia ya simu.
Kampuni ya Willis Trading iliwasilisha madai yake kwenye Mahakama ya Uingereza inayojishughulisha na masuala ya biashara na majengo kwa kudai kuwa walikuwa wamevunja makubaliano baina yao.
Kampuni hiyo inadai kulikuwepo makubuliano walipwe fidia ya Dola 45 milioni (Sh103 bilioni) mwaka 2014 lakini serikali ya Tanzania haikutelekeza makubaliano hayo.
Mattaka alifikishwa mahakamani Machi 2016 akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kutokana na kufikia makubaliano hayo ya ukodishaji ndege bila ya kufuata taratibu za serikali za ununuzi na kesi bado iko mahakamani.
Mahakama ya Uingereza imekataa utetezi wa ATCL, ambapo wanamsukumia lawama Mattaka.
Jaji Butcher amedai kuwa ATCL inapaswa kutekeleza makubaliano ya mwaka 2013 na kulipa Dola 30.1 milioni kwa Wallis Trading.