The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Serikali kuanzia July 1, 2020 ilifanya marekebisho ya sheria ya kodi ya mishahara (PAYE) na kutoa unafuu fulani kwa watumishi.
Naipongeza Serikali kwa maamuzi haya japo tunahitaji iende zaidi ya hapa kwa kuhakikisha inaboresha mishahara ya watumishi kwa kuiongeza kila mwaka.
Kama serikali imeweza kupunguza makato ya kodi ya mishahara (PAYE), tunaomba sasa ivielekeze vyama vya wafanyakazi kama Chama Cha Walimu (CWT), Chama cha wafanyakazi serikali za mitaa (TALGWU) nk navyo vipunguze makato haraka bila kuchelewa.
Mathalani Chama Cha Walimu (CWT) kinakata 2% ya mshahara wa kila mwalimu kila mwezi. Kishushe makato yake hadi 1%.
NHIF nao washushe makato yao hadi 2% toka 4% ya sasa.
Na wakati huohuo serikali nayo ihakikishe inaongeza mishahara ya watumishi wake haraka iwezekanavyo.