Serikali kuja na Vitambulisho vipya kwa Machinga vitakavyodumu zaidi ya mwaka

Vije tu Tena waboreshe ikiwezekana kabla hakijapitwa na uda wawe wameshaandaa vingiii tabia naenda na pesa yng alafu wanajibu kuwa eti vimeisha sipendi, maana hawa wakata leseni za biashara niwapigaji balaa kwanza wanakuja wanapo jiskia wenyewe wakikukatia Leo wanjisahaulisha mpakamuda unapita wakikurudia sasa ndy utaomba po! Wanachukua kamtaji kote na ukilipa sasa unapewa stakabadhi ya mjimwengine shez nitaenda kulipa mwenyewe vikija kero za kufingiana biashara sizitaki tena
 
Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali ipo katika mchakato wa kutoa vitambulisho vipya vya wafanyabiashara wadogo.

Mtendaji mkuu huyo wa shughuli za Serikali ameagiza machinga kutosumbuliwa katika biashara zao huku akiwataka wajasiriamali hao kutotumika na wafanyabiashara wakubwa kuuza bidhaa mitaani kwa kuwa kitendo hicho huchangia kukwepa kulipa kodi.

Majaliwa ameeleza hayo leo Alhamisi Januari 28, 2021 katika ufunguzi wa kongamano la mashauriano na machinga jijini Dar es Salaam.

Amesema vitambulisho vinavyoandaliwa vitakuwa na taarifa za ziada ikilinganishwa na vya awali vilivyokuwa vinatolewa kwa Sh20,000 na kwamba vitadumu zaidi ya mwaka mmoja.

“Mwaka jana Serikali ilianza kutoa vitambulisho na itaendelea kuvitoa ili kuwezesha kufanya biashara zao bila usumbufu. Serikali inaandaa vitambulisho bora zaidi vitakavyomtambulisha machinga mwenyewe na kutambulika katika mifumo mingine, itaondoa utaratibu wa vitambulisho vya sasa.”

“Kama tumeweza kufanikisha ubora wa vitambulisho vya Taifa, leseni tutashindwa nini vitambulisho vya machinga? Watalaamu watajadiliana na kutueleza na vitakuwa na ukomo zaidi ya mwaka mmoja,” amesema.

Katika ufafanuzi wake, Majaliwa amesema Machinga ni kundi muhimu linalorahisisha upatikanaji wa bidhaa nchini, kuchochea kujiajiri, kuchochea ukuaji wa pato la Taifa na kupunguza umaskini nchini.

Kongamano hilo la machinga kutoka mikoa 26 nchini limehusisha mfuko wa NSSF, huduma za bima ya afya na taasisi za kifedha zilizoeleza mazingira ya upatikanaji wa mikopo kwa urahisi zaidi kupitia vikundi badala ya mkopo binafsi.
TAL in action. Hopefully every single sale will be receipted. The Marching guys are paying taxes in advance. Huu ndiyo uzalendo halisi.
 
Back
Top Bottom