Serikali kuboresha mafunzo ya kukabiliana na uhalifu kwa JWTZ

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
jwtz(2).jpg



Serikali imesema itaendelea kuboresha mafunzo ya kukabiliana na uhalifu hasa ugaidi kwa Askari Wa JWTZ ili kuifanya Tanzania inakuwa nchi salama.

Waziri wa ulinzi na JKT Dr.Hussein Mwinyi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya askari kutoka nchi kumi duniani ya jinsi ya kukabiliana na uhalifu.

Dr.Mwinyi amesema kasi ya uhalifu duniani kwa sasa ni kubwa hivyo Tanzania kama taifa ni lazima ishirikiane na mataifa mengine kuidhibiti.

Mkuu Wa mafunzo hayo Brigedia Jenerali Yohana Maboko amesema kupitia mafunzo hayo Askari Wa Tanzania watapata utaalamu zaidi kutoka nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani jinsi ya kukabiliana na uhalifu kisasa zaidi.

Mafunzo hayo ya wiki mbili yamehusisha Askari zaidi ya mia mbili kutoka nchi kumi na taasisi tatu za kimataifa.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom