Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Serikali imesema itaendelea kuhakisha inasimamia nidhamu kwa watumishi wa umma.
Serikali imesema itaendelea kuhakisha kuwa inasimamia nidhamu kwa watumishi wa umma na kuweka mbele misingi masilahi umma na haitasita kuwawajibisha wale wote watakaoendelea kufanya kazi kwa mazoea kwa sababu sasa hivi serikali ipo kazini.
Hayo yamesemwa na Mh waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati akiahirisha bunge mjini Dodoma ambapo amesema serikali itaendelea kutumbua majibu bila ya kumwonea aibu mtu yoyote.
Aidha kuhusu hali ya chakula nchini Mh waziri mkuu amesema ni ya kuridhisha japo kwa maeneo ambayo ni lazima serikali inongeza nguvu.
Awali waziri wa fedha Mh Philipo Mpango amehitisha hoja yake ya mpango wa serikali wa maendeleo ambapo amesema serikali itahakisha kuwa inayafanyia kazi yale yote yaliyosemwa na waheshimiwa wabunge.
Pia katika mkutano huo waziri wa mambo ya nje na waziri wa mambo ya nje ya nchi, ushirikiano wa kimataifa na kikanda Africa Mashariki Balozi Dr. Augustine Mahiga ametoa kauli bungeni kuhususi sakata la wa kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kitanzania huko India.
Aidha bunge lilifanya uchaguzi wa wabunge ambao watawakilisha nchi katika mabunge mengine huku wabunge hao nao wakielezea nafasi zao katika mabunge hayo.