Hali ni mbaya sana mitaani na anayebisha akapimwe akili, kwa sasa, wapo wananchi wanaoshindia mkate wa bakhalesa, wapo ambao siku inaweza kupita bila kula kabisa, nina uhakika na hilo, na katika hilo, niseme kwamba, hakuna nchi yenye watu wavumilivu kama Watanzania, si kwenye mambo ya kisiasa, haki zao n.k
Hakuna mwenye matumaini ya kesho na kama wapo ni hao walioko serikarini na wafanyabiashara wakubwa, nao hao wafanyabiashara wanawaza kesho itakuwaje maana bidhaa zimerundikana tu stoo, mitaani pesa hakuna, yaani ni mabalaa juu ya balaa
Wakati wazungu wakiendelea kutukopesha, sisi huku tunazitumbua tu bila kufahamu kesho itakuwaje
Tunaposikia nchi kama Lebanon zipo kwenye hatua mbaya kabisa ya kufilisika na hakuna taifa linalojitokeza kusema litasaidia kuinua uchumi wa nchi hiyo, mikopo na Misaada kwa sasa inaelekezwa kwenye nchi ambazo bado zina rasilimali ili mzungu badaye avune na kuwaacha mahohehahe
Kwani sisi hatuwezi kubana matumizi huku tukiendea kesho kwa tahadhari kubwa?
Je, tunawatu ambao kweli wanauwezo wa kuipima kesho itakuwaje ili kuishauri serikali au tunasubiri hali iwe mbaya zaidi kuliko sasa na kusababisha taharuki kubwa miongoni mwa jamii?
Hakuna vita mbaya kama ya kugombania chakula
Serikali iwe chonjo sana na mwelekeo wa dunia sasa!