Serikali "Kufidia" makampuni 50 yaliyoathirika na "Mtikisiko wa Uchumi Duniani"!

Mimi nawaambia watu hapa kuwa Kikwete ana/ataiba pesa za wabongo kuliko viongozi wote waliomtangulia combined watu wanabisha. Wanaomtetea Kikwete hawasemi kizuri chochote alichofanya zaidi tu ya kuwa yeye ni mcha mungu na muungwana.

Akhhh kazi kweli kweli. Kikwete anaipeleka hii nchi kuzimu
 
Reverend,
Asante sana kwa kuanzisha huu mjadala. Niliposoma hiyo taarifa kwenye gazeti nilichanganyikiwa kana kwamba nimeishiwa akili au napata wazimu. Nakumbuka wakati wa mkutano wa IMF pale Dar mhishimiwa aliulizwa Tanzania inachukua hatua gani kukabiliana na huu mterereko wa uchumi duniani akajibu kuwa hakuna chochote ni mwendo mdundo tu. Sasa najiuliza kuna kampuni gani za Kitanzania ambazo biashara zake nje ya nchi zimekumbwa na huo mterereko, sikupata jibu. Halafu nikaangalia mfano wa Obama hapa Marekani. Yeye hakumwaga pesa ovyo tu. Alichofanya ni kuyakopesha makampuni yaliyoathirika ili yasifunge milango na baadhi yameshaanza kurudisha mikopo waliyopewa na serikali. Sasa sisi tunaigaiga tu vitu vya nje na kufanya maigizo yasiyo na mikono wala miguu. Na kama ni kuathirika mimi ningefikiri kuwa wazalishaji wa Kitanzania (kama wapo) ndio wangeathirika na hawa ndio serikali ingepaswa kuwakingia kifua cha stimulus package. Nasikia kwenye hiyo orodha ya makampuni yatakayopewa ahueni kuna kampuni za uchimbaji madini. Go figure.
 
1. JMK has never been original in anything at any time of his life ...He is still growing and I hope It wont too late!!

2. Nchi haina difined direction Idiologicaly, politically and economicaly in which to follow to any defined specific Goal...Ni Ku iga Iga tu na "kuichukuli jinsi itakavyokuja"

3. Habari ya "kufidia"...what is this..? Im very sure kwa kukosa definition ya kila kitu hapanchini kumepelekea Tz Kunakili kila kinachofanyika kwingine duniani kama njia ya kuwafurahisha na kujifanya kwenda na wakati au?... ?Hakuna mantikiyeyote kwenye maelezo yote yaliyotolewa hapa kuhusu mambo ya kufidia na ku stimulate!

4.Kwa kiasi nilichomsoma President. Alifikiri na kudhani Kama Rais wa awamu ya 4 atafanya miujiza ya kiuchumi Tz Kwa Kupitia sekta ya UTALII na MADINI. Kwa namna fulani ALILENGA KABISA kupuuzia kabisa KILIMO na UFUGAJI kwa madai ni uchumi wa Kizamani na vinamkumbusha Azimio La Arusha na mambo ya kujitegemea amabayo hataki kabisa kuyasikia na mdomo wake haujawihi kutamka neno KUJITEGEMEA tangu aingie madarakani.

4. LAKINI: Amekuwa suprised kwani Tangu litokee anguko la Uchumi duniani ndoto zake zikazimwa maramoja. Ghafla tunasikia KILIMO KWANZA .....etc Lo Hata yeye anajua kilimo?

5. Kwa Kifupi ni upuuzi Kusaliti Kilimo na ustwishaji wa ufagaji Tz katika kutafuta maendeleo ya wote. Nilifikiri amejifunza kiukweli and He is honest na hikli swala la KILIMO.

6. KILIMO KWANZA kingepewa hela zote hizo za hayo Makampuni. Na kufanya:

6.1 Kutengeneza Mifereji ... Mabwawa na ANY other effective irrigation systems in speciallised locations in the country.

6.2 Kwenye sehemu maalum amabazo umwagiliaji ungewekezwa MASSIVELY na wanachi wenyewe...Matrekta yangenunuliwa na nyenzo nyingine kuwezesha 6.1

6.3 Incentives za namna fulani zingetolewa kwa wakulima kufikia lengo la juu kabisa la uzalishaji.

7. Hata hivyo alichokuwa anakikimbia Kikwete na kuuita uchumi wa kizamani inamlazimu HATA KWA UNAFIKI kukirejea....hakuna Namna ya kumsaidia mwannchi wa kipato cha chini Tanzania Nje ya kupitia KILIMOCHA NA UFUGAJI WA KISASA. Hizo njia nyingne basically sio Basic. Na zina prove kuwa more prone to MAFISADI kuliko kuwawezesha wananchi na wafugaji wenyewe kwanza ndio hayo menguine yafuate.

8. Ni kilimo "CHA NGUVU" na sio Madini_utalii "WA NGUVU". Mapato ya Utalii Na Madinili na biashara nyingine zozote zinapitia kwnye mikono ya vyombo visivyo
mikononi mwa wakulima na wafugaji Na mpaka mzunguko huo wa mapato umfikie mukulima na amfugaji Wapuuzi wote, mafisasdi wote, wasaliti wote wa kisiasa watakuwa wamesha shiba na kupelea makombo..ndipo mkulima na mfugaji apate. Ndio maana kuuwekeza kwenye KILIMO hakupendwi na WASALITI WA UTU WA MTANZANIA.
 
Dear Interested Observer!

I agree with you hapa Tanzania SIYAONI hayo makampuni hamsini labda as you said serikali iyape stimulus mashirika yake ya umma kama Dawasco,Tanesco, ambayo yanaadhirika vibaya na kupanda kwa bei ya mafuta ili hali Ewura inawazuia kupandisha bei ya haduma wanayotoa kwani hawa jamaa hawafanyi biashara in the real sense. Kama Tanesco wananua umeme kutoka Songas kwa Tshs, 150/=( Ukiongezea na Capacity charge ni karibu Tshs.300/= kwa unit {KWhr) moja) na kuizia Zanzibar kwa Tshs. 50/= na bei ya wastani ya Tshs 120/= kwa wateja wengine hapo hakuna biashara bali ni usanii

Kama JMK aka matonya angetumia ABC ya uchumi aliyosoma pale mlimani zaidi ya miaka 30 iliyopita angeamua kutumia hiyo stimulus katika kustabilize bei ya mafuta pamoja na STABEX kwenye kilimo pamoja na pembejeo ahamasishe kilimo. Mabenki hayana historia ya kuimarisha uchumi!! Hayo makampuni ni ya wabunge na wanamtandao waliompeleka madarakani anataka tu kuwalipa fadhila. BENKI kuu iko Mochwari kama wamekubali kumteua fisadi Peter Noni wa RA akaongoze TIB unatarajia muujiza gani!! Look at those fools hata DECI hawakuigundua for 3 soild years Hamshangai tu kwamba the stupid Minister of Finance alifungua tawi la DECI kule kwao na bado JMK anazidi kumkumbatia asimpige paranja kwa sababu tu ya Udini!! hayo makampuni ambayo hayapeleki BOT audited accounts watayapata wapi?? Si bora mkawapa hata wanafunzi vitabu na walimu mishahara tujue moja??

The president and the govt he is leading is not serious na narudia lini Mkwere akawa serious apart from dancing. Kama kuna kampuni iliyoadhirika kikweli kweli si tungeona imefanya massive layouts na hilo bado halijatokea!!!

Mkereme, maelezo yako nimeyakuibali. Mahesabu yao hawa watunga sera si kustimulate uchumi, bali ni kustimulate kura za 2010 ziegemee upande wao. watapata wapi hela za kununulia kofia, khanga na shahada za wapiga kura?. Lazima akili ifanye kazi hapo. USA, ambao ni matajiri ambao kila siku Vasco anatembelea kuona kama watatusaidia nini, mpaka sasa wametumia only 8% ya stimulus money, kwani wanajua kuwa huwezi kutoa pesa za bure kwa makampuni kwa kisingizio cha kukuza uchumi, either makampuni yakopeshwe au serikali iyachukue na kuyaendesha kwa pesa za walipa kodi na wahisani (back to socialism)

There's nothing here like stimulus, its another EPA in making to 2010 election.
 
1. JMK has never been original in anything at any time of his life ...He is still growing and I hope It wont too late!!

2. Nchi haina difined direction Idiologicaly, politically and economicaly in which to follow to any defined specific Goal...Ni Ku iga Iga tu na "kuichukuli jinsi itakavyokuja"

3. Habari ya "kufidia"...what is this..? Im very sure kwa kukosa definition ya kila kitu hapanchini kumepelekea Tz Kunakili kila kinachofanyika kwingine duniani kama njia ya kuwafurahisha na kujifanya kwenda na wakati au?... ?Hakuna mantikiyeyote kwenye maelezo yote yaliyotolewa hapa kuhusu mambo ya kufidia na ku stimulate!

4.Kwa kiasi nilichomsoma President. Alifikiri na kudhani Kama Rais wa awamu ya 4 atafanya miujiza ya kiuchumi Tz Kwa Kupitia sekta ya UTALII na MADINI. Kwa namna fulani ALILENGA KABISA kupuuzia kabisa KILIMO na UFUGAJI kwa madai ni uchumi wa Kizamani na vinamkumbusha Azimio La Arusha na mambo ya kujitegemea amabayo hataki kabisa kuyasikia na mdomo wake haujawihi kutamka neno KUJITEGEMEA tangu aingie madarakani.

4. LAKINI: Amekuwa suprised kwani Tangu litokee anguko la Uchumi duniani ndoto zake zikazimwa maramoja. Ghafla tunasikia KILIMO KWANZA .....etc Lo Hata yeye anajua kilimo?

5. Kwa Kifupi ni upuuzi Kusaliti Kilimo na ustwishaji wa ufagaji Tz katika kutafuta maendeleo ya wote. Nilifikiri amejifunza kiukweli and He is honest na hikli swala la KILIMO.

6. KILIMO KWANZA kingepewa hela zote hizo za hayo Makampuni. Na kufanya:

6.1 Kutengeneza Mifereji ... Mabwawa na ANY other effective irrigation systems in speciallised locations in the country.

6.2 Kwenye sehemu maalum amabazo umwagiliaji ungewekezwa MASSIVELY na wanachi wenyewe...Matrekta yangenunuliwa na nyenzo nyingine kuwezesha 6.1

6.3 Incentives za namna fulani zingetolewa kwa wakulima kufikia lengo la juu kabisa la uzalishaji.

7. Hata hivyo alichokuwa anakikimbia Kikwete na kuuita uchumi wa kizamani inamlazimu HATA KWA UNAFIKI kukirejea....hakuna Namna ya kumsaidia mwannchi wa kipato cha chini Tanzania Nje ya kupitia KILIMOCHA NA UFUGAJI WA KISASA. Hizo njia nyingne basically sio Basic. Na zina prove kuwa more prone to MAFISADI kuliko kuwawezesha wananchi na wafugaji wenyewe kwanza ndio hayo menguine yafuate.

8. Ni kilimo "CHA NGUVU" na sio Madini_utalii "WA NGUVU". Mapato ya Utalii Na Madinili na biashara nyingine zozote zinapitia kwnye mikono ya vyombo visivyo
mikononi mwa wakulima na wafugaji Na mpaka mzunguko huo wa mapato umfikie mukulima na amfugaji Wapuuzi wote, mafisasdi wote, wasaliti wote wa kisiasa watakuwa wamesha shiba na kupelea makombo..ndipo mkulima na mfugaji apate. Ndio maana kuuwekeza kwenye KILIMO hakupendwi na WASALITI WA UTU WA MTANZANIA.

Azimio jipya,

Good points mkuu, heshima mbele pia.

Watu kama wewe serikali inawaogopa kwa hoja zenu zenye nguvu. No wonder Kikwete kamuweka Mkullo wizara ya fedha na uchumi ili mambo yote yaendeshe holela holela tu mradi liende na mkuu apate pesa za kusafiri nje ya nchi.

Kazi kweli kweli.
 
Dear Interested Observer!

I agree with you hapa Tanzania SIYAONI hayo makampuni hamsini labda as you said serikali iyape stimulus mashirika yake ya umma kama Dawasco,Tanesco, ambayo yanaadhirika vibaya na kupanda kwa bei ya mafuta ili hali Ewura inawazuia kupandisha bei ya haduma wanayotoa kwani hawa jamaa hawafanyi biashara in the real sense. Kama Tanesco wananua umeme kutoka Songas kwa Tshs, 150/=( Ukiongezea na Capacity charge ni karibu Tshs.300/= kwa unit {KWhr) moja) na kuizia Zanzibar kwa Tshs. 50/= na bei ya wastani ya Tshs 120/= kwa wateja wengine hapo hakuna biashara bali ni usanii

Kama JMK aka matonya angetumia ABC ya uchumi aliyosoma pale mlimani zaidi ya miaka 30 iliyopita angeamua kutumia hiyo stimulus katika kustabilize bei ya mafuta pamoja na STABEX kwenye kilimo pamoja na pembejeo ahamasishe kilimo. Mabenki hayana historia ya kuimarisha uchumi!! Hayo makampuni ni ya wabunge na wanamtandao waliompeleka madarakani anataka tu kuwalipa fadhila. BENKI kuu iko Mochwari kama wamekubali kumteua fisadi Peter Noni wa RA akaongoze TIB unatarajia muujiza gani!! Look at those fools hata DECI hawakuigundua for 3 soild years Hamshangai tu kwamba the stupid Minister of Finance alifungua tawi la DECI kule kwao na bado JMK anazidi kumkumbatia asimpige paranja kwa sababu tu ya Udini!! hayo makampuni ambayo hayapeleki BOT audited accounts watayapata wapi?? Si bora mkawapa hata wanafunzi vitabu na walimu mishahara tujue moja??

The president and the govt he is leading is not serious na narudia lini Mkwere akawa serious apart from dancing. Kama kuna kampuni iliyoadhirika kikweli kweli si tungeona imefanya massive layouts na hilo bado halijatokea!!!

Mkereme,

Wakati Uchumi wa Dunia ulipoanza kuanguka Mwezi September 2008, nayo bei ya mafuta ilianza kuporomoka. Hivyo hicho nacho kitakuwa kisingizio batili kwa kuwa Bei za mafuta kwa pipa duniani zilishuka marudufu karibu asilimia 60-70!
 
Jamani hizi ni profit making companies, sasa zinapopata faida huwa zinaipa serikali pesa za ziada kwa kufanya vizuri??? Jibu ni hapana!! Kwa hiyo pesa za serikali wanazopewa sio fidia bali inabidi ziwe mkopo, ili uko mbele wanapopata faida pesa za wananchi zirudishwe.

Bilioni 29, zinajenga shule za sekondari ngapi vijijini?? Hospitali vijijni nako ngapi zingejengwa??

Hapo naomba wabunge waje juu sababu kuna wananchi kibao wamepata hasara kutokana na mitikisiko ya uchumi kwa hiyo nao basi wapewe fidia kama serikali iko generous kiasi hicho?? Also wakulima wao waliwauzia mazao kwa bei ndogo nao vipi watapewa fidia??

Solution hapa ni kukopesha tu hayo makampuni tena yaonyeshe kuwa yako solvent na waweke collateral, hawataki NEXT!!!
 
Jamani eee; waambieni na mi wanipe hiyo tenda ya kuwasaidia kuchota pesa za uchaguzi (just making fun of them) !!!
 
Pesa hizo zitatolewa kama mikopo kwa makampuni husika. Makampuni hayo mengi yanamilikiwa na wahindi. Na baada ya kupata hiyo mikopo makampuni hayo yatakuwa dissolved (mufilisi). Ukweli ni kwamba lengo kubwa ni kupata pesa za uchaguzi.

Kwanini uwanunue na kuwahonga watu ili wakupigie kura?. Kama kweli wewe ni msafi na una nia safi ya kulitumikia Taifa kama kiongozi kwanini ununue kura?. Na sisi wananchi kwanini tununuliwe na kuhongwa ili tuwapigie kura wahuni hawa?. Kwanini tuuze haki zetu na za watoto wetu kwa hawa wahuni?.

Watanzania wenzangu, tutakapoweza kuwapata viongozi kwa njia halali (bila ya kutumia rushwa) tunaweza kutegemea maendeleo na haki katika nchi yetu. Lakini hawa viongozi wa kununua kura matokeo yake ndiyo haya tunayaona leo, nchi inayumba na kila mtu anafanya atakavyo ili mradi alisaidia katika ununuzi wa kura zilizompa ushindi kiongozi husika, si polisi wala mahakama inaweza kumtia hatiani mtu huyo.

Ningependekeza sisi wananchi tushinikize hili suala lisifanyike kabisa. Hakuna cha mikopo kutolewa wala misaada, kwani hapa wahuni hawa wanataka kutengeneza EPA kwa baraka zetu sisi wananchi. Kama kuna pesa huko serikalini basi zitumike katika kuwalipa waalimu malimbikizo ya mishahara yao, kuwapatia watoto wetu madawati, na kununua madawa yanayohitajika katika zahanati zetu na vitu vingine vya maendeleo kwa ajili ya jamii.

Ninamshukuru Mwakyembe kwa kauli yake aliyowahi kusema kwamba Watanzania si mabwege tena.
 
nasikia wakina RA,chenge na wenzao washaanza fungua kampuni hewa mpya ili wale bingo hizo..hahahaha amakweli wajinga ndo waliwao!!!
 
Mkereme,

Wakati Uchumi wa Dunia ulipoanza kuanguka Mwezi September 2008, nayo bei ya mafuta ilianza kuporomoka. Hivyo hicho nacho kitakuwa kisingizio batili kwa kuwa Bei za mafuta kwa pipa duniani zilishuka marudufu karibu asilimia 60-70!

Rev. Kishoka!

Tuko pamoja hoja hapa ni kwamba mafuta yalishuka bei kutoka USD 150 kwa pipa moja(Barrel) HADI kufikia USD 35 ni sawa na kugawanya bei kwa nne na ushei ambayo ni sawa na punguzo la asilimia 75% lakini hapa TZ bei ilipungua kutoka Tshs 1700/= kwa lita ya petroli na kufikia wastani wa 1200/= kwa lita ambalo ni punguzo la asilimia 30% na leo hii bei imerudi pale pale leo mafuta ya petrol Total wanauza 1500/= kwa lita with full blessing za hao wapuuzi Ewura wakati mafuta yamepanda na kufikia around Usd 60 kwa pipa kwenye soko la dunia what a shame!!! .

Kwa mahesabu kidogo tu ya ulinganisho utaona ni jinsi gani palipo na wizi kwa walalahoi from the gvt and the Oil mafia hawa Ewura ni machizi nini sijui Masebu anajua hesabu na hao wapambe wake au wanapewa rushwa na Oil Magnets wa Bongo!!

Over that period hapajakuwepo na ongezeko sawia la huduma ya Dawasco na Tanesco hata kama wanao ufisadi wao wa ndani bado they actually need a stimulus left or right!!! Endeleeni na nyie kujadili Kishoka uwanja uko wazi!!!
 
Wait a minute, kumbukumbu zangu zikinirudia sasa, nakumbuka kuwa Gavana wa BOT Benno Ndulu na Rais wa Jamhuri Tanzania Jakaya Kikwete, walitoa kauli mara kadhaa mwanzoni mwa mwaka kuwa Tanzania haijaathirika hata chembe na mtikisiko wa Uchumi wa Dunia.

Kisha wakati wa G20 pale London, Kikwete aliongoza msafara kwenda kuomba Stimulus package, then leo tunatoa stimulus package kwa makampuni.

Swali ni hivi, je wote Ndulu na Kikwete walikurupuka na kutoa majibu bila kufanya tathmini ya kweli walipodai kuwa hatujaathirika kama Taifa? Kama ndivyo, je ni halali kwangu kuwaita ni viongozi wasio makini?

Kama hawakukurupuka ghafla bin vup na kutoa hizo kauli, je bado inawezekana kuwa uwezo wao wa kupima mambo na kufanya tathmini ya yanayotokea kuwa ni mdogo na una mushkeli? Kama ndivyo, je kwa nini wanaendelea kuongoza Taifa?

Kama uongozi wao na utendaji kazi wao ni wa kubahatisha bahatisha sawa na ile ya Hamadi Kibindoni, je Taifa letu litakaa liweze kupata msukumo chanya wa maendeleo na hata kujengeka si kwa Siasa Safi tuu, bali kwa Uongozi Bora?
 
Mkuu Rev., usifedheheke sana na kuweka focus kwenye aina ya uongozi tulionao Kitaifa. Kuna makumi ya threads zinazoongelea competences za watawala wetu.

Kwenye hili swala mimi nadhani ni bora tuweke focus kwenye hizo kampuni. Kama ulivyodokezea kwenye mwanzo wa thread, maswali ya kujiuliza ni mengi kuhusiana na hizi kampuni.

--- Ni muhimu tujue hizi kampuni zina muda gani hapa Tanzania, zina ajiri wananchi wangapi, zinauza nini na soko lake liko wapi?

--- Mapato yake ni yapi? Annual report zake kwa miaka iliyopita zinasema nini?

--- Projection zao ni zipi kabla na baada ya mtikisiko wa uchumi?
--- Zilijiandaa vipi baada ya habari za mtikisiko kuanza kusikika kote duniani?
--- Malipo kwa wanahisa wake ni yepi kabla na baada ya habari ya mtikisiko?

Mimi najiuliza, kwanini serikali isipunguze kodi, mfano kwenye vyombo vya usafiri na kwa kutumia hizi pesa za rescue basi isaidie umma wote kwa kujaza pengo litakaloachwa na pungufu la kodi hiyo kimapato kwa kutumia hizo pesa.
 
Haya leo hii IMF imetangaza kuzipa nch maskini Billioni 8 kutokana na kuathiriwa uchumi wao..Ni zaidi ya kaisi kilichoombwa na nchi hizo kwa billioni 2..sasa wataalam wetu wataachaje kuzifanyia mahesabu ili tupate angalau dau kubwa ktk mkato wa huu msaada!..Kichekesho ni kwamba hayo mashirika 50 nadhani yatapita mengi kwa sababu sisi hatuna utamaduni wa Bunge kuyahoji hayo mashikrika na pengine mkaguzi wa mahesabu wa serikali kuwa shahidi wa serikali ktk kuwakilishwa hayo maombi..

Hatuwezi kufikiria nje ya tamaduni zetu kuwa neno MSINGI lina maana moja tu nayo ni FEDHA.. Mtu akiomba ama akisema anatafuta msingi bila shaka ana maana anatafuta fedha za kuanzishia shughuli yake..Na mara nyingi kama sii zote mtu huyo huwa hana aidea ya biashara anayotaka kuifanya..Hivyo ni ktk kukamilisha msemo wa kwamba Viongozi wetu ni reflection yetu..
Hawawezi kufikiria nje ya kabati la tamaduni za NDIVYO TULIVYO..
 
Jamani, tazameni jinsi Serikali yenu ilivyojaa uongo na inavyojikanganya.

Mary Nagu anatamka kukua kwa biashara na majirani kati ya mwaka 2007-2008 ambapo ni ongezeko marudufu la kuuza bidhaa, halafu leo tunaambiwa wameathirika kupita kiasi?

Hivi hawa jamaa wanafikiri sisi ni wajinga kiasi hicho?

SOSTHENES MWITA in Dodoma, 29th July 2009 Daily News

TANZANIA'S exports to other East African member states rose by 82.6 per cent last year, reaching 315.5 million US dollars, from 172.8 million dollars recorded in 2007, the Minister for Industry, Trade and Marketing, Dr Mary Nagu, said here yesterday.

Moving her ministry's budget estimates in the National Assembly, the minister said apart from East African countries -- Kenya, Uganda, Rwanda and Burundi, exports to SADC, Europe, America and the Gulf also surged.

Dr Nagu said SADC countries imported goods worth 443.4 million US dollars from Tanzania last year, up from 301.1 million US dollars recorded in 2007, reflecting an increase of 47.3 per cent.

The minister said Tanzania imported goods worth 6,439.9 million US dollars last year as compared to 4,860.6 million US dollars in 2007, she said. The industrial sector in the country grew by 9.9 per cent last year as opposed to the 8.7 per cent in 2007.

The minister asked the House to endorse 26,498,512,000/- to be spent on the ministry on recurrent votes and 29,206,157,000/- on development projects. Dr Nagu told the House that the manufacturing sector had 92,015 employees last year, up from 91,112 in 2007.

She said three cement factories -- Tanzania Portland Cement Company (TPCC), Tanga Cement Company (TCC) and Mbeya Cement Company (MCC) had a combined production of 1,770,000 tonnes of cement in 2007.

She said the demand for cement made TPCC to expand its factory and increase production to 1,400,000 tonnes annually, boosting the country's output to 2,970,000 tonnes this year.

The minister said that Minjingu Fertilizer Factory, which has an installed production capacity of 60,000 tonnes a year, increased production from 6,500 tonnes in 2005 to 40,000 tonnes last year.

The factory expects to start producing NPK fertilizer this year and increase output to 75,000 tonnes a year. The factory has a workforce of 441.

Dr Nagu told the House that establishment of new textile mills boosted production from 99.1 million square metres of cloth in 2005 to 150 million square metres last year, an increase of 34 per cent.

However, she said, the sector utilises only 20 per cent of locally produced cotton. The rest of cotton is exported raw.
 
Mimi nawaambia watu hapa kuwa Kikwete ana/ataiba pesa za wabongo kuliko viongozi wote waliomtangulia combined watu wanabisha. Wanaomtetea Kikwete hawasemi kizuri chochote alichofanya zaidi tu ya kuwa yeye ni mcha mungu na muungwana.

Akhhh kazi kweli kweli. Kikwete anaipeleka hii nchi kuzimu

I don't think Kikwete ni mkwapuaji, ila karidhika sana na Cheo cha Urahisi (sic) na fahari ya kuwa Raisi na kusahau wajibu wa kuwa Rais!
 
I don't think Kikwete ni mkwapuaji, ila karidhika sana na Cheo cha Urahisi (sic) na fahari ya kuwa Raisi na kusahau wajibu wa kuwa Rais!

I have never seen such a correct stetement!

Sasa hahitaji kingine...! Ndoto za utotoni zimefikiwa!

Chochote kitakacholikuta Taifa ..isnt his responsibility...Nyie ambao ndoto hazijatimia see where you fit .... and do whatever suite you...Its you r problem ..na nyie wekeni ndoto zenu...tafuteni njia ya kuzifikia...Hata mkiuza Nchi na rasilimali zake zote...swala si ndoto...Hata ikibidi kuwa bubu na kutokemea uovu wowote ili kuongeza chart ya kupendeza na kupendwa...ni swala la ku stabilise ndoto ili hatimaye kupumzika salaama baada ya kipindi cha pili...Mungu turehemu!

Karidhika saaana....Psychoticaly
 
Jamani eee; waambieni na mi wanipe hiyo tenda ya kuwasaidia kuchota pesa za uchaguzi (just making fun of them) !!!

Serikali inapaswa kujua kuwa sasa watu wameelimika na wanauelewa mkubwa.Kama kweli wako serious na hii stimulus package wafanye yafuatayo;

1. Mampuni yajiorodheshe na kuonesha ni jinsi gani yamepata hasara.

2. Orodha hiyo iwekwe public ili wenye kucontest hayo makampuni waweze kufanya hivyo kwa kutumia data.

3.Kuwe na mchakato uliowazi utakaopitishwa na Bunge la Tanzania kuidhinisha mikopo kwa kampuni ambazo zimeonyesha kweli zinastahili malipo ili watanzania waridhike kuwa pesa zao zimetumika ipasavyo.

4.Serikali isisistize kuwa hii ni mikopo itakayo tolewa na benki za biashara ambazo zitapata guarantee ya serikali ya hizo bil.21 ili kuziwezesha hizo kampuni kuwalipa wakulima na kuendelea na biashara ya ununuzi wa mazao.

5.Kwa kuwa mabenki ya bisharashara ndiyo hasa yanajua haya makampuni basi ndiyo yatumike kutoa hiyo mikopo na sio msaada kama Serikali inavyotaka kufanya sasa.

Endapo mchakato huo ukifanywa wazi kama nilivyoainisha hapo juu wananchi watakuwa na imani kwamba Serikali imedhamiria kweli kuwanasua na makali ya anguko la uchumi duniani.

Lakini kama serikali itafanya mambo kwa kificho kama inavyoelekea kufanya sasa basi isubiri kusulubiwa katika uchaguzi mkuu ujao ambao kwa kiasi kikubwa unachangamoto sana kwa chama tawala.
 
Back
Top Bottom