Serikali kudai fidia ya ndege kukamatwa. Yasitisha safari za Afrika Kusini kwasababu ya vurugu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,481
9,242

Serikali ya Tanzania imesema ipo katika mchakato wa kufungua kesi ya kudai fidia ya pesa iliyotumika kuendeshea kesi ya Ndege ya ATCL, iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dkt Damas Ndumbaro, amesema kuwa licha ya wao kushinda kesi dhidi ya kushikiliwa kwa ndege ya ATCL, lakini lazima itachukua hatua stahiki dhidi ya aliyefungua kesi hiyo.

''Sisi tumemaliza kesi kinachofuata ni kudai fidia kwa sababu Mahakama imetupa gharama yote ya kesi, kwahiyo tutadai gharama za kesi na fidia ya hasara ambayo tumeipata kutokana na kesi hii'', amesema Waziri Ndumbaro.

Ndege hiyo aina ya Airbus A220-300 ilizuiliwa nchini Afrika ya Kusini kwenye uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, kwa amri ya Mahakama, siku ya Agosti 24 na iliachiwa huru Septemba 4, 2019, hii ni baada ya Serikali kutuma jopo la Mawakili kwa ajili ya utetezi wa kesi hiyo.

Hermanus Steyn alifungua kesi ya fidia dhidi ya serikali ya Tanzania kwa kile alichodai kuwa alikuwa anamiliki ardhi, mifugo na mali nyingi ambazo zilitaifishwa na serikali ya Tanzania miaka ya 1980 na ilipofika miaka ya 1990 walikubaliana fidia atakayolipwa, kwa ujumla wake dola milioni 33 na tayari ameshalipwa dola milioni 20 kati ya hizo.
 
Wadai na fidia za hasara ATCL walizopata kwa ndege kuzuiliwa. Labda itasaidia kupunguza deni ............!!
 
Kosa la kwanza kwa waliofufua hili shirika ilikuwa ni kuendelea kutumia jina na kampuni hiyohiyo yenye madeni lukuki. Tungejifunza kwa wenzetu.
Kwa mfano, SABENA lilikuwa ni shirika la usafiri wa anga la Belgium. Kuna miaka ya 80s kwenda 90s, walikuwa na madeni, na biashara ikawa inakwenda mrama. Walichofanya ilikuwa ni ku-declare kampuni imefirisika. Kampuni ikifirisika unafanyaje? Wanakuja kufanya ukaguzi, kisha asset valuaation, kisha wanalipa most current liabilities mpaka pale mpunga utakapoishia. Baada ya hapo, inakuwa ni hasara kwa wote, hasa waliokuwa na equity (Kumbuka: Asset = Liabilities + Equity)
Kisha wakafungua Brussels airlines, inapiga mzigo mpaka leo
Pia mnakumbuka sakata la GM kule US, walifuata almost the same path
So, watu wamshauri St. John 'The Stone'. Liquidate ATCL kisha fungua kampuni nyingine, anza upya
 
Hiyo ndege haikukamatwa kutokana na deni la nyuma la ATCL bali kutokana na deni la serikali ya Tz hivyo kubadili jina la ATCL sio suluhisho.
Uamuzi wa serikali wa kupata kwanza insurance kutoka serikali ya Afrika Kusini kabla ya kuendelea na safari ni bora na wa muhimu ili tukio kama hilo lisitokee tena kwa nchi ya Afrika Kusini pia kumfungulia kesi ya madai huyo mkulima itakuwa funzo kwa wengine watakaotaka kujaribu kufanya ujinga huu huu.
 
Fidia ya hasara haiwezi kufikia $10,000,000 ambayo ndo chenji anayoidai huyo mzungu..sababu hata kama tiketi ya ndege husika ni $500 x 220 = $110,000 uzoefu unaonesha ATCL haijawahi kwenda na abiria wengi wa kiasi hicho ime hua wanakuaga atleast 70-100 na tiketi za ATCL ni chini ya $500 i.e $288-350, gharama za kuhifadhi ndege siku zote hizo haziwezi kufika hata $50,000 kwa siku ilizokaa hio ndege hata ukisema ATCL inafanya safari mara 4 kwa wiki gharama hazifiki $1,000,000 ukijumlisha gharama za mawakili hazitafika $3,000,000 kwaio wana $7,000,000 za kumlipa mkulima...
 
Bado deni halijaisha litaendelea ni suala la muda tu tusubiri muone kesho yake ni nzuri kuliko jana
 
Yeye alikuwa na haki ya kudai haki yake mahakamani na mahakama ilimsikiliza; wakati unapofika na yeye atadaiwa na itapigwa hesabu kiasi kwamba lile salio alilokuwa analidai litafutwa na deni jipya au akikataa kulipa mali yake itakamatwa vile vile - bahati nzuri ya kwake haiwezi kupaa!
 
Ndege haifanyi safari moja tuu,inaenda SA inarudi inaenda mwanza mara 2,na bado inaweza kwenda harare siku hiyo hiyo
Fidia ya hasara haiwezi kufikia $10,000,000 ambayo ndo chenji anayoidai huyo mzungu..sababu hata kama tiketi ya ndege husika ni $500 x 220 = $110,000 uzoefu unaonesha ATCL haijawahi kwenda na abiria wengi wa kiasi hicho ime hua wanakuaga atleast 70-100 na tiketi za ATCL ni chini ya $500 i.e $288-350, gharama za kuhifadhi ndege siku zote hizo haziwezi kufika hata $50,000 kwa siku ilizokaa hio ndege hata ukisema ATCL inafanya safari mara 4 kwa wiki gharama hazifiki $1,000,000 ukijumlisha gharama za mawakili hazitafika $3,000,000 kwaio wana $7,000,000 za kumlipa mkulima...
 
Kuna ndege yoyote iliyoathirika kutoka na vurugu za South,au ndio wamepata sababu ya kutia mpira kwapani wakati wa mapumziko?

Yaani jinsi tunavopambanua mambo kuna walakini. Wanataka kuifanya kama vile kuna vurugu uwanjani OT na safari za ndege zimeathirika. Kilicho rahisi hapa ni woga wa ndege kushikiliwa tena (kama mkulima atakata rufaa na mahakani kutoa hukumu in his favour). Ninahisi huu ni mwisho wa ndege zetu kwenda kwenye nchi ambazo mahakama zao ziko huru!!
 
Yeye alikuwa na haki ya kudai haki yake mahakamani na mahakama ilimsikiliza; wakati unapofika na yeye atadaiwa na itapigwa hesabu kiasi kwamba lile salio alilokuwa analidai litafutwa na deni jipya au akikataa kulipa mali yake itakamatwa vile vile - bahati nzuri ya kwake haiwezi kupaa!

Mkuu nisaidie jambo hili. Mkulima alipata ruhusa ya mahakama kuzuia ndege isiondoke na ndio maana respondents wengine walikuwa ni wale watakaosimamia utekelezaji wa maamuzi ya mahakama. Sio kwamba mkulima alikuwa na namna ya kuishikilia kwa namna yake bila kuhitaji mtu mwingine (kama kuchukua basi la mtu na kulifungia uani kwa mdeni wangu, ka mfano).

Katika hali kama hii - hasara imesababishwa na nani? Hukumu ya mahakama???
 
Ndege haifanyi safari moja tuu,inaenda SA inarudi inaenda mwanza mara 2,na bado inaweza kwenda harare siku hiyo hiyo
Inayoenda harare ni ingine tofauti hio ya SA ni TC209 na pia wakati hii ikezuiwa ndege ya Harare ilikua inapiga kazi na ya Mwanza ilikua inapiga kazi
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom