Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Habari wanajamvi
Serikali imeanza mchakato wa kuboresha sheria ya kukusanya kodi ya magari inayoitwa Motor Vihicle au Road Licence ikiwa ni pamoja na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuhudumia wamiliki wa magari ambayo yatakuwa yamesimama kwa kipindi kirefu bila ya kutembea barabarani kwa sababu za msingi.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaju wakati akijibu swali la Mh Desderius Mipata Mbunge wa Nkasi Kusini aliyetaka kujuwa serikali inampango gani wa kuitizama upya sheria hiyo.
Dk Kijaju amesema kuwa sheria hiyo haitoi unafuu wowote kwa gari lililosimama kwa muda mrefu bila ya kutembea barabarani akaongeza kuwa utaratibu huo umekuwa unaleta adha kwa wamiliki wa magari na hasa pale ambapo kuna ushaidi wa kutosha kwamba gari husika limesimama kwa muda mrefu kwa sababu za msingi.
Akaongeza kuwa baada ya taratibu zote kukamilika mapendekezo ya mabadiliko ya sheria hiyo itapelekwa bungeni ili kujadiliwa na kuidhinishwa .
Chanzo: ITV