Serikali kufanya uhakiki kwa watu waliotokea Msumbiji

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Wana jamvi

Serikali inaanza kuwahakiki watu waliofukuzwa kutoka Msumbiji na kuingia nchi juzi juzi katika operation iliofanyika nchini Msumbiji, hatua hii inakuja kujiridhisha kama wale wote waliorejeshwa ni watanzania wote au kuna wazamiaji, hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh Balozi Dr Augustino Mahiga wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Daresalaam.

Chanzo: ITV
 
Hatua nzuri sana, wakimaliza hii wakague raia wasiokua na vibali nao warudishwe makwao. Huruma yetu inatuponza wakati mwingne.

Sawa lakini lengo ni hilo kwa msumbiji kwanza ndio wa kuanza nao hao wengine zoezi linaendelea mikoa yote
 
... Kwa hiyo walivyokuwa wana cross mpaka wetu kurudishwa home migration hawakufanya hilo zoezi?
 
Ilikuwaje wakawakubali wote bila hata kuwahakiki pale pale mpakani Kama Sio mtz unamuacha hapohapo msumbiji wadili nae wenyewe!! Tanzania tumelala sana nchi zingine hawakukubali Kama huna document yoyote ya kuprove ni mwananchi wao!!
 
... Ni kweli kwamba jamaa ni wazamiaji?

Tusubiri taarifa lakini sidhani 100% wote, mi naipenda Israel na misimamo juu ya raia wake, Raia wake yoyote duniani akiguswa utasikia meno yanaumana pale Tel- aviv daah wanajua kuwatetea watu bana daah hongereni Israel
 
Tanzania wakimbizi wengi wako uraiani!!! Na wana vibali vyote tu. Unamuona mtu mkenya adi kiswahili cheke kibovu ila ananunua kiwanja na kujenga nyumba. Yaani adi wanigeria saivi wanaviwanja Tanzania. Hii nchi iliachwa wazi mda mrefu sana, kufanya uhakiki saivi itatambua asilimia ndogo sana ya wageni
 
Back
Top Bottom