Serikali kufufua mgodi wa Buzwagi uliofungwa na Acacia kwa madai ya Madini kuisha Ardhini

Huko Tulawaka pamoja na kuachiwa karibia kila kitu na beberu, he STAMIGOLD, wametengeneza faida kiasi gani??

Wangeruhusu tu wachimbaji wadogo wahangaike huko, serikali ikusanye mapato.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
..acha uongo.

..barrick ndio walioanzisha acacia na waliokuwa na hisa nyingi zaidi.

..vigogo wa ccm ndio waliowaleta barrick na acacia nchini na kuwafungulia milango wajichotee madini.

..walioruhusu barrick watulipe kishika uchumba cha usd 300 million, badala ya deni la usd 191 billion, ndio wezi wakubwa na vibaraka wa mabeberu.
Na ndio hizo hizo zinawapa ruzuku. Kuweni na shukrani basi? Bila CCM kuwepo sijui nyie wengine mngekuwa wapi?
 


Kifupi:

Mgodi ukifika CUT OFF GRADE ni kufunga tu.

Sasa kama huu ulifungwa kwa kufika cut off grade sijui serikali wana mbinu gan ya kuuendesha kwa faida.

Vinginevyo labda haukufika huko

------
Cut-Off grade is the minimum grade required in order for a mineral or metal to be economically mined (or processed)

Moja kati ya parameters zinazotumika kutambua cut-off grade ya mgodi ni gharama za method inayotumika.. Cut-off grade inatofautiana kulingana na utofauti wa method inayotumika.

Binafsi bado sioni sababu ya kupinga kama muwekezaji amehakikisha anayo mbinu itakayomfanya apate faida. Cha msingi sheria zote zifuatwe.
 
Na ndio hizo hizo zinawapa ruzuku. Kuweni na shukrani basi? Bila CCM kuwepo sijui nyie wengine mngekuwa wapi?
Acha kutudanganya,vipi sehemu nyingine za dunia ambapo hamna huyo mnyama wa kijani,Maisha si bora zaidi.
 
Acha kutudanganya,vipi sehemu nyingine za dunia ambapo hamna huyo mnyama wa kijani,Maisha si bora zaidi.
Majungu hayo, hama nchi kwani lazima uishi Tanzania? UK wana vyama viwili tu vikubwa na wanabadilishana USA vile vile wana vyama vikubwa viwili tu na ndio vinabadilishana. Mlizoea enzi zenu chuma kiko Ikulu sasa wacha kiwasafishe. Una haki ya kuhamia Bengal!
 
Majungu hayo, hama nchi kwani lazima uishi Tanzania? UK wana vyama viwili tu vikubwa na wanabadilishana USA vile vile wana vyama vikubwa viwili tu na ndio vinabadilishana. Mlizoea enzi zenu chuma kiko Ikulu sasa wacha kiwasafishe. Una haki ya kuhamia Bengal!
Unatuumiza macho na marangi yako ya kusisitiza unayo amini wewe.
 
Moja kati ya parameters zinazotumika kutambua cut-off grade ya mgodi ni gharama za method inayotumika.. Cut-off grade inatofautiana kulingana na utofauti wa method inayotumika.

Binafsi bado sioni sababu ya kupinga kama muwekezaji amehakikisha anayo mbinu itakayomfanya apate faida. Cha msingi sheria zote zifuatwe.

Nakubaliana na wewe kwenye hilo suala la cut grade na njia ya uchimbaji na processing. (Upo sahihi kabisa)

Pia mimi sijapinga muwekezaji kuendeleza uchimbaji.

Wasi wasi wangu tu ni njia ambayo itatumika na kuzalisha faida. Hapa ndio nina mashaka.
 
PAMOJA na mmiliki wa sasa wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, kampuni ya Acacia Mining, kutangaza kutaka kufunga mgodi wake, serikali ya Tanzania imesema, mgodi huo, uatendelea kufanya kazi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Acacia iliamua kuufunga mgodi wake wa Buzwagi, uliyopo wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, baada ya kujiridhisha kuwa utajiri wa madini uliyopo katika eneo hilo, umemalizika.

Taarifa ya mgodi huo kuendelea kutumika, imetolewa leo Jumanne, tarehe 19 Januari 2021 na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Prof. Palamagamba Kabudi, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya Madini ya LZ Nickel Limited.

Akizungumza katika halfa hiyo, mbele ya rais John Magufuli, Prof. Kabudi alisema, “faida kubwa ya mradi huu, ni kuanza matumizi mbadala ya miundombinu iliyokuwa inatumika kwenye uendeshwaji wa mgodi wa Buzwagi, ambao unatarajiwa kufungwa hivi karibuni.”

Alisema, muwekezaji huyo mpya, ameomba kwa serikali kuruhusu kutumika kwa miundombinu ya mgodi wa Buzwagi, pindi mgodi huo utakapofungwa.

Aidha, kampuni hiyo imeomba kibali cha kuchenjua masalia ya madini yaliyoko katika mgodi wa Buzwagi, kwa maelezo kuwa teknolojia yake ya kuchenjua masalia hayo kuwa madini, yaweza kufanya kazi hiyo.

Alisema, “…mheshimiwa rais, wawekezaji hawa wameomba mgodi huu utakapofungwa wauchukue ili badala ya kufungwa ufanye kazi nyingine, ili kuuongezea uhai zaidi sababu wanasema yale masalia yaliyoko pale Buzwagi bado yana madini.”

Ameongeza, “…na kwa teknolojia hii mpya, bado watavuna madini haya ambayo sasa ni rundo. Teknolojia ya wale ilikuwa haiwezi kuyachenjua. Hawa wanaweza; sasa masalia yote ya Buzwagi yatarudishwa tena kwenye mitambo na kutoa madini.”

Prof. Kabudi alitoa taarifa hiyo wakati anataja faida za mkataba huo wa uchimbaji madini ya Nickel katika mgodi wa Kabanga mkoani Kagera na ujenzi wa Kiwanda uchakataji madini mkoani Shinyanga.

Ametaja faida nyingine za mradi huo, ni kuongezeka kwa ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya madini.

“Mradi huu utaongeza ukuaji wa sekta ya madini, kwa kuanzisha na kuendeleza uchimbaji wa madini ya Nickel na madini muambata kama kopa na kobati,” ameeleza
Hakuna muwekezaji anataka kufanya KAZI YA HASARA. Kama vile ambavyo biashara binafsi zinafungwa nyingi, migodi nayo inafungwa sababu hakuna faida. Sirikali angalieni kodi zenu na regulations zenu. Watz ndio wataumia mwisho wa siku.
 
Sio kweli Barrick walitafuta management company ya kuendesha mgodi tenda wakashinda kampuni ya acacia katika malipo na incentive walizopewa ni hisa kidogo kuwa pamoja na malipo watakayolipwa pia watapewa hisa ni kama Tanzania brewerias walipokuja walimpa managing director Arnold Kileo hisa kuwa pamoja na malipo ya ku manage wakampa hisa moja

Acacia walipishika management ya mgodi ndio wakaanza kuiibia Tanzania na main shareholders Barrick ndio maana serikali ilikataa katakata kujadiliana chochote na management Accacia ikataka kujadili na main shareholder Barrick aliyemwajiri Acacia

Akina Lisu Fatuma karume na Tundu Lisu wakawa wanaikingia kifua management company ya Acacia ndio kibaka Lisu akawa akitutishia kuwa Acacia itatupeleka MIGA!!! Yaani anatushia eti management itatupeleka MIGA

Dk Magufufuli akakomaa na main shareholders anawaambia Acacia siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa Barrick.Leo ndio haya matunda tunayaona Acacia vibaka walifunga mgodi wakitishia nyau kwa ushauri wa vibaka Lissu Fatuma karume na zitto kabwe leo mgodi huo unaendelea! Barrik oyeee Dk Magufuli hoyee Tundu Lisu ziiiii Fatuma Karume ziiiii Zito Kabwe ziiiiiii

..maelezo yako ni ya uongo.

..na hata yangekuwa ya ukweli hayaisafishi barrick kutokana na wizi wa madini hapa Tz.

..sisi tulisema tunadai usd 191 billion lakini bila maelezo ya kutosha tumekubali kishika uchumba cha usd 300 million.

..mimi nadhani kuna MAJIZI ndani ya ccm na serikali ndiyo yameingia makubaliano ya kifisadi ya kukubali kishika uchumba toka barrick.
 
Kichwa cha habari na taarifa haviendani, huyu muwekezaji haendi kuchimba madini bali anataka kuchenjua zile shehena za makinikia na udongo uliojazwa kule TSF na zile low grade ambazo Acacia wameziacha kuepuka gharama ya kuendesha uchenjuaji wa hasara kutokana na kiasi cha madini wanayotegemewa kuyapata kutoka kwenye mchanga huo.

Pia ikumbukwe kwamba Buzwagi madini hayajaisha, bali gharama zinazohitajika kuyachimba madini hayo ni kubwa sana hivyo kupelekea mgodi kujiendesha either kwa faida ndogo sana ama kwa hasara.

Inasemekana (hili sina uhakika nalo), kampuni iliyofanya utafiti wa madini pale Buzwagi nadhani ni Pangea minerals, waliwaingiza chaka ABG na kuwafanya watengeneze Mining map yao nje ya eneo lenye kiasi kikubwa cha madini, hali hii ilipelekea kubadili ramani yao ghafla sana kuelekea upande uliokua na kambi za kampuni ya ulipuaji, na hivyo kupelekea shimo kubana.
Inasemekana iliwalazimu kuanza uchimbaji upya ili wapanue shimo hilo, kitu ambacho walikitafsiri kama hasara kwao.
 
Porojo tu.

Kutumia mabanda yalioachwa kama madarasa, soko ama makazi ndiyo kufufua mgodi??

Rubbish!!!
Kampuni kama yapi markez ikimaliza mkataba wa ujenzi wakaacha kambi yao mikononi mwa serikali, na wananchi wa eneo hilo wakaamua kuitumia kufungua shule ya sekondari au chuo cha ufundi kuna ubaya gani?
Wakati mwingine makamanda sijui huwa mnatumia nini kufikiri?! Mnaiabisha sana chadema. Chadema iliyokuwa hazina ya hoja mbadala sasa hivi imegeuka kuwa genge la wasemaovyo tu. Bure kabisa 😢😢
 
Alafu mwisho wa siku inagundulika mmiliki wa huu mgodi ni kagame wakiwa na share na magufuli nyuma ya pazia.
 


Kifupi:

Mgodi ukifika CUT OFF GRADE ni kufunga tu.

Sasa kama huu ulifungwa kwa kufika cut off grade sijui serikali wana mbinu gan ya kuuendesha kwa faida.

Vinginevyo labda haukufika huko

------
Cut-Off grade is the minimum grade required in order for a mineral or metal to be economically mined (or processed)
Hoja ya Kabudi ni ya kipuuzi kabisa. Inawafaa wajinga wa sekta hii.

Wanachotaka kufanya hiyo kampuni nyingine ni sawa na ukawa na shamba la mahindi, unavuna kutumia combine harvester. Umemaliza, halafu anakuja mtu anaomba apite kwenye shamba lililovunwa kuangalia uwezekano wa kuvuna mahindi yale machache yaliyokuwa yameanguka kabla ya harvester kupita ili aokoteze na kujipatia riziki ndogo.

Hiyo teknolojia anayoiongela Kabudi imekuwepo kwa miaka mingi. Mineralization inafuata structure. Na kuna wakati kunakuwa na minor structural displays kama vile fractures na shear displays ambako mineralized fluids zilipenya wakati wa mineralization. Hizi hazifuatwi na makampuni makubwa ya uchimbaji. Vikampuni vidogo huweza kuyachukua mawe, kisha kufanya crushing ili kupata aggregates ambazo baadaye zinapita kwenye sorting systems ambapo zile zilizokuwa mineralized zinakuwa picked na kwenda kufanyiwa processing kwaajili ya kupata madini yanayotafutwa.

Kwa ujumla, unachokipata kupitia process hiyo ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na kile alichokipata mvunaji wa kwanza. Hiyo ndiyo sababu huwezi kuona kampuni kubwa zikijishughulisha na uvunaji dhahabu wa namna hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom