Serikali kufanya biashara, imefika mahali Serikali inafyatulisha matofali. Wananchi tujiajili kwa kazi zipi?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,869
49,554
Uzalendo kwanza,

Wakuu hii hali ya Serikali ya CCM awamu ya tano kufanya biashara ambazo sie wananchi tumejiajiri nazo ni jambo la kushangaza sana.Imagine kwa sasa wamefikia hatua ya kufyatulisha matofali ya kuuza kwa kupitia halmashauri ,magereza, JKT nk

Hivi kwa hali hii tutaishije? Saizi wameanzisha kampuni binafsi za ulinzi via suma jkt,polisi,magereza,migambo nk,ikumbukwe kazi hizi tulikuwa tunaomba kama tenda za huduma kwa sekta binafsi na Serikalini kwa sasa haitawezekana tena maana watajipa.Kampuni binafsi za ukandarasi wa majengo zilishajifia maana hizo kazi serikali inafanya yenyewe.

Kwa mfano kwa sie watu wa Tunduma tulikuwa tunajiajiri kwa kuanzisha parking yards tunapata chochote lakini kwa sasa serikali inajenga parking zao maelfu ya ekari ,hii inamaana watawalazimisha madereva wa malori kwenda kupaki maeneo yao halafu sisi tutapigwa jua.

Ifike mahala CCM na Serikali yao wajitafakari wanataka sie wananchi tufanye shughuli gani maana wameacha jukumu lao la msingi kututengenezea mazingira wezeshi tufanye biashara wao wakusanye kodi sasa nao wanaanza kufanya biashara hadi za mama ntilie,kukodisha frame nk nk, tunakwenda wapi mbona tunatiana kwenye umaskini?

Ina maana kwa miaka 5 ijayo huyu Magu akipita tutakuwa wanyonge square sio kwa hali hii,wananchi wenzangu tujitafakari kuichagua ccm maana sijui tutajiajiri kwa kazi gani sasa.
 
Wanasema tatizo hatuna ubunifu, sisi tunabeti angalau inasogeza siku za maisha mbele.
 
Lipo tatizo kubwa ktk sector nyingi serikali kufanya biashara.
Nachoshangaa ni kuona baadhi ya watu wanaona serikali iko sahihi,wanashindwa kujua ajira za vijana wao hazitapatikana,seems watanzania ni watu wa kuridhika na umaskini
 
Na wewe fanya biashara hizohizo ila uziboreshe utapata wateja. Mfano siku hizi pale Mwanza watu hawashobokei tofali za SUMA JKT maana wafyatua tofali wapo wengi tena tofali zenye ubora mkubwa kuliko wa zile za SUMA JKT na wanapiga show kama kawaida. Wewe ulitaka usiwe na ushindani ili utuuzie mibumbo siyo?
 
Hakika haitakiwi apite. Kijana mwenye akili timamu hawezi kusapoti CCM, CCM tuwaachie wazee wa nyerere
 
Kwa sasa ni mwendo wa TBA+SUMA JKT kwny kula mashavu.

Mfanyabiashara/mjasiriamali kwake ni adui mkubwa.
 
Kwa upande wa simu Magufuli amewalazimisha watumishi wote wa umma kutumia mtandao wa TTCL na kwamba ni marufuku ofisi ya umma kutumia mitandao mingine.
 
Mimi nilimuonaga yule muuza madafu akimuuzia Raisi nikaambiwa ni mtu wa Serikali

Nikajisemea kumbe hawa wauza mafenesi ni ni moja ya miradi ya Awamu hii ya Mao tse tung mweusi
 
Petty business ingebakia kwa wajasiriamali, serikali yenyewe ikajikita kwenye miradi mikubwa.
Lakini kuna vile vile uzembe ukishapata tenda unajisahau.
Kuna kampuni za ulizi za wazawa wataanza kazi vizuri mara baada ya miezi michache unagunduwa hawafai.
 
Wanaua tu sector binafsi Sasa Kama wana nguvu na pesa si wawafukuze wachina wajenge wao hiyo miradi Sasa wao wamekomalia miradi midogomidogo ili kutukomoa wajasiriamali.​
Wameshindwa kubuni sera na kuzisimamia.​
 
Petty business ingebakia kwa wajasiriamali, serikali yenyewe ikajikita kwenye miradi mikubwa.
Lakini kuna vile vile uzembe ukishapata tenda unajisahau.
Kuna kampuni za ulizi za wazawa wataanza kazi vizuri mara baada ya miezi michache unagunduwa hawafai.
Ndio maana kuna ushindani mkuu wa kazi ,hapo ni uzembe wa wafanya tathmnini
 
Back
Top Bottom