Serikali kuanika vigogo wa Madawa ya Kulevya bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kuanika vigogo wa Madawa ya Kulevya bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Feedback, Jul 2, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Serikali imesema wakati wowote kuanzia sasa itaweka bungeni hadharani mbinu na majina ya wanaodaiwa kuhusika na biashara chafu ya madawa ya kulevya, itawaeleza wabunge kwa njia ya semina elekezi.

  Je hii ni sinema ileile kwa kutumia mkanda tofauti au ni mpya kabisa.

  ===========
  NIPASHE:

  Serikali imesema itawaonyesha hadharani vigogo wote wa dawa za kulevya, akiwamo Kiongozi wa Kanisa la Lord Choosen Charismatic Revival, lililopo maeneo ya Kinondoni Biafara, aliyekamatwa na kilo 81 ya dawa hizo aina ‘Cocaine', maeneo ya Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema vigogo hao pamoja na kiongozi wa kanisa hilo, ambaye ni raia wa Nigeria, wataonyeshwa kupitia mkanda wa video katika semina itakayoandaliwa na serikali kwa wabunge.

  Waziri Lukuvi alisema hayo jana alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, kwa nyakati tofauti, katika Bunge la Kumi linaloendelea, mjini hapa.

  Alisema semina hiyo itafanyika katika kipindi cha Bunge na kuwaomba wabunge wote kuhudhuria ili waonyeshwe mambo yote yanayofanyika, wakiwamo watu wanaohusika na dawa za kulevya, aina ya dawa zilizokamatwa na mbinu zinazotumiwa na watu kuzitoa nje na kuziingiza nchini, soko lao pamoja na waathirika wote.

  Waziri huyo alisema tayari amekwishaiagiza Tume ya Dawa za Kulevya pamoja na Kikosi Kazi, kujiandaa vizuri kwa ajili ya kuendesha semina hiyo, ikiwa ni pamoja na kuwaonyesha wabunge vigogo hao, nyendo na soko lao la dawa za kulevya.
   
 2. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  source p/se?
   
 3. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sijui ila ukisikia usubiri kuona.
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
 5. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  whatever happened to presumption of innocence?

  whats the point ya kuwa na Mahakama na vyombo vya sheria?

  kuna kila dalili za mistrial hapa
   
 7. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kama polisi wanayo majina wanaogopa nini kuyataja ama kuwakamata watuhumiwa? Hii ni kiini macho tu
   
 8. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,173
  Likes Received: 1,175
  Trophy Points: 280
  Semina elekezi, madawa ya kulevya????????????????????
   
 9. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  Si waende mahakamani!
   
 10. S

  Sakane Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kama kuna evidence mhimili wa tatu Mahakama inafanya kazi gani? kwani wabunge ndio nani?
   
 11. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hii serikali yetu inaendeshwa kisanii, sasa majina yakiwekwa hadharani mwisho wake ni nini? Kama wanayo majina kwanini wasiende mahakamani? Maana hawawezi kumtaja mtu kama hawana ushahidi inaweza kuzaa kesi za kuchafuliwa majina na zikaigharimu serikali
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,168
  Trophy Points: 280
  Serikali iache kutuchezea akili, wauza unga wapelekwe mahakamani sio bungeni. Maana kuna baadhi ya wabunge nao ni vinara wa biashara hii haramiu.
   
 13. hKichaka

  hKichaka Senior Member

  #13
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata sisi tulikuwa tunajua kuwa mtu wa kawaida huwezi kuuza madawa ya kulevya ,,hii ni biashara ya vigogo tu angalia hata nchi ya kenya huwa ni vigogo tu ndio wanaouza haya madawa ya kulevya
   
 14. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  haha eti serikali itatoa SINEMA ELEKEZI.
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ponjoro.....Upo mbali na vyombo vya hbr wewe,
   
 16. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Ogopa zaidi ukisikia imetanganzwa mapema hivi kwani ndiyo KABISAAA HAITOTOKEA!! Hawa wazee wa madawa nao ni MIPAPA MINGINE MIKUBWA; nguvu yao ni kubwa kama MAFISADI PAPA. Watawabana mbavu wanaopanga kutangaza majaina yao na I CAN BET MY SHOES HAYATOTANGAZWA HAYO MAJINA..
   
 17. kongomboli

  kongomboli Senior Member

  #17
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Jamani hawa watu si walishasamehewa na jk tangu 2005 ambapo raia wema tulimpa rais majina yao naye akawasamehe pamoja na wale wa EPA akiwaomba waache mara moja!! Bunge linataka kumpinga jk boss wao!!
   
 18. B

  Babamwema Member

  #18
  Aug 18, 2015
  Joined: May 28, 2015
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sssshiiiittttt!!!!!! "" The Stupid System Of Leadershp, Wauwaji Wa Fahaham Za Wananch Masikini, Wauza Dawa Za Kulevya Wapelekwe Bungeni""" Hata Serkali Ya Hitler Haikufanyaga Uovu Wa Namna Hii
   
 19. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2015
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  Hee na hii ilikufa kimya illiondoka na amina chifupa maskini akamwacha lafahanina yatima
   
Loading...