Serikali kubeba jukumu la mishahara ya wafanyakazi wa TAZARA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kubeba jukumu la mishahara ya wafanyakazi wa TAZARA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Aug 16, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  WAZIRI wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe amesema serikali itabeba jukumu la kulipa mishahara ya wafanyakazi Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA, baada ya wafanyakazi hao kucheleweshewa mshahara yao kwa kipindi cha miezi mitatu.

  Kauli hiyo imekuja baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kufikisha kilio chao kwa Waziri huyo kuwa wamekuwa wakiishi maisha ya kubangaiza kutoakana ucheleweshwaji wa mishahara yao.

  Akizungumza na wafanyakazi hao, kwenye ofisi za Shirika hilo (TAZARA), jijini Dar es salaam jana, Dk Mwakyembe alisema akiwa waziri wa wizara hiyo anawaahidi hatakubali kuona wanaishi bila kulipwa mishahara huku wakifanya kazikwa juhudi.

  Dk Mwakyembe alibainisha kuwa serikali imepokea kilio chao hivyo italipa sh bilioni1.3 kama mshahara wa miezi miwili kati ya miezi hiyo mitatu wanayodai kuanzia leo (jana).

  Aliitaja miezihiyo itakayolipwa kuwa ni pamoja na Juni na Julai ambapo amewataka viongozi wa Shirika hilo kutoa maelezo kuwa ni kwanini hadi sasa hawajalipa mishahara wafanyakazi hao.

  Akizungumzia madai ya wafanyakazi hao ya kutaka kung'olewa madarakani kwa Mkurugenzi Mkuu,Mbegusita Akashambatwa na Naibu wake, Damus Ndumbalo, alisema shirika hili ni la kimataifa linalohusisha nchi mbili hivyo maamuzi yake ni lazima ya husishe viongozi wa pande zote mbili.

  Aidha, alitoa onyo kuhusu vitendo vya hujuma ikiwa ni pamoja na wizi kuwa wale wote wanaojihusisha watambuwe kuwa dawa yao iko jikoni inachemka.

  Katika hatua nyingine amesema amesikitishwa sana kuona kuwa wafanyakazi wa Mradi wa Ukarabati wa Train Mijini, hadi leo hawjalipwa mishahara ya miezi miwili,fedha hizo lilikwishatengwa.

  "Nilisikitika sana kumkuta yule dada Mwanamisi akiwa amevaa overrol lake huku akiunganisha vyuma tena amefunga mfungo wa Ramadhani ambapo aliniambia tunafanyakazi lakini hatujalipwa mishahara inishangaza sana nataka walipwe haraka"alisema Dk Mwakyembe.

  Awali Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi shirika hilo, Ernest Kiwele, alisema wamechoshwa na tabia za viongozi hao kuwa wamekuwa chanzo cha matatizo yote yanayowakabili wafanyakazi hao.

  Alisema Mkurugenzi Mkuu na Naibu wake wamekuwa wakiendesha Shirika hilo kwa kujali zaidi maslahi yao na jamaa zao hata wale waliosimamishwa kazi kwa kuwalipa mishahara
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hii serikali bwana!!!!!
   
 3. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,094
  Likes Received: 1,477
  Trophy Points: 280
  tazara ni shirika la ubia kati ya tanzania na zambia hivyo mwakembe asitake kujipatia umaarufu na kusema serikali itabeba mzigi kama hizo pesa zinatoka mfukoni mwake kama ni swala la kutoa pesa inabidi serikali zote mbili zitoe au kama nyingine inashindwa kuchangia iuze hisa zake
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe, tembeza bakora kwa wakurugenzi wote Tazara. Kisha wafanye mahausi boi wako
   
 5. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hiyo kali kaka. mahausi boi tena. nacheka kama mkapa teh teh teh teh
   
 6. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,163
  Likes Received: 1,098
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  A statement issued by TAZARA's Head of Public Relations, Mr Conrad Simuchile, stated that the amount was the first instalment out of the 22.9bn/- approved and committed for that purpose in December 2009.

  "This announcement comes in the wake of the co-shareholding Government of Zambia having disbursed a total of ZK45.5 billion to TAZARA's account, for the Authority's recapitalisation and reconstruction as well as for payments of dues to retired workers, as agreed with their counterparts in 2009 and as provided for in the 2012 Budget," reads the statement.

  The Managing Director of TAZARA, Mr Akashambatwa Mbikusita-Lewanika has welcomed the development.
  "The 5bn/- from the government of Tanzania shall be welcome and very much needed step towards the fulfilment of the two shareholding governments' December 2009 promise to take over historically accumulated debts that cannot possibly be serviced from day-to-day revenues.

  "We are expecting the disbursement to be immediately availed and cannot wait for the balance that has been long out-standing since 2009," Mr Mbikusita-Lewanika said. Mr Mbikusita-Lewanika further said that there was still need for the two governments to complete the take over and liquidate the institution.
   
Loading...