Serikali kuhamia Dodoma .... kwanini serikali haitaki kukiri kwamba imeshindwa??

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Ikulu ya Chamwino kuhamishwa

Martha Mtangoo, Dodoma


IKULU ndogo ya Chamwino mkoani hapa pamoja na Ofisi ya Rais, vinatarajiwa kuhamishwa kutokana na eneo lililojengwa Ikulu hiyo kutotosheleza mahitaji tofauti na ilivyokuwa awali.

Kuhama kwa Ikulu ya Chamwino kunasababishwa na mazingira ya sasa ya kiutendaji kushindwa kutosheleza mahitaji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu, Sera na Bunge), Philip Marmo aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa jana kuwa awali Ikulu hiyo ilikuwa inatosheleza kupokea wakuu wa nchi tano tu na viongozi kadhaa kwa mara moja lakini mabadiliko ya kiuendeshaji kwa sasa hali hiyo haiwezekani.

Marmo alisema kunaongezeko kubwa la mahitaji ya kiutendaji ambayo yanafanya Ikulu hiyo ya Chamwino ya sasa kutotosheleza mahitaji.

“Ikulu pamoja na Ofisi ya Rais italazimika kuhamia mahali pengine upande wa kuelekea barabara ya Dar es Salaam kwa kuwa Ikulu ya Chamwino haikidhi mahitaji na hamtakiwi kushangaa kabisa,” alisema.

Waziri huyo alisema wiki ya kwanza ya Novemba, Bodi ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu, (CDA), itakaa kujadili mambo mbalimbali, ikiwamo kuandaa waraka kwa Baraza la Mawaziri kukubali kupendekeza eneo lingine ambalo litajengwa Ikulu hiyo.

Alisema mabadiliko hayo yanasababishwa na mpango kabambe wa kuangalia upya dhamira ya serikali ya kuhamishia Makao Makuu Dodoma ambapo alisema Dodoma haitoshi na iwapo pangekuwa panatosheleza Rais angehamia Ikulu ya Chamwino.

Alisema awali Bodi hiyo ilikaa na kupendekeza azma ya mwaka 1974 ya Dodoma kutojengwa jengo lenye ghorofa zaidi ya nne kufutwa kwa kuwa dhana hiyo imepitwa na wakati licha ya kuwa Dodoma ni ukanda ambao tetemeko la ardhi hupita mara kwa mara.

Kuhusu nia ya serikali kuhamia Dodoma, Marmo alisema kwa sasa hakuna uwezekano wa hata kuongeza wizara moja kuhamia Dodoma kutokana na ongezeko la idadi ya watu lililopo na kuongeza kuwa ongezeko hilo limesababishwa na kuanzishwa kwa vyuo vikuu.

Source: HabariLeo

Maswali:

Kuna haja gani ya kufanya tathimini wakati majibu tayari wanayo kwamba Dodoma haiwezi kutosheleza mahitaji ya serikali kuhamia huko.

Kama tayari wanasema kwamba Dodoma haitoshi, kwanini waendelee kupoteza hela kwa kuhamisha Ikulu kutoka Chamwino?

By the way, kwanini Chamwino ilijengwa kwa kiwango cha Ikulu ndogo na huku walikuwa wakijua kwamba makao makuu ya serikali yangehamia Dodoma na hivyo Chamwino ilitakiwa iwe na hadhi ya Ikulu kamili na siyo Ikulu ndogo.

Ninakiona hapa ni justification ya kutohamia Dodoma, na wameishaipata na sasa jibu litabadilika. Badala ya kusema watahamia nusu nusu sasa hawahami kabisa. Sioni hata sababu ya kuhamisha Ikulu ndogo ya Chamwino, maana itakuwa na hadhi sawa na zile Ikulu nyingine zote za mikoani ambazo zina hadhi ya Ikulu ndogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom