Serikali kuhamia Dodoma: Wizara ya Katiba na Sheria tayari, Wizara ya Kilimo February 14

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Wizara ya Katiba na Sheria rasmi Dodoma, Kilimo Feb 14
=============================================

WAKATI Wizara ya Katiba na Sheria ikiingia rasmi katika ofisi zake mpya mjini Dodoma jana baada ya kuhamia mwishoni mwa wiki, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nayo imetangaza kuhamia mjini humo wiki mbili zijazo, huku ikiwatoa hofu watumishi wanaohamia huko kwa kuwataka kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mathew Mtigumwe jana aliwaondoa hofu watumishi wa wizara yake kuwa suala la kuhamia Dodoma kuwa litafuata misingi na stahili za watumishi kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.

Alitoa kauli hiyo wakati wa kikao maalumu kilicholenga kujadili kwa pamoja namna ya utendaji kazi katika wizara hiyo sambamba na kutoa utaratibu utakavyokuwa kuelekea kuhamia makao makuu ya nchi, Dodoma.

Alisema awamu ya kwanza ya uhamisho utahusisha watumishi 88 kutoka Idara Kuu ya Mazao, watumishi 41 watahamia Dodoma kuanzia Februari 14 na 15, mwaka huu huku wengine 47 watahamia muda wowote kati ya mwezi huu na Juni mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amezindua rasmi ofisi za wizara Dodoma na kuwataka watumishi waliohamia kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Makao Makuu ya wizara hiyo yaliyozinduliwa yapo katika Chuo Kikuu cha Dodoma na tayari watumishi wa wizara hiyo 31 wamehamia rasmi wakiongozwa na Dk Mwakyembe, Katibu Mkuu Profesa Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju.

Awamu ya pili ya tatu zinatarajiwa kufuata utaratibu uliowekwa na kufikia mapema mwakani, watumisho wote wa wizara hiyo watakuwa wamehamia Dodoma.

Baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa mwelekeo wa kuhamia makao makuu ya nchi kwa makatibu wakuu, manaibu wao pamoja na mawaziri na manaibu wao ifikapo Februari 28, mwaka huu, tayari wizara kadhaa zimehamia ikiwemo ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyohamia wiki iliyopita.

Chanzo: Muungwana
 
Nendeni mtuachie dar yetu. Kama una miaka 55 si mstaafu kwa hiari. Mnang'ang'ania kazi serikalini utafikiri mtafiamo. Ona sasa wazee wazima mnavyohama kama ndege pori!!!!
 
Nendeni mtuachie dar yetu. Kama una miaka 55 si mstaafu kwa hiari. Mnang'ang'ania kazi serikalini utafikiri mtafiamo. Ona sasa wazee wazima mnavyohama kama ndege pori!!!!

Na Wewe si Ujiajiri Kama alivyoshauri Kigwangala?
 
This Time mnaondoka Watumishi wa Umma!

Maombi ya kuhamia Manispaa za Jiji la Dar Es salaam Yamezidi kutoka Wizara mbalimbali ilimradi tu wasihame.

Mfupa uliomshinda Jks wote wawili, Mwiny na Mkapa umetafunwa na JPM
 
Nendeni mtuachie dar yetu. Kama una miaka 55 si mstaafu kwa hiari. Mnang'ang'ania kazi serikalini utafikiri mtafiamo. Ona sasa wazee wazima mnavyohama kama ndege pori!!!!
Taratibu mkuu....sina hata miaka minne toka nimeanza kazi so kuwa mvumilivu kidogo
 
This Time mnaondoka Watumishi wa Umma!

Maombi ya kuhamia Manispaa za Jiji la Dar Es salaam Yamezidi kutoka Wizara mbalimbali ilimradi tu wasihame.

Mfupa uliomshinda Jks wote wawili, Mwiny na Mkapa umetafunwa na JPM
hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe
 
usisahau ngata ya kubebea ndoo za maji maana kule kupata Petrol ni rahisi kuliko Maji

Unaongelea Dodoma ya mwaka gani mkuu? Hebu acha uongo, tatizo la maji Dodoma no kwamba maji yana chumvi lakini upatikanaji WA maji ni wa uhakika kwa asilimia zote
 
Unaongelea Dodoma ya mwaka gani mkuu? Hebu acha uongo, tatizo la maji Dodoma no kwamba maji yana chumvi lakini upatikanaji WA maji ni wa uhakika kwa asilimia zote

Dar Es salaam yenyewe haina uhakika wa Maji kwa asilimia zote ije kuwa huko Jangwani 'eti upatikanaji wa Maji ni wa uhakika asilimia zote', kwanza unajua jinsi ya ku calculate asilimia?

Hapa Tunazungumzia Mafuriko ya Watu zaid ya Million moja kwa Mara moja tokea Jijini Dar Es salaam Wewe unazungumzia Maji ya kuhudumia Wagogo elf 30!

Kama Makazi tu ya kutosha Wahamia Dodoma hakuna ije kuwa Maji?
 
Dar Es salaam yenyewe haina uhakika wa Maji kwa asilimia zote ije kuwa huko Jangwani 'eti upatikanaji wa Maji ni wa asilimia zote'.

Hapa Tunazungumzia Mafuriko ya Watu zaid ya Million moja kwa Mara moja tokea Jijini Dar Es salaam Wewe unazungumzia Maji ya kuhudumia Watoto elf 30!

Kama Makazi tu ya kutosha Wahamia Dodoma hakuna ije kuwa Maji?
Hata wakiwa milioni 2 still hakutakuwa na tatizo la maji, maji ya Dodoma ni ya underground sio ya mabwawa yanayoathirika kirahisi na misimu ya mwaka.

Dar es salaam kila kitu kibovu kipo hapa kuanzia uchafu etc. Hivyo comparison yako ya uhaba wa maji Dar kufananisha na mikoa mingine haupo valid kabisa.
 
Kwani huko kwny Shida ya Maji Hawana Ardhi wanaishi angani kiasi cha kushindwa kuchimba? Unadhani upatikanaji wa Maji ni rahisi rahisi Kama kuomba omba kwny Foleni za Magari?
Hata kisima kina kiwango cha mwisho kulingana na wingi wa mahitaji
 
Back
Top Bottom