Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Licha ya kuwepo kwa mgogoro wa umiliki wa ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi, serikali imesema uhusiano wa nchi hizo kwa sasa ni mzuri kuliko wakati wowote na kwamba hatua ya kukamilika kwa ujenzi wa meli mbili za mizigo ambazo zimejengwa na serikali ya Tanzania katika bandari ya Itungi mkoani Mbeya itaongeza uhusiano wa kibiashara miongoni mwa nchi hizo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameyasema hayo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya wakati ilipotembelea bandari ya Itungi wilayani Kyela kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi wa meli tatu zinazojengwa na serikali katika ziwa Nyasa.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema Tanzania na Malawi zinategemeana kwa mambo mengi na kwamba mwezi uliopita nchi hizo zimetiliana saini mkataba wa kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara na mafunzo kwa watumishi wa umma.
Kwa upande wake meneja wa bandari ya Itungi, Ajuaye Heri Msese, amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa meli mbili za mizigo bandarini hapo, sasa mamlaka ya bandari inaiomba serikali kuangalia uwezekano wa kujenga kipande cha reli kuanzia eneo la Uyole mahali ilipo reli ya TAZARA jijini Mbeya mpaka katika bandari ya Itungi kwa lengo la kuiunganisha kwa reli bandari hiyo na bandari ya Dar es Salaam.
Chanzo: ITV