Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,874
Nimeangalia video ya Mh. Rais @samia_suluhu_hassan akizungumza kuhusu serikali kuingia mkataba na kampuni ya Kituruki (Yutek Gemi San Ltd ) ya ujenzi wa meli 5 ,takribani Tsh. Bil.400 .
Rais Samia anasema mkataba huo uliingiwa tar 15 Juni 2021 huko Mwanza kati ya Serikali kupitia kampuni ya huduma za Meli Tanzania (MSCL) na kampuni hiyo ya Kituruki itwayo YUTEK GEMI SAN LTD.
Katika kufuatilia utekelezaji wa ujenzi wa meli hizo baada ya kuunda timu ya ufuatiliaji ,Rais Samia anasema mambo kadhaa waliyabaini yenye kutia wasiwasi.
1.Timu iligundua Mkandarasi huyo wa kampuni ya Yutek haina eneo lake la ujenzi wa meli yaani Ship-yard isipokuwa ni madalali tuu.
2.Timu iligundua uwezo wa kifedha wa kampuni hiyo ya Yutek ni mdogo mno na Timu hadi inaondoka haijapewa taarifa zozote za kifedha.Na hadi kampuni hiyo haijafanya chochote kuhusu ujenzi.
Ukimuangalia Mh. Rais Samia anavyoongea , sura yake ,matamshi yake huonesha kwamba ana mzigo mzito sana ameubeba.
Lakini mimi najiuliza wataalamu wanaolipwa na kodi zetu , kumsaidia Rais wanamsaidia namna gani ?
Alichoongea Rais Samia , kuhusu nchi kuingia mkataba na huyo Mkandarasi wa Uturuki, unapata kujua bado Rais anajukumu la kutengeneza mifumo imara na kuwa na watu imara wa kumsaidia kazi.
Inafahamika wazi kabla ya kuingia mkataba wowote uwe mkataba binafsi au mkataba wa nchi ,uwe mkataba mdogo au mkubwa na kampuni katika masuala ya kibiashara kuna kitu kinaitwa "Due Diligence" ikiwa na maana ya kupitia na kukagua ( Complete review and Audit) hali ya kampuni unayoingia nayo makubaliano au mkataba huo kabla ya kuingia mkataba wenyewe ili kujua uwezo wa kifedha wa kampuni hiyo (Financial Due Diligence),uhalali wa kampuni hiyo kisheria (Legal due Diligence),uwezo wake katika kufanya kazi (Operational Due Diligence) na mambo mengine, hii ni hatua ya awali kabisa kabla ya kuingia mkataba.
Kwa kauli ya Rais Samia inaonekana Due Diligence haikufanyika kabla ya kuingia mkataba huo,kama wangefanya Due Diligence awali wangebaini changamoto hizo mwanzo kabisa,wangefahamu mapema kama kampuni hiyo haina eneo lake la ujenzi kupitia kufanya Operational Due Diligence, wangefahamu uwezo mdogo wa kifedha wa hiyo kampuni mapema mno kupitia kufanya Financial Due Diligence.
Makosa haya yamekuwa yakijitokeza mara nyingi sana nchini kwetu ,itakumbukwa tar 30 , Januari 2019.Serikali iliingia mkataba huko Arusha na kampuni ya Indo Power Solutions Ltd ya nchini kenya chini ya Mkurugenzi wake Brian Mutembei ili kununua korosho tani laki moja zenye thamani ya Tsh.Bil.418 .Ila mwezi wa 5 ,2019 serikali ikavunja mkataba na kampuni hiyo baada ya kugundulika kampuni hiyo ni ya kijanja kijanja na ni madalali .
Changamoto hizi zenye maslahi ya nchi kiuchumi zinahitaji dawa.
Sitaki kulaumu sana bali nijikite katika ushauri kwa Mh. Rais na serikali ili haya mambo yasitokee tena .Ana nafasi ya kubalisha haya.
1.Tufanye marekebisho ya sheria yetu ya usalama wa taifa tuweke kitengo kitakachojikita na masuala ya ujasusi wa kiuchumi (Economic Intelligence),ndio itakuwa na kazi ya kukusanya taarifa za kiuchumi na makubaliano ya kibiashara kwa maslahi ya nchi kuliko Rais kuanza kuunda Tume ya kuchunguza na kufuatilia baada ya mambo kuharibika.
Marekani walifanya hivyo 1949 walirekebisha sheria yao ya ujasusi ya 1947 na kuweka kitengo cha "Office of economic Research Report".Bado hatujachelewa Mh. Rais , unaweza fanya hivyo .
Nchi nyingi sana sasa hivi zina vitengo hivyo ,nchi nyingi sasa duniani zimeingia katika ushindani na kulinda maslahi yao kiuchumi na kibiashara kwa maslahi ya nchi zao na mataifa yao ,hata sisi Tanzania bado hatujachelewa kufanya hivyo.Katika Thesis ya Valentyn Levytaskyi itwayo "Economic Intelligence of the Modern State ya 2001 " ameelezea vizuri sana kuhusu umuhimu wa nchi kuwa na kitengo cha ujasusi wa kiuchumi.
2.Mikataba yetu iwe wazi , kama ambavyo sheria ya Access information Act 2016, kifungu cha 5 ,na Access information Regulation 2017 kanuni ya 5 inavyoelezea kuhusu mikataba kuwekwa wazi kwa umma.Jambo hili halifanyiki nchini.
3.Itungwe sheria ya Bunge inayoipa Mamlaka Bunge ya kupitia na kupitisha mikataba yote yenye maslahi na nchi yenye kuanzia kiasi fulani cha fedha labda mikataba kuanzia bil. 10 lazima iende Bungeni kupitiwa na kupitishwa.
Ukisoma katiba yetu ya 1977 ibara ya 63(3)E , kuhusu wajibu wabunge katika kujadili na kuridhia makubaliano na mikataba , ibara hii haijajitosheleza kwani ina tafsiriwa tofauti kwamba ni mikataba inayoingia kati ya nchi yetu na nchi nyingine au jumuiya za kimataifa (Bilateral Agreement and Multilateral Agreement) na haitafsiriwi kama pia ni mikataba hii inayoingiwa kati ya taasisi ya Serikali au idara ya Serikali na taasisi nyingi au kampuni au nchi. Hivyo jukumu la kuwa na katiba yenye kutoa tafsiri nzuri katika ibara hii haliepukiki.
Nchini Tanzania ni mikataba ya rasilimali za nchi tuu kama madini na gesi ndio huweza jadiliwa na kupitishwa na Bunge kupitia sheria ya Natural wealth and resource (Permanent Sovereignty) Act ya 2017 na Natural wealth and resource (Review and re-negotiation of unconscionable terms act ya 2017 ).Bado pia sheria hizi zina mapungufu kadhaa .
Hivyo tunapaswa kuwa na sheria itakayoipa mamlaka Bunge , kupitia na kuidhinisha mikataba yote kabla ya Serikali kuingia mikataba hiyo .
4. Tuwe na mifumo imara itakayosaidia nchi kuwa na viongozi imara , pamoja na Bunge imara litakalo kuwa na uwezo wa kujadili ,kukosoa na kuishauri serikali .Na sio kuwa na Bunge la chama kimoja ambalo halina uwezo wa kukosoa na kuishauri serikali. Yote haya yanaweza fanyika kikamilifu kwa kuwa na mifumo imara kupitia mabadiliko ya katiba .
Hivyo katiba mpya ,ni jambo la msingi sana ili kutatua changamoto hizi.
Ahsante.
Abdul Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana ACT wazalendo Taifa.
05/12/2021.
Kigoma.