Serikali kuajiri zaidi ya Watumishi 43,400 Mwaka 2023/24

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,360
49,022
simachawene.jpg

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene akiwasilisha maombi ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2023/2024 leo bungeni jijini Dodoma

Haya Sasa Vijana mumeletewa tumaini. jipya na Rais Samia kazi ni kwenu 2025.

=====

Dodoma. Serikali imesema itatoa vibali vya ajira ili kujaza nafasi 43,464 zilizoidhinishwa kwenye mwaka 2023/2024.

Katika mwaka 2022/2023, Serikali ilitoa vibali vya ajira mpya 30,000 na vibali vya ajira mbadala 7,721 kwa waajiri kutoka katika taasisi mbalimbali vimetolewa.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Aprili 19, 2023 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene.

“Itashughulikia vibali vya ajira ili kujaza nafasi 43,464 zilizoidhinishwa katika Ikama,”amesema.

Amesema pia watahakiki na kuidhinisha madai ya malimbikizo ya mishahara na kusahihisha taarifa zinazohusiana na masuala ya kiutumishi na mishahara ya watumishi kwa taasisi 433.

Aidha watakagua orodha ya malipo ya mshahara katika taasisi 150.

Katika mwaka 2023/2024, ofisi hiyo imeliomba Bunge kuwaidhinishia Sh1 trilioni kwa ajili ya mafungu yake sita ya bajeti.

Mafungu hayo ni Ofisi ya Rais Ikulu, Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, na Sekretarieti ya katika Utumishi wa Umma.

Mafungu mengine ni Tume ya Utumishi wa Umma na idara ndogo ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom