Serikali kuchukua hatua dhidi ya wahujumu BoT?

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
802
Serikali kuchukua hatua dhidi ya wahujumu BoT

*Balozi wa Ufini ashangaa kasi ya tuhuma za rushwa
*Ahoji: Mbona taasisi za kimataifa zinatoa ripoti nzuri?


Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu, Bw. Edward Lowassa amesema Serikali ndiyo iliyoitisha uchunguzi wa hesabu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na itachukua hatua kuhusu tuhuma za rushwa endapo ripoti ya wakaguzi wa kimataifa, waliopewa kazi ya kuikagua benki hiyo itathibitisha hivyo.

Alikuwa akizungumza na Balozi mpya wa Ufini nchini, Bw. Juhan Toivonen, aliyekwenda kumtembelea ofisini kwake mtaa wa Magogoni Dar es Salaam jana.

Bw. Lowassa alisema ni vema mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania wakajua ukweli, kwamba Serikali imeamua kwa dhati kupambana na rushwa na kwamba ndiyo iliyoitisha uchunguzi wa BoT.

"Ripoti ya ukaguzi ikikamilika, Serikali itachukua hatua zinazostahili, kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Nne imedhamiria kweli kupambana na rushwa kwenye ngazi zote," alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Nne, kamwe haifanani na Serikali inayoendekeza rushwa kama zinavyoonesha taarifa zinazochapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari nchini hivi sasa.

"Kama ingekuwa ni Serikali inayoendekeza rushwa, basi ni dhahiri ingeshindwa kukusanya kodi…ingeshindwa kupeleka mabilioni ya fedha za maendeleo kwa wananchi vijijini, kama ilivyofanya katika bajeti ya mwaka huu," alimwambia Balozi huyo.

Serikali ya Awamu ya Nne sasa inakusanya wastani wa sh. bilioni 250 kwa mwezi ikilinganishwa na sh. bilioni 25 za mwaka 1995/96. Katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, Serikali pia ilipeleka sh. bilioni 286 kwa halmashauri za wilaya kwa ajili ya kugharimia shughuli za maendeleo.

Bajeti ya mwaka huu ambayo ni kubwa kifedha kuliko yoyote iliyowahi kupitishwa katika historia ya nchi hii, vilevile imetenga maeneo ya kipaumbele na kuyapa fedha za kutosha.

Elimu imetengewa sh. trilioni moja; Miundombinu (Barabara) sh. bilioni 777, Afya sh. bilioni 589.9; Kilimo sh. bilioni 379 na Maji, sh. bilioni 309.

Naye Balozi alisema anashangazwa na kasi ya taarifa za tuhuma za rushwa katika vyombo vya habari nchini, wakati ukweli ni kwamba taasisi za kimataifa za uchunguzi wa rushwa zinatoa ripoti nzuri kwa Tanzania.

Shirika la Kimataifa la Kupambana na Rushwa (Transparency International) katika ripoti yake ya hivi karibuni, lilieleza kuwa Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki kwa mapambano dhidi ya rushwa. Tanzania ilikuwa nchi ya 14 katika Afrika wakati Uganda ni ya 22 na Kenya ikiwa ya 42.

Balozi Toivonen alisema nchi yake inakamilisha taratibu za kuipa Tanzania msaada wa dola milioni 36 za Marekani (kiasi cha sh. bilioni 45) katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Waziri Mkuu pia alionana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Dk. Kandeh Yumkella na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa, Balozi Keitaro Sato, ambaye aliwahi kuwa Balozi wa Japani nchini.
Source: Majira
 
Ukaguzi wa BoT ndiyo umekuwa wimbo wa Taifa wa kujitetea ... wakati tunajua wazi kwamba swala hilo la ukaguzi wa fedha hizo za nje ni shinikizo la kutoka nje. Kibaya zaidi agenda ya ukaguzi wa mahesabu hayo haihusu ubadhirifu ambao umeainishwa na report ya CAG, lakini ninamshangaa EL kukomaa kwamba wahusika watachukuliwa hatua.

Serikali inaweza kukusanya fedha nyingi sana, lakini je fedha hizo zinatumika bila ya kufunjwa? CAG report ya mwaka wa fedha ulioisha imeonyesha mabilioni ya shilingi ambayo yalitumika katika ununuzi hewa wa vitu na kuna hela ambayo haikuwa accounted for, je hilo Bwana EL anasemaje? Maana naona anajisifia tu kwamba serikali yake inakusanya kodi nyingi. Swala kubwa ni harufu ya rushwa na ubadhirifu. Na rushwa inayoongelewa hapa ni hiyo ya kwenye mikataba ambayo wao wameifanya iwe siri. Mbona hawataki kuweka wazi mkataba wa Richmonduli. Pia mbona mkataba wa ujenzi wa Twin Towers nao ulifichwa hata pale wakaguzi walipotaka kujua mkataba unasemaje? Hayo ana majibu yake?

EL usije na majibu mepesi ambayo hata mabalozi watakuona wewe hamnazo maana unajibu maswali ambayo hujaulizwa. Na hata justification ya kwamba nchi/serikali yako haina rushwa sioni kama ina hold water.

Sasa balozi anapopata puzzle kwamba kwanini kuna tuhuma nzito sana za rushwa na bado report za kutoka nje zinaonyesha Bongo mambo safi? Hapo ndipo palipo na kiini macho. Serikali imekuwa kwa makusudi kabisa inaficha mikataba ili kutoonyesha harufu za rushwa. Wacha tusubiri report za TI baada ya kuvuja kwa Mkataba wa Buzwagi ambao tumeambiwa umeboreshwa zaidi kuliko ya miaka iliyopita. Sijui hao TI watapata picha gani?
 
Shirika la Kimataifa la Kupambana na Rushwa (Transparency International) katika ripoti yake ya hivi karibuni, lilieleza kuwa Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki kwa mapambano dhidi ya rushwa. Tanzania ilikuwa nchi ya 14 katika Afrika wakati Uganda ni ya 22 na Kenya ikiwa ya 42.

Taarifa ndivyo zinavyoonesha. Ni kweli tumepiga hatua lakini kuna wanaotuvuta mashati. Kuna mambo hayaendi sawa. Kama EL aliyoyaongea dhidi ya tuhuma za BoT na endapo uchunguzi utakuwa na majibu 'tarajiwa' na wananchi na wakachukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na kuwafilisi wote waliohusika basi itakuwa mojawapo ya hatua kubwa kwenye mapambano dhidi ya Rushwa.

Kinyume na hapo... Watanzania wataendelea kuona usanii. Neno hili usanii linaweza kufutika kwa kuweka bayana mambo.

Bado tunaweza!
 
Ukaguzi wa BoT ndiyo umekuwa wimbo wa Taifa wa kujitetea ... wakati tunajua wazi kwamba swala hilo la ukaguzi wa fedha hizo za nje ni shinikizo la kutoka nje. Kibaya zaidi agenda ya ukaguzi wa mahesabu hayo haihusu ubadhirifu ambao umeainishwa na report ya CAG, lakini ninamshangaa EL kukomaa kwamba wahusika watachukuliwa hatua.

Serikali inaweza kukusanya fedha nyingi sana, lakini je fedha hizo zinatumika bila ya kufunjwa? CAG report ya mwaka wa fedha ulioisha imeonyesha mabilioni ya shilingi ambayo yalitumika katika ununuzi hewa wa vitu na kuna hela ambayo haikuwa accounted for, je hilo Bwana EL anasemaje? Maana naona anajisifia tu kwamba serikali yake inakusanya kodi nyingi. Swala kubwa ni harufu ya rushwa na ubadhirifu. Na rushwa inayoongelewa hapa ni hiyo ya kwenye mikataba ambayo wao wameifanya iwe siri. Mbona hawataki kuweka wazi mkataba wa Richmonduli. Pia mbona mkataba wa ujenzi wa Twin Towers nao ulifichwa hata pale wakaguzi walipotaka kujua mkataba unasemaje? Hayo ana majibu yake?

EL usije na majibu mepesi ambayo hata mabalozi watakuona wewe hamnazo maana unajibu maswali ambayo hujaulizwa. Na hata justification ya kwamba nchi/serikali yako haina rushwa sioni kama ina hold water.

Sasa balozi anapopata puzzle kwamba kwanini kuna tuhuma nzito sana za rushwa na bado report za kutoka nje zinaonyesha Bongo mambo safi? Hapo ndipo palipo na kiini macho. Serikali imekuwa kwa makusudi kabisa inaficha mikataba ili kutoonyesha harufu za rushwa. Wacha tusubiri report za TI baada ya kuvuja kwa Mkataba wa Buzwagi ambao tumeambiwa umeboreshwa zaidi kuliko ya miaka iliyopita. Sijui hao TI watapata picha gani?

Mkuu uliyoandika yananifanya nichoke zaidi! Dah, kuna mambo mengine si ya kukumbuka. Halafu kuna issue ya hawa mabalozi...

Pia nakosa imani kuwa majibu haya yanayotolewa na Waziri mkuu na waziri wa Fedha (Kuzirejesha hela za wote waliozikimbiza nje) kwani yanaonekana kuwa magumu kutimizika.

Labda inawezekana... Lakini hata muda wenyewe mdogo! Hivi barabara ya Sam Nujoma ilishakamilika (ambayo ilikuwa ikamilike mwaka jana - 4km road)
 
Ongoing BoT special audit: World Bank official pushes for action

-’We always want to trust our partners in development...’


MASATO MASATO said:

Dar es Salaam

THE World Bank says it is hoping for a truly serious investigation into reports of massive funds misuse at the Bank of Tanzania (BoT), as well as the adoption of strict remedial measures on the part of the government to avoid a repeat of the alleged improprieties at the central bank.

’’We at the World Bank would like to see due process fully applied in the investigation, and proper remedial measures taken,’’ the visiting World Bank vice-president for the African region, Ms Obiageli Ezekwesili, said in Dar es Salaam yesterday.

’’I hope and believe that necessary steps to ensure due diligence in the investigation will be adhered to?we always want to trust our partners in development,’’ added Ms Ezekwesili in an exclusive interview with THISDAY.

The recently-appointed VP of the World Bank made the remarks in response to questions about the Bank’s position on the reported disappearance of millions of US dollars from the BoT’s external payment arrears (EPA) account, now the subject of a special government audit ordered by the International Monetary Fund (IMF).

Ms Ezekwesili, who is more comfortable with the knickname ’Oby’, is a former minister of education in her native Nigeria. She was appointed to the IMF post in March this year.

On his part, the World Bank’s country director for Tanzania, John Murray McIntire, told THISDAY that the Bank was keenly monitoring developments in the ongoing BoT audit ordered by its sister institution IMF.

McIntire added that since the audit on the EPA’s 2005/06 records was still underway, the final audit report should be awaited before jumping to any conclusions.

Earlier, Ms Ezekwesili said the country has made impressive strides in attaining macro-economic stability, but added that much more effort was needed to achieve faster economic growth.

While acknowledging that the macro-economic figures were not fairly reflected in the lives of the ordinary Tanzanian man in the street, she said the numbers cannot be ignored either. ’’These are statistics that we cannot take away,’’ she argued, saying the country now needs a sustained economic growth rate of over 7 per cent to ensure that the effects eventually trickle down to citizens in the rural areas where the majority poor live.

On the subject of education sector growth, the World Bank VP saluted the government for boosting school enrolment numbers, but added that there was a need to improve the quality of education in the country.

’’I have visited a school at Ilala (in Dar es Salaam), where I found over 100 children in a single classroom. But those students were very excited to be in school at all,’’ said Ms Ezekwesili, who is particularly conversant with the subject as a former Nigerian minister in charge of education.

She added: ’’True, plenty of investment is still needed to improve quality of teachers, classrooms, text books ...but it’s good that the government has started.’’

Ms Ezekwesili is also one of the founding members of Transparency International, an organization dedicated to fighting worldwide corruption. This is her first official visit to Tanzania as World Bank VP, where she is scheduled to tour a number of local projects supported by the bank.

Various prominent development partners have in recent weeks threatened to impose an aid freeze on the country if there is no real seriousness in addressing widespread allegations of high-level corruption in the country. The ambassadors of the United States, United Kingdom and the Netherlands in Tanzania have publicly criticised the government for failing to take any real action against the allegations.

Diplomats are concerned that corruption could see billions of shillings in aid money ultimately line the pockets of dishonest local officials while ordinary Tanzanians continue to struggle in conditions of abject poverty.

The incumbent BoT Governor, Dr Daudi Ballali, has for the best part of the year been under mounting pressure to resign as a sign of accountability in the face of the widespread allegations of serious payment improprieties at the central bank. In the meantime, the government on September 10 this year appointed Massawe Ernst & Young company to conduct the special audit of the EPA account within a set 60-day deadline, ending in early November 2007.



Halafu EL anatuambia eti watawashughulikia wakati hata hizo actions ni shinikizo kutoka nje. Mwaka huu haponi mtu, labda kama report ya hao Auditors kama itasafisha huo uchafu.
 
Tujihadhari pia na takwimu, maana watu wanaweza kumanipulate takwimu na kufanya tuonekane tuko bora kumbe tuko hovyo. Takwimu za Kimataifa siyo za kuamini sana nazo, tuangalie hali halisi sisi tunavyoiona hapa ndani. Zipo baadhi ya taarifa zenye utata hebu angalia pia mfano wa taarifa ya mwaka huu ya Global Peace Index and the Economist Intelligence Unit (kama ilivyotolewa na Vision of Humanity http://www.visionofhumanity.com), Tanzania ni ya 57 kwa amani wakati tunajidai kuwa sisi ni kisiwa cha amani.!!!

Kwa hivyo suala la ripoti za Kimataifa kueleza kuwa rushwa nchini Tanzania inapungua si sababu pekee ya kutufanya turidhike kuwa tunafanya vyema. Inabidi tutazame kwa kina zaidi.
 
Benki ya Dunia yadai uchunguzi

na Ratifa Baranyikwa

WAKATI serikali ikisuasua kufikia uamuzi wa kuzishughulikia tuhuma za ubadhirifu ndani ya Benki Kuu (BoT) zilizotolewa hivi karibuni na Dk. Willibrod Slaa (Karatu-CHADEMA), Benki ya Dunia imesema ni matumaini kuwa, serikali itachukua hatua madhubuti kuhusu tuhuma hizo.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, Obiagel Ezekwesili, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kuhudhuria mkutano unaohusu masuala ya ukimwi utakaofanyika mkoani Arusha.

Benki ya Dunia imetoa kauli hiyo wakati serikali ikisisitiza kuwa Dk. Slaa na wengine wanaotoa tuhuma hizo wanatakiwa kwenda mahakamani na wala haijawahi kugusia kuwa itafanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ili kubaini kama ni za kweli au la.

Hata hivyo, Ezekwesili alisema kuwa Benki ya Dunia, inataka kuona hatua za kuchunguza madai hayo zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuweka wazi kile kitakachobainika katika uchunguzi huo.

Akizungumzia suala la uchunguzi ambao unaendelea kuhusiana na tuhuma nyingine zinazoihusu BoT, alisema Tanzania kama nchi, inao uhuru wa kufanya uchunguzi wao, na wao kama Benki ya Dunia haingilii bali wanachotaka ni kuona hatua zinachukuliwa.

Serikali, kupitia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeiagiza kampuni ya kimataifa kufanya ukaguzi BoT kuhusiana na ubadhirifu wa mabilioni ya shilingi zinazodaiwa kufujwa kupitia akaunti ya kulipia madeni ya nje.

Uchunguzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi ujao na Dk. Slaa na wapinzani walioibuka na tuhuma nyingine wanadai kuwa kinachokaguliwa katika BoT ni sehemu ndogo sana ya ubadhirifu ambao umefanywa ndani ya chombo hicho nyeti katika uchumi wa nchi.

Ezekwesili alisema kitendo cha BoT kutuhumiwa hadharani kinaweza kuwa ni matokeo ya kutokuwepo kwa uwazi katika shughuli zake, utekelezaji na ukaguzi wa mahesabu.

Wakati Benki ya Dunia ikitoa mwelekeo huo huo, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, jana alisisitiza kuwa, serikali ndiyo iliyoagiza ukaguzi wa hesabu za BoT na itachukua hatua kulingana na matokeo ya ukaguzi unaofanywa hivi sasa.

Akizungumza na Balozi mpya wa Finland nchini, Juhan Toivonen, aliyekwenda kumtembelea ofisini kwake Mtaa wa Magogoni jijini Dar es Salaam jana, Lowassa alisema kuwa ni vema mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wakafahamu kuwa Serikali imeamua kwa dhati kupambana na rushwa na kwamba ndiyo iliyoitisha uchunguzi BoT.

"Ripoti ya ukaguzi ikikamilika, Serikali itachukua hatua zinazostahili kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Nne imedhamiria kikweli kupambana na rushwa kwenye ngazi zote," alisema.Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Nne kamwe haifanani na serikali inayoendekeza rushwa kama zinavyoonyesha taarifa zinazochapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari nchini hivi sasa.

"Kama ingekuwa ni serikali inayoendekeza rushwa, basi ni dhahiri ingeshindwa kukusanya kodi… ingeshindwa kupeleka mabilioni ya fedha za maendeleo kwa wananchi vijijini kama ilivyofanya katika bajeti ya mwaka huu," alisema.

Hivi sasa Serikali inakusanya wastani wa sh bilioni 250 kwa mwezi, ikilinganishwa na wastani wa sh bilioni 25 tu mwaka 1995/96. Katika bajeti ya mwaka huu, Serikali pia imepeleka sh bilioni 286 kwa halmashauri za wilaya kwa ajili ya kugharimia shughuli za maendeleo.

Bajeti ya mwaka huu vilevile imetenga maeneo ya kipaumbele na kuyapa fedha za kutosha.

Chini ya utaratibu huo elimu imetengewa sh trilioni 1; miundombinu (barabara) sh bilioni 777, afya sh bilioni 589.9; kilimo sh bilioni 379 na maji sh bilioni 309.

Kwa upande wake, balozi huyo alisema hata naye anashangazwa na kasi ya taarifa za tuhuma za rushwa katika vyombo vya habari nchini wakati ukweli ni kwamba taasisi za kimataifa za uchunguzi wa rushwa zinatoa ripoti nzuri kwa Tanzania.

Shirika la Kimataifa la Kupambana na Rushwa (Transparency International) katika ripoti yake ya hivi karibuni, limeeleza kuwa Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki kwa mapambano dhidi ya rushwa. Tanzania ilikuwa nchi ya 14 katika Afrika wakati Uganda ni ya 22 na Kenya ikiwa nyuma, 42.

Balozi Toivonen alisema kuwa nchi yake inakamilisha taratibu za kuipatia Tanzania msaada wa dola za Marekani milioni 36 (sawa na takriban sh bilioni 45) katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Source: Tanzania Daima
 
Hivi hao WB hawajui anayetoa (Elinani) taarifa kwamba watachukua hatua ni mmojawapo wa wezi?
 
Ni kweli kwamba toka September.10 Jamaa wa Massawe Ernest & Young wanafanya Ukaguzi huko BOT utakaowachukua siku 60.Kazi hiyo inatarajiwa kukamilika November.10.Sina imani sana na Ukaguzi huu ambao unaitwa wa kampuni ya Nje na Binafsi!.Huyu Mzee Massawe, partner wa E&Y ana mahusiano ya karibu ya kibiashara na watu wa BOT na HAZINA.Kwa maana hiyo hapo kuna conflict of interests, kwa mtazamo wangu kama ilikuwa ni lazima kuwatumia E&Y kungeitwa Meneja na timu Mpya kutoka popote lakini sio Timu hiyo ya Massawe.

Hao ma-partner wa hizo kampuni kubwa za Ukaguzi za nje wana mahusiano ya karibu na Serikali na ofisi ya CAG,kwa maana hiyo kufanya Ukaguzi wa kuwaumbua marafiki zao nafikiri si rahisi sana. Massawe wa Ernest & Young na Mndolwa wa PWC Wote ni washirika na timu moja na Viongozi wa serikali.Tusubiri tuone huo Ukaguzi kama anavyodai Waziri Mkuu.
 
Inaonekana WB wana usongo sana na hayo mahesabu. Sasa ole wake Massawe afanye madudu, inawezekana akawaharibia jina partner wake. Nina mashaka sana kwamba WB wana data nyingi sana lakini hawajataka kuziweka wazi na hivyo wanasubiri huyo Auditor aje azifanyie kazi. Mara baada ya zoezi hilo kukamilika kama Auditors watatoa report fake nina mashaka credibity ya Kampuni hiyo ya kimataifa inaweza kwenda na maji. Hapo wanahitaji kusuka ama kunyoa, vinginevyo wanaweza kuwa wanajichimbia kaburi la kibiashara!
 
Inaonekana WB wana usongo sana na hayo mahesabu. Sasa ole wake Massawe afanye madudu, inawezekana akawaharibia jina partner wake. Nina mashaka sana kwamba WB wana data nyingi sana lakini hawajataka kuziweka wazi na hivyo wanasubiri huyo Auditor aje azifanyie kazi. Mara baada ya zoezi hilo kukamilika kama Auditors watatoa report fake nina mashaka credibity ya Kampuni hiyo ya kimataifa inaweza kwenda na maji. Hapo wanahitaji kusuka ama kunyoa, vinginevyo wanaweza kuwa wanajichimbia kaburi la kibiashara!

Hilo unalo sema ni kweli, Kwani Madudu Yote ya BOT yamesambaa kila kona, kwahiyo kila mtu ana subili yawe formal, lakini asilimia kubwa yanajulikana!
Hii ndiyo nafasi pekee ya kurusha turufu yao, wakicheza tu watajimaliza wenyewe! wacha tusubili tuone watakavo jikaanga ama watakavo jiiburia turufu kubwa!
 
Quote:

"Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Nne, kamwe haifanani na Serikali inayoendekeza rushwa kama zinavyoonesha taarifa zinazochapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari nchini hivi sasa.

"Kama ingekuwa ni Serikali inayoendekeza rushwa, basi ni dhahiri ingeshindwa kukusanya kodi…ingeshindwa kupeleka mabilioni ya fedha za maendeleo kwa wananchi vijijini, kama ilivyofanya katika bajeti ya mwaka huu," alimwambia Balozi huyo. "



Mimi sioni any correlation between misemo miwili ya ndugu waziri mkuu; "kuendelea kula rushwa" na "kutoshindwa kukusanya kodi na kupeleka mabilioni ya fedha za maendeleo kwa wananchi vijijini". Hapa ninafikiri ndugu Lowassa anajaribu kutoa tu maelezo in a political style ili kuendelea kuwachezea akili wadanganyika. Binafsi sioni hoja yoyote iliyojengeka hapa. Huwezi kuchanganya ukusanyaji wa kodi unaofanywa na organization nyingine (TRA) pamoja na upokeaji rushwa uliofanywa na mafisadi ambao ndio waliokua wakizungumziwa kwenye maongezi yake na balozi huyu mpya. Hivi ni vitu viwili tofauti vilivyofanywa na vyombo viwili tofauti vinavyojitegemea. Hakuna aina yoyote ya mahusiano kati ya vitu hivi viwili. Kungekuwa na mahusiano kama balozi wa Finland angelalamikia ufisadi wa TRA in relation to ukusanyaji wake wa kodi. Hapa ndugu waziri alikua anataka kutuchanganya tu.

Unaweza kukusanya kodi kubwa kwa kutumia chombo kimoja (TRA kwa mfano) wakati huohuo Mafisadi wa idara nyingine ya serikali wakawa wanakula rushwa ya mabilioni ya shilingi ili kujibinafsisha wao wenyewe.

I wish vijana wa form one wangeisoma hii point ya Lowasa na kumchapa swali atakapoenda kuwahutubia... Unaweza ku-predict reaction ya waziri itakuwaje.

Viongozi, akili za wadanganyika zimechoka kuchezewa.... MUACHE. Fateni maadili..
 
Pesa iliyopotea yetu hadi twende kupiga magoti kwa wakubwa ati waje kufanya hesabu, yaani hawa watakomba pesa zaidi mara mia na kitakachotoka bila shaka ni utumbo wa kulindana, Hii shughuli ilitakiwa kufanywa na Kamati ya bunge ambayo ndio moja ya kazi zake mizengwe kama hii inapotokea. Je serikali ilikuwa inaogopa nini kuwaambia wabunge wachunguze ubadhirifu/tuhuma huu/hizi?
 
JK afanya kweli

2007-10-03 17:53:44
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Kuna taarifa kuwa Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete imeanza kufanya kweli kwa kuchukua hatua za dhati kubaini wale wote wanaonacheza `dili chafu` za kutafuna mapesa ya nchi na kulipaka matope taifa.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinasema uchunguzi wa chini kwa chini dhidi ya watu kadhaa wanaokisiwa kuwa katika kundi hilo la wachonga dili unaendelea.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya vigogo ambao mwenendo wao una walakini, wameanza kuhaha wakihofia kumwaga unga pindi dili zao chafu zitakapofichuliwa.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, uchunguzi huo umekuwa wa siri mno ili kutowashtua wahusika na kupoteza ushahidi.

Inadaiwa kuwa uchunguzi huo huenda ukanasa wengi kwani katika wizara mbalimbali dili kibao za ulaji pesa zimekuwa zikifanyika na kuhusisha baadhi ya vigogo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, hata hatua ya Serikali kukaribisha kampuni moja ya kimataifa ili kufanya ukaguzi wa hesabu za Benki Kuu (BoT) ni moja ya mikakati hiyo ya kunasa mafisadi.

Habari zaidi zimesema baada ya kampuni hiyo ya nje kukamilisha kazi yake, itatoa ripoti ambayo ndiyo itatoa mwelekeo wa nini kifanyike baada ya hapo.

Kadhalika, jana, Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa alizungumzia pia hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya nne katika kupiga vita rushwa na vitendo vya ufisadi.

Akizungumza wakati alipokutana na Balozi mpya wa Finland nchini, Waziri Mkuu Lowssa alisema Serikali imeshaitisha uchunguzi kabambe wa hesabu za BoT kwa kutumia kampuni ya kimataifa ili ikithibitika kuwa tuhuma za rushwa ni za kweli, hatua stahili zichukuliwe.

``Ripoti ya ukaguzi ikikamilika, Serikali itachukua hatua zinazostahili kwakuwa Serikali ya awamu ya nne imedhamiria kikweli kupambana na rushwa kwenye ngazi zote,`` alisema.

Source: Alasiri.

Kama haya ni ya kweli basi tutegemee kupoteza mawaziri wengi tu,pamoja na maswahiba wake,vinginevyo hakuna kitakachoeleweka,tutazidi kuwazomea tu,ikishindikana tunaingia barabarani kama wanavyofanya wenzetu huko BURMA.Hadi kufika december kama bado hakijaeleweka,lazima krismasi itakua chungu kwao.
 
huyu ndiye kiongozi asiyetufaa
1.Mwenye kupenda kufanya na kusema mambo ya mzaha
2.asiyejua Mambo ya Uchumi
3.Mkabila
4.Anayependa kujitarisha yeye na familia na marafiki zake
5.Mfisadi na anyekumbatia ufisadi
6.Mhuni
7.Mtu wa kupenda kusifiwa na asiyefuata utawala Bora
8.Asiyependa kupewa ushauri na wenzake
9.Mla Rushwa
10.Asiye na maono na mweleko wa uongozi wake

baada ya kusema hayo,
je unafikiri aliyetoa kauli hiyo ni kiongozi anayefaa?

Je unadhani watachukua hatua yeyote?hivi bado kuna mtu anasadiki maneno anayosema EL?mie huwa hata sitaki kumsikiliza sababu amekosa sabu za kuwa kiongozi anayefaa.
nachokifahamu mimi,wansubiri muda wa balali hapo december ukatike then wachague mchwa mwingine atutafute.

wanabodi naomba mtupe majina ya viongozi wengine wasiofaa,ili wananchi wawakatae 2010,

tena kwa kuanzia uchaguzi wa madiwani unaokuja,wana wa watanzania naomba msiwachugue viongozi wasioofa.

naomba kutoa hoja
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom