Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Najiuliza hivi ni makampuni gani hayo 50 ambayo yamepata hasara na kutaabikia kutokana na kuvurugika kwa Uchumi wa Dunia pale nchini kwetu Tanzania?
Ni shughuli gani za uzalishaji mali ambazo makampuni haya yanazifanya?
Je, ni wazalishaji wa ndani ya nchi wanaotumia mali ghafi na rasilimali kutengeneza bidhaa na kuziuza nje ya nchi na hivyo mapato yao yamekwenda fyongo na kuwa hasara tubu na bidhaa zao kudoda?
Je, makampuni haya yanaweza kutuonyesha vitabu vyao vya mahesabu vya takriban miaka mitano kabla ya May 2008, na mahesabu yao tangu May 2008 mpaka leo hii?
Je, Makampuni haya yanaweza kutuonyesha ni wapi masoko yao yalilipo na kutupatia takwimu za kiuchumi za nchi ambazo walikuwa wakipeleka bidhaa ili kudhihirisha kuvurugika kwa uchumi na hivyo kukosa soko la bidhaa zao?
Je, makampuni haya yanaweza kutuambia ni njia gani walizotumia hata pamoja na kutafuta masoko mapya ndani na nje ya nchi kuhakikisha kuwa bidhaa hizi zilizozalishwa na Wananchi wetu zinapata soko?
Je, ni lazima tuwape fedha kama fidia? kwa nini tusiwape mkopo wa kuongeza mtaji au kuwafutia kodi na ushuru japo kwa miezi 6?
Kama umeshafika hapa kunisoma, jiulize mbona Mchungaji haongelei makampuni yanayoagiza bidhaa kutoka nje?
Jibu lake ni kuwa wao wanaoagiza, hayajaingia hasara yeyote!
Kwanza wamepata faida marudufu kutokana na kununua bidhaa zao huko ughaibuni kwa bei rahisi na ya nichekee, hivyo itakuwa ni uopngo wakisema kuwa wamepata hasara!
Makampuni yanayoagiza bidhaa, wamepata faida kubwa kwa kununua bidhaa kwa bei ya chini , na bado wameendelea kuwalangua Watanzania kwa kisingizio uchumi wa dunia mbaya!
Hawa hawastahili msamaha wa kodi, kupewa mkopo au kupewa fidia.
Naomba uwasiliane na mwakilishi wako na pigia kelele jambo hili mpaka kieleweke.
Ikiwa kutakuwa na Kampuni inayopagiza bidhaa kutoka nje itadai imeingia hasara, naomba kampuni hiyo itupe orodha ya bidhaa inazoagiza, pamoja na nchi wanakonunua bidhaa hizi. Ama watupe thamani na bei ya bidhaa wanazoagiza tangu January 2006 mpaka leo hii ili tutoe tathmini ya kweli. Zaidi, watupe orodha inayoonyesha bei zao zikishafika nchini, pamoja na kumbukumbu za malipo yao ya ushuru na kodi kwa Serikali na stetimenti ya Benki zao kwa akaunti zao zote kwa miaka mitatu iliyopita.
Tukiweza kuyaona haya yote, ndipo tuanze mchakato wa kubaini ni nani apewe msaada wa kujihimu kutokana na kuanguka kwa uchumi wa Dunia.
La mwisho na ushauri wangu, ni hivi, Benki Kuu isichape noti mpya au kugawa pesa kama peremende, bali itoe mkopo wa riba ndogo au bila riba kabisa kwa makampuni yote ambayo yatathibitika yamepita vipimo vya mchungaji. Pili labda kuwepo na msamaha wa kodi na ushuru kwa makampuni yale yanayopeleka bidhaa nje (export) kati ya miezi 6 hadi mwaka mmoja.
Maoni yangu nayatoa kutokana na habari hii ninayoambatanisha hapa chini!
Makampuni 50 yaliyoathirika na mtikisiko wa uchumi kulipwa fidia
Na Salim Said
SERIKALI imeiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kufanya mchanganuo wa kampuni 50 ambazo zitapata uhalali wa kuingia katika orodha ya zile zitakazofidiwa na serikali baada ya kupata hasara kubwa kutokana na athari za mtikisiko wa uchumi ulioikumba dunia kuanzia mwaka jana.
Serikali ilitenga Sh 21.9 bilioni kwa ajili ya kuwanusuru kampuni zilizopata hasara kutokana na kuanguka kwa bei ya mazao katika soko la dunia.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijja aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwamba, tayari BoT imeanza mchakato wa kuratibu kampuni hizo.
Tayari BoT inafanya mchanganuo wa kuzitambua kampuni 50 ambazo ziliathirika zaidi na mtikisiko huu kwa kula hasara kutokana na kununua mazao kwa bei kubwa na kuyauza kwa bei ndogo, baada ya bei kushuka katika soko la dunia, alisema Khijja mara baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Shirikisho la Wenyeviwanda Tanzania (CTI).
Baada ya mchanganuo wa BoT tutaweza kujua ni kampuni gani inastahiki kupata fedha hizo na ipi haistahiki ili tusije kuingia katika hasara kwa kutoa fedha kwa kampuni ambazo hazikustahiki, alisema Khijja.
Khijja alibainisha kuwa, kuna baadhi ya kampuni ambazo zilipata hasara miaka mingi iliyopita, lakini tayari kuna nyingine ambazo zimejitokeza na kueleza kwamba nazo zimetikiswa kiuchumi.
Aidha alisema, serikali imeahidi kuzichukulia dhamana baadhi ya kampuni ili kuweza kupata mikopo katika benki mbalimbali nchini, lakini itafanya hivyo kwa zile kampuni ambazo hazina historia nzuri katika sura ya kibenki.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (Sido) Mike Laiser alilalamikia mabenki nchini kwa kutoza riba kubwa kwa wakopaji na kuweka riba ndogo kwa mtu anapoweka fedha benki.
Ukikopa unapigwa riba kati ya asilimia 18 hadi 25 lakini wewe ukiweka fedha benki riba yake ni asilimia mbili hadi nne, hili bado ni tatizo kubwa katika maendeleo ya SMEs, alisema Laiser.