Serikali kuchunguza madai wananchi kuibiwa data, vifurushi na kampuni za simu

Hivyo ni vifurushi vya uchumi wa kati.
Mfabo hii nimeisoma hukp Facebook sijui nn kitajili maana nilivyosoma na kutaka kujiunga kinternet kwa kutumia mtandao wa tigo ndo nashangaa kuona gharama zinapanda badala ya kushuka.
Screenshot_20210127-155758.jpg
 
Mchawi ni serikali mtapoteza muda wenu wenu kuwalaumu!!wao pia ni wafanya biashara, kodi ziko juu wafanyeje?!!mngeanza kwanza na kupiga kelele na TTCL, ni shirika la serikali mbona na wao wako juu, wakati ni shirika la umma?!!jana umemsikia waziri wa viwanda juu sakata la kupanda kwa bei za mafuta ya kupikia?ndio utajua kuwa kwa sasa ni ngumu serikali kumsaidia mwananchi!!na mambo yako juu ya uwezo wao, kwani bei za manunuzi huko nje zimepanda, serikali kuwasaidia wananchi wake, ni kupunguza kodi ili bei iwe ile ile!!kodi iko pale pale bei za bidhaa zitashuka vipi? Kodi kila leo zinapanda bei zitapungua vipi?
Akijibu hii unitag.
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amelielekeza Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA- CCC) kufanya tathmini ya malalamiko yanayotolewa na wananchi dhidi ya kampuni za simu kuhusu kukatwa na kuibiwa vifurushi ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

Dkt. Ndugulile ametoa maelekezo hayo alipokutana na watendaji wa baraza hilo pamoja na Tume ya Taifa ya Tehama kuangalia utendaji wa taasisi hizo na namna zinavyoweza kusaidia Serikali kwenda na kasi ya maendeleo ya teknolojia.

Kwa mujibu wa waziri huyo, kumekuwa na malalamiko mengi ya wananchi kuhusu vifurushi vinavyotolewa na kampuni za simu hivyo ni muhimu kuyafanyia kazi ili ufumbuzi wake upatikane.

Amesema taarifa alizonazo ni kwamba wananchi wanalalamikia huduma za vifurushi ikiwemo kupunjwa na kutozwa fedha nyingi tofauti na data au muda wa maongezi wanaopewa na kutaka suala hilo kupatiwa ufumbuzi.

Hata hivyo, amewataka wananchi kuitumia vizuri mitandao kwa kuwa sheria zipo na hataki ifike wakati Serikali inaingia kwenye mikinzano na wananchi kwa sababu ya mitandao.

Katibu Mtendaji wa TCRA-CCC, Mary Msuya amekiri malalamiko mengi dhidi ya kampuni za simu na kuahidi kutekeleza maelekezo ya waziri ili kutatua changamoto wanazokumbana nazo.
MWENYE MREJESHO PLEASE
 
Yani hela yangu,najiunga halafu et napangiwa mpaka siku fulani na muda fulani ndo mwisho wa matumizi.Kwanini isiwe kama luku?kwamba matumizi yangu ndo yawe limit ya kifurushi?

Huu wa sasa ni wizi
 
Back
Top Bottom