Serikali kukata rufaa hukumu ya kuzuia Wakurugenzi wa Halmashauri na Jiji kusimamia uchaguzi

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali Mwanasheria mkuu akiambatana na Wakili mkuu wa Serikali watazungumza na wanahabari kuhusu sheria za uchaguzi hivi punde.


UPDATES:
Serikalini imejipanga kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu kuhusu Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupinga vifungu vya Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu Wasimamizi wa Uchaguzi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, imeanza taratibu za Kisheria za kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani Tanzania ili sehemu ya uamuzi huo upitiwe upya

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi amesema kuwa, leo Mei 13, 2019 Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imewasilisha Mahakama ya Rufani Tanzania notisi ya kukata rufaa

Aidha, amebainisha kuwa "Kutokana na Serikali kutoa notisi ya kukata rufaa, hukumu ya Mahakama kuu haiwezi kutekelezwa mpaka Mahakama ya Rufaa itoe uamuzi wa rufaa, hivyo kama kuna changuzi zozote zitaendelea kama kawaida"

Mei 10, 2019 Mahakama Kuu Kanda ya Dar ilibatilisha vifungu vya sheria vinavyowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri na Jiji kusimamia Uchaguzi katika kesi iliyofunguliwa na Bob Wangwe akiwakilishwa na Wakili wake Fatma Karume

9576B634-8D39-40A7-82DC-CC9085509060.jpeg

B70D2537-039C-466C-818A-45D59574782D.jpeg

0DF16043-A5F6-4DEB-AF74-247E81A5035B.jpeg

1960E5B9-903C-4858-AE83-A7BDEBB3AC37.jpeg
 
Back
Top Bottom