Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,477
- 30,137
Kila mwananchi ameona utaratibu mpya ambao umeanzishwa na serikali hii ya awamu ya 6 ya kuanza kuzifanyia "monitoring" taasisi zote za dini na kuzisajili upya kila baada ya miaka 5.
Huu ni utaratibu mpya kabisa, ambao haujawahi kuwepo tokea nchi yetu ipate uhuru wake, miaka 60 iliyopita.
Ni utaratibu mpya ambao umekuwa "introduced" kwa mara ya kwanza na utawala huu wa awamu ya 6.
Siku za nyuma taasisi yoyote ya dini ilikuwa ikipata usajili wa "permanent" wakati wa kuanzishwa kwake.
Nini lengo la mpango huo mpya?
Ni wazi kuwa serikali hii ya ukandamizaji imeamua sasa kuingilia nyumba za ibada na kuzifanyia "monitoring" na kuwatisha viongozi hao wa dini na kuwafunga midomo.
Huo ni mkakati mmojawapo wa serikali ya ukandamizaji, kutaka isikosolewe na viongozi wa dini, pale inapokuwa haitendi haki.
Hii ni ishara ya wazi kuwa serikali hii sasa itaanza kupata laana ya Mungu kutokana na vitendo vyake vya mfululizo vya ukandamizaji wa haki za binadamu.
Moja ya jukumu kubwa kabisa la viongozi hao wa dini ni kusimamia haki na kukemea kwa uwazi pale inapoona haki hiyo haitekelezwi na viongozi hao wa serikali.
Ni wajibu wao mkubwa viongozi hao wa dini kukemea kwa nguvu zote maovu yanayofanywa ndani ya jamii na serikali yake
Kwa maana hiyo viongozi hao wa serikali wameamua kuwapoka mamlaka hayo, viongozi hao wa dini.
Vile vile viongozi hao wa serikali ni lazima wakumbuke kuwa wao hubeba vitabu vya dini, Biblia na Quaran wakati wa kuapishwa kwao na kuahidi kwa Mungu kuwa watawatendea haki wananchi wanaowaongoza Katika utekelezaji wa majukumu yao.
Swali la kujiuliza hivi hawa viongozi wetu wa kisiasa wanawatendea haki wananchi wao, kwa mujibu wa viapo vyao walivyoapa wakati tunawakabidhi madaraka hayo?
Imenenwa Katika Biblia Katika kitabu cha Mithali sura ya 14:34 "Haki huliinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote".