Serikali kuendelea kununua ndege huku barabara hazipitiki

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,325
Serikali imesema itaendelea kununua ndege katika mkakati wa kuikwamua Tanzania kutoka kwenye lindi la umaskini.
FB_IMG_1581165668724.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndege haziwezi kuondoa umasikini wananchi wa Ethiopia wasingekua wanaikimbia nchi yao
Kabudi jana kawashauri Ethiopia wajiulize raia wao wanakwama wapi hadi lindi la vijana wao kukimbilia nje.Tujitazame nasi lindi la umoja wa kitaifa na ustawi shakani, zipo kampeni nchi nzima ccm pekee, uvccm wanawakusanya vijana sharti wawe ccm kuwaunganisha na fursa mikopo ya kisheria toka halmashauri , manispaa na majiji.Tujitathimini pia kijani hakitavalika mtaani kwa mbegu ya chuki ccm wanayopanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyezisoma hizo plate namba aniambie ni za nchi gani. Ndugu panda ndege kuepuka adha hizo. Ununuzibwa ndege umekuwa slow sana naishauri serikali inunue nyingi zaidi.
 
Unanunua ndege shule hazina walimu wala miundombinu halafu unaenda kutafuta pilot nje ya nchi na kuwalipa pesa za kutupwa ndio akili matope ya urais wa Magufuli.
Karibia mika 60 tukiamua mambo yetu sisi wenyewe, ikiwa ni pamoja na mipango yetu ya maendeleo!

Wacha Aiseee, tumekosea sana njia, hasa kwenye miaka hii ya karibuni. Rubani wa ndege, bado tunakwenda kutafuta nje ya nchi? Hapo jirani Kenya wao wakipeleka marubani uarabuni!

Angalia, India, Pakistani, China, miaka chini ya 30, tayari wana bomu, sisi hata viatu hatuwezi tukatengeneza vyetu wenyewe!

Na dalili zote sasa zinaonyesha ndio tunazidi kudidimia kabisa chini ya utawala huu unavyoendesha mipango yake ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom