Serikali kuhamia Dodoma

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,924
3,904
Dodoma. Rais John Magufuli ameamua kukamilisha safari iliyoanza miaka 42 iliyopita ya kuhamishia makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma kwa kuanza kukarabati Uwanja wa Ndege na kuhamishia sherehe za mashujaa mjini hapa.

Wakosoaji wamekuwa wakieleza kuwa Serikali haina nia ya dhati ya kuhamisha makao yake kutoka Dar es Salaam kutokana na kuendelea kujenga ofisi zake kwenye mji huo maarufu wa kibiashara, huku Dodoma ikiendelea kuwa na ofisi ndogo za wizara.

Wadau wanasema kusita huko kuhamia Dodoma kumekuwa kukisababisha Serikali kuendeshwa kwa gharama kubwa kutokana na shughuli zake kurudufiwa.

Lakini Serikali ya Awamu ya Tano inaonekana kudhamiria kukamilisha safari ya kuhamia kwenye mji huo ulio katikati ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amesema kwenye mkutano wa kitaifa wa amani ulioandaliwa na Jumuiya ya Waislamu wa Ahamadiya mjini hapa kuwa hatua ya kupanua Uwanja wa Ndege wa Dodoma ni sehemu ya Serikali ya Magufuli kuhamia makao makuu.

Amesema Rais Magufuli atazindua awamu ya kwanza ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja huo utakaogharimu Sh11.8 bilioni wakati atakapokuja mjini hapa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika Julai 23.

“Hiyo ni miongoni mwa mipango inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuiwezesha kuhamia Dodoma,” amesema Rugimbana. “Rais ameamua kutumia baadhi ya fedha zilizobakia katika mwaka wa fedha uliopita kuufanyia ukarabati uwanja huu.”

Meneja mradi huo, Mhandisi Mbila Mdemu amesema ukarabati utahusisha njia za kuruka na kutua, barabara za viungio na maegesho ya ndege.

“Mwaka 2005 kulifanyika tathmini na usanifu kuona jinsi gani kiwanja hiki kitakavyoboreshwa na kuongezwa urefu wa barabara za kutua na kuruka kwa ndege,” amesema.

My take: Ni matamko mazuri lakini watoe deadline kwamba hadi ifikapo mwaka flani serikali itakua imehamisha ofisi zake zote Dodoma. Hizi za kuongea tu sidhani kama zinasaidia sana.
 
kama wameshindwa kuhamisha wizara zao.
serikali wajenge magorofa yanayoweza kuwa makazi ya watu kwa kuwakodisha au kuwauzia.

kama serikali imeweza kujenga magorofa ktk baadhi ya makambi ya jeshi kwa nini wasijenge makazi ya watu kwa mikoa kwa hawamu.
mfano kenya wameweza kujenga makazi kwa raia.
 
Maswali ni mengi na hayana majibu
 
Kwa hiyo Msalato International Airport bye bye, may be 2030....mipango kem kem....!
 
Huu 'wimbo' wa kuhamia kwa akina Mbukwenyi umeshapoteza mvuto masikioni mwetu.Tunachoona ni marekebisho ya 'mistari ya wimbo',mwimbaji na namna ya kuimba.
 
Huyu jamaa mpaka anamaliza miaka yake mitano atajikuta hana kitu cha maana mkononi alichokifanya, hivi ni nini kipaumbele? Elimu anatamani iwe bure, matumizi ya kawaida ya serikali anakomaa ayapunguze sana wakati huo huo anataka makusanyo ya kodi yaongezeke sana, kodi hizi anataka zitoke kwa wafanya biashara wakiwemo wa mahoteli ambao biashara zao kwa ujumla zina uhusiano mkubwa sana na matumizi ya kawaida ya Serikali, Mifumo ya kodi anataka iwe tight sana wakati huo huo anaitaka Tanzania ya Viwanda
 
kama wameshindwa kuhamisha wizara zao.

serikali wajenge magorofa yanayoweza kuwa makazi ya watu kwa kuwakodisha au kuwauzia.

kama serikali imeweza kujenga magorofa ktk baadhi ya makambi ya jeshi kwa nini wasijenge makazi ya watu kwa mikoa kwa hawamu.

mfano kenya wameweza kujenga makazi kwa raia.
Mhhh nimefika mpaka mwisho sijaelewa unaongelea nini, hapa kinachoongelewa ni azma ya serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake Dom, haya andika tena
 
Si ni yeye aliwapiga madongo wapinzani kwa kusema mbona wao wapinzani hawahamii Dodoma?
 
Mhhh nimefika mpaka mwisho sijaelewa unaongelea nini, hapa kinachoongelewa ni azma ya serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake Dom, haya andika tena

hilo jambo la kuhamisha serikali dodoma litatimia miongo kadhaa ijayo.
 
Kwa hiyo Msalato International Airport bye bye, may be 2030....mipango kem kem....!
Msalato wamepiga chini..Naskia kipindi Gadafi yupo aliahidi kujenga uwanja Dodoma na serikali ikaamua kutenga eneo msalato. Sasa Gadafi wakivyomuua serikali ikaona the best way ni kuendeleza huu uliopo.
 
Back
Top Bottom