Serikali kubali makosa acheni unafiki na ubishi kwa Lissu

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,646
2,000
Yaani serikali yetu inatakiwa kuangalia manufaa ya nchi kwa ujumla kwenye swala hili la Lissu kupigwa risasi.
1. Serikali imefanya makosa makubwa kwa wafanyakazi wake kujihusisha na shughuli za kigaidi hivi
2. Kuna Wafanyakazi wengi wa serikali ambao hawana hatia lakini wanaonekana kama wana support hizi njama.

Yaani mabalozi wetu waanze kufanya kazi ya kutetea swala ambalo lipo wazi wazi ni kuwavunjia heshma yao na ya nchi yetu. Tumekuwa na wafanyakazi wa serikalini wanaonekana kana watoto au wajinga kutetea swala hili ambalo haliwezi kabisa kulitetea kwa mtu mwenye akili timamu.

Maendeleo ya nchi kama kununua ndege, maji , madawati, kujenga zaanati na trini hazina uhusiano wowote na mwanasiasa kupigwa risasi. Hivyo wanaosema eti ukiongelea issue ya Lissu uongelea miradi wanakosea maana haya mambo ni tofauti.

Serikali kama kweli hili swala sio ustaarabu wetu basi tukubali makosa, ombeni msamaha kwa Watanzania, wahusika washitakiwe, Lissu apewe settlement zake zote za maumivu na nchi yetu iendelee na maendeleo. Bila hivyo hili swala litakaa kwa miaka na miaka na ku cost sana
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
10,114
2,000
February 11, 2019
Birmingham, Alabama USA

Dhana za kuchafua nchi,uzalendo na ubeberu

Tundu Antipas Lissu, Haonyeshi Kuwa na Chuki au Kumhujumu Yeyote, Kilio chake Ni kuona Kila Kiongozi Katika Tanzania anatenda haki na Kuheshimu Uhuru wa Mwananchi. Na anahamasisha Kila Mwananchi ikiwemo Viongozi wa Dini Kukemea Uovu.
Source : Thobias Marandu

1550001753399.jpeg

Frederick Douglass was an American social reformer, abolitionist, orator, writer, and statesman. After escaping from slavery in Maryland, he became a national leader of the abolitionist movement in Massachusetts and New York, gaining note for his oratory and incisive antislavery writings. Frederick Douglass | HISTORY
 
Katali

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
373
250
Tundu lisu ni chukizo kwa watanzania wengi ambao wanamkubali JPM na Serikali yake tuombe wasije wakatumia ile mbinu ya wananchi wenye hasira kali na kutuondoa kutoka watu wa kusadikika wale wasiojulikana akirudi apewe ulinzi na nchi za magharibi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
10,114
2,000
11 Feb 2019
Birmingham, Alabama USA
Imekuwa rahisi kumsema Mungu Tanzania kuliko Rais Magufuli
Aliyasema Hayo alipokuwa Akijibu Maswali ya Watanzania Katika Mji wa Historia ya Ukombozi wa Mtu Mweusi Marekani, Mji wa Birmingham AL.
Source : Thobias Marandu
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,925
2,000
Yaani nimeipenda speech ya Alabama ,Yaani amewakaanga kweli kweli wauaji ,maswali Yote tata ameyajibu kwa ufasaha kabisa ,nimegundua through those questions he is very intelligent .
Wengi hatukujua uwezo wake mzuri wa ufahamu wa mambo hadi sasa ambapo ameweza kuitumia 'platform' hii kuuonyesha bayana.

Ni jambo la kustaajabisha kidogo, kwa mtu aliyenusurika kifo kubaki 'stable' kiasi kile bila ya kuonyesha alama za uchungu na msongo mkubwa wa mawazo. Tukio lililompata amelichukuwa na kulifanya kama ni historia iliyobakia kuifanyia kazi ili isiendelee kutokea kwa wengine.

Magufuli atakapoamua kushughulika na yale mazuri tunayoyapenda sote, na kuyaacha yanayoleta simanzi kwenye taifa, bila shaka na yeye ataona kuwa kuna waTanzania wengi kama Mh. Tundu Lissu wanaoitakia mema Tanzania yetu na kila mmoja wetu anao mchango wa kuliendeleza taifa hili.

Hii haiwezi ikawa ni kazi ya mtu mmoja au kikundi fulani ndani ya CCM pekee.

Tuache kuwekeana lebo za 'uzalendo' au 'usaliti' kwa kutokubaliana tu katika baadhi ya mambo au utekelezaji wake na kufikia hatua za kuumizana kwa njia zozote ziwezekanazo.

Zipo sheria na taratibu tulizojiwekea katika usuluhisho wa mambo ambayo yanahatarisha taifa letu. Tuzitumie kikamilifu inapobidi kufanya hivyo.

Tanzania itaendelea kwa haraka zaidi kama tutatanguliza haki mbele ya yote.
 
PumziNdefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
566
1,000
Yaani serikali yetu inatakiwa kuangalia manufaa ya nchi kwa ujumla kwenye swala hili la Lissu kupigwa risasi.
1. Serikali imefanya makosa makubwa kwa wafanyakazi wake kujihusisha na shughuli za kigaidi hivi
2. Kuna Wafanyakazi wengi wa serikali ambao hawana hatia lakini wanaonekana kama wana support hizi njama.

Yaani mabalozi wetu waanze kufanya kazi ya kutetea swala ambalo lipo wazi wazi ni kuwavunjia heshma yao na ya nchi yetu. Tumekuwa na wafanyakazi wa serikalini wanaonekana kana watoto au wajinga kutetea swala hili ambalo haliwezi kabisa kulitetea kwa mtu mwenye akili timamu.

Maendeleo ya nchi kama kununua ndege, maji , madawati, kujenga zaanati na trini hazina uhusiano wowote na mwanasiasa kupigwa risasi. Hivyo wanaosema eti ukiongelea issue ya Lissu uongelea miradi wanakosea maana haya mambo ni tofauti.

Serikali kama kweli hili swala sio ustaarabu wetu basi tukubali makosa, ombeni msamaha kwa Watanzania, wahusika washitakiwe, Lissu apewe settlement zake zote za maumivu na nchi yetu iendelee na maendeleo. Bila hivyo hili swala litakaa kwa miaka na miaka na ku cost sana
Muhusika namba moja hapa ni Jiwe ndio maana serikali yote imepata kigugumizi.
Tunahitaji katiba mpya itakayo rahisisha uwajibishwaji wa majizi na wauaji kama Jiwe.
 
Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,646
2,000
Kubalini kama Iran maana hii inazidi kuchoma nchi kuna watu kotoka nchi nyingine wananiuliza kuhusu hili
 
Nyanjomigire

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
6,552
2,000
Muda unakuja kuna siku watu watapigwa mvua tu. Aliyekuwa dikteta wa Chile Augusto Pinochet aliburuzwa mahakamani zaidi ya miaka 20 baada ya kung'atuliwa madarakani kwa uovu aliyotenda alipokuwa rais.

Hivyo kwa kuwa matukio mengi hapa duniani yana "Precedent", hakuna kinachozuia historia isijirudie hata hapa Tanzania.

Walioko madarakani leo wakae wakijua kuwa, the situation won't stay the same always. There is a time when they will have to stand trial for the atrocities they committed to the now defenseless people of this country.
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
10,018
2,000
Tundu lisu ni chukizo kwa watanzania wengi ambao wanamkubali JPM na Serikali yake tuombe wasije wakatumia ile mbinu ya wananchi wenye hasira kali na kutuondoa kutoka watu wa kusadikika wale wasiojulikana akirudi apewe ulinzi na nchi za magharibi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata "Mo" ni chukizo kwa wanao mkubali Magufuli, japo kaendelea kuhishi katikati ya kundi limchukialo.
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,924
2,000
Muda unakuja kuna siku watu watapigwa mvua tu. Aliyekuwa dikteta wa Chile Augusto Pinochet aliburuzwa mahakamani zaidi ya miaka 20 baada ya kung'atuliwa madarakani kwa uovu aliyotenda alipokuwa rais.

Hivyo kwa kuwa matukio mengi hapa duniani yana "Precedent", hakuna kinachozuia historia isijirudie hata hapa Tanzania.

Walioko madarakani leo wakae wakijua kuwa, the situation won't stay the same always. There is a time when they will have to stand trial for the atrocities they committed to the now defenseless people of this country.
Hiyo ni kweli kabisa Mkuu Nyanjomigire

Hakuna chenye mwamzo kwenye dunia hii kikakosa kuwa na mwisho.......

Hawa watawala wetu wanajidanganya kuwa kwa kuwa wenyewe ndiyo wenye vyombo vyote vya dola, kwa hiyo wataficha udhalimu "waliomtendea" Lissu milele na milele

Ipo siku isiyokuwa na jina, wale wote waliofanya udhalimu ule wa kutisha, wataanza kulia na kusaga meno!
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,907
2,000
Wafahamu kuwa issue ya Lissu imevuka kiwango cha mpambano wao na Lissu au Chadema, this is next level!
Sasa hivi ni mpambano wao na Mungu. Jee binadamu aweza pambana na Mungu kwa silaha, ubabe au hoja?
Binadamu anapambana na Mungu kwa maombi na toba pekee.
Magu na serikali ya chama chake wajitokeze hadharani na kutubu kwa Mola, huku wakiweka ukweli hadharani na kuomba msamaha kwa Tundu na wananchi.
Vinginevyo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,924
2,000
Wafahamu kuwa issue ya Lissu imevuka kiwango cha mpambano wao na Lissu au Chadema, this is next level!
Sasa hivi ni mpambano wao na Mungu. Jee binadamu aweza pambana na Mungu kwa silaha, ubabe au hoja?
Binadamu anapambana na Mungu kwa maombi na toba pekee.
Magu na serikali ya chama chake wajitokeze hadharani na kutubu kwa Mola, huku wakiweka ukweli hadharani na kuomba msamaha kwa Tundu na wananchi.
Vinginevyo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Chakaza Iran imekiri kuitungua ndege ya Ukraine baada ya kukanusha kwa siku nne mfululizo.....

Sioni sababu kwa nini serikali hii ya Sisiem, isikubali yaishe kwa kukiri hadharani kuwa "wao" ndiyo waliohusika na shambulio lile baya kabisa, la kutaka kutoa roho yake Tundu Lissu

Kukiri makosa yako siyo udhaifu bali ni ujasiri
 
Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
759
1,000
Kosa la papa mkubwa,hawezi kukiri kwa by nature ana inferiority complex ni dhaifu sana. Sifa kubwa ya mtu asiejiamini ni muoga na muongo( he can't stand always right) he is weak. Hamuoni akifanya mwingine reaction anazochukua that seeks popularity from lumpen people and deadly praising? Ts easy to read him than understanding him
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom