Serikali kufanya tathmini ya ununuzi wa Pamba kabla ya msimu

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725


Serikali imesema inafanya tathmini ya hali ya ununuzi wa zao la pamba msimu wa mwaka 2019 ili kuondoa changamoto zilizojitokeza kabla msimu mpya wa ununuzi kuanza mwaka huu.

Akizungumza na viongozi wa wilaya ya Chato mara baada ya kutembelea viwanda vya kuchambua pamba, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema msimu mpya wa ununuzi utatangazwa mara baada ya tathmini ya msimu uliopita kufanyika.

“ Wizara imegundua kuwa hali ya mazao shambani kwa pamba bado ,kwani hata vitumba bado havijapasuka kutokana na uwepo mvua nyingi ,hivyo baada ya ziara hii kwenye mikoa ya kanda ya ziwa serikali itakaa na watalaam ili kuamua lini wakulima wataanza kuuza pamba yao kupitia Vyama Vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) “ alisema Kusaya

Aliongeza kusema kabla msimu haujafunguliwa serikali itahakikisha madeni ya wakulima,wanunuzi na ushuru wa AMCOS, halmashauri pamoja na mfuko wa pembejeo yanalipwa.

“Kila mwananchi atalipwa madai yake na jitihada za serikali ni kuona madeni haya yanalipwa kabla ya msimu mpya wa ununuzi wa pamba kuanza” alisitiza Katibu mkuu

Katika hatua nyingine Chama Kikuu cha Ushirika Chato( CCU) kimetakiwa kuhamasisha wakulima wengi zaidi kuzalisha zao la pamba ili ipate malighafi za kutosha kutumika kwenye kiwanda chake cha kuchambua pamba.

Kusaya alitoa wito huo kufuatia taarifa ya Meneja Mkuu wa Chama hicho Joseph Masingiri kusema kiwanda kimeshindwa kuendelea na uchakataji marobota kutokana na uhaba wa pamba ambapo msimu wa 2019 ni kilo milioni 13.6 ,000 tu zilinunuliwa wakati uwezo wake ni kilo milioni 30.

Ili kukabiliana na changamoto za zao hilo,Katibu Mkuu Kusaya amewataka wataalam wa halmashauri na wa chama kikuu kuhamasisha wakulima kuzalisha mazao ya mkonge na korosho ili kuwa na uhakika wa kipato pale zao la pamba linapoyumba.

“ Tulime pamba na mazao mengine ya biashara kama mkonge na korosho yanayostawi vizuri kwenye mkoa huu wa Geita na kanda ya ziwa yote .Wizara ya kilimo ipo tayari kuleta mbegu bora za mkonge na korosho toka taasisi za utafiti ili zigawiwe kwa wakulima “ Kusaya.

Kusaya alitaja faida za zao la mkonge kuwa katika kipindi cha miaka mitatu baada ya kupanda mkulima ataanza kuvuna na kuendelea hadi miaka kumi na tano huku akiendelea na kilimo cha mazao mengine .
 
'Akizungumza na viongozi wa wilaya ya Chato mara baada ya kutembelea viwanda vya kuchambua pamba, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya'.

Basi usimalizie kusoma kwani ukiisoma unautesa moyo wangu-Daz Nundaz 'BARUA'.
 
Back
Top Bottom